Donald Bakari
Member
- Sep 4, 2020
- 32
- 30
Katibu Mkuu ameongea vizuri na kwa staha. Wagombea wanatakiwa kutekeleza majukumu yao barabara. Chama kimewaamini wanatakiwa kuwa mstari wa mbele kukipigania.Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally amemtaka Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamisi Kigwangalla kumzungumzia Mgombea wa Urais wa CCM, Dkt. Magufuli badala ya kuendelea na malumbano yake yanayohusu mpira dhidi ya Mmiliki wa Simba SC, Mohammed Dewji
Dkt. Bashiru amaema“Naona Hamis Kigwangalla yupo mitandaoni kujibizana na Mohammed Dewji mambo ya mipira, tupo kwenye uchaguzi. Nataka nione ana-tweet na wafuasi wake namna Mwenyekiti na Mgombea Urais wetu atakavyoshinda.”
Ameongeza, “Siingilii maisha binafsi, hakuna maisha binafsi unapokuwa mgombea wa CCM"
Dkt. Kigwangalla na Mo Dewji walianza kujibishana mtandaoni baada ya Kigwangalla kuhoji namna alivyopatikana CEO mpya wa Simba ambaye anaelewa kuwa PA wa Mo Dewji
Katika kujibu hoja hiyo Mo aliendelea hadi kumuomba msamaha Waziri Kigwangalla kutokana na mkopo wa pikipiki kutofanikiwa (hali iliyotafrisiwa kuwa Mo anadhani Kigwangalla anafanya hivyo kutokana na kunyimwa mkopo)
Hata hivyo, Kigwangalla aliendelea na kusema mkopo hauhusianj bali tu yeye anahoji kama Mwanachama wa Klabu ya Simba. Aliweka bayana barua pepe aliyoombea mkopo wa pikipiki na pia alionesha tweet zake za nyuma ambazo pia alikuwa a ahoji mambo kadhaa ndani ya Simba
Naamini wamemsikia na watafanyia kazi maelekezo haya.