Baada ya DR Congo kuingia EAC, sasa changamkieni fursa kama ifuatavyo

Baada ya DR Congo kuingia EAC, sasa changamkieni fursa kama ifuatavyo

Hivi issue za kuvuka border kazima uwe na nn
Passport, Yellow Fever Vaccination Card, Kwa Sasa pia Cheti cha Chanjo na Hati ya Kipimo cha Corona(sina uhakina kama inaapply same kwa kila nchi), na Visa kama hiyo nchi unahifaji visa
 
Achana na wakenya wenye elimu yenye tija walioanza kuwekeza kwenye mabenki na IT na kuanza kutafuta masoko ya bidhaa zao za viwandani na wamewekeza kwenye madini.
Achana na Watanzania wa taqwa na classic waliowekeza muda mrefu kwenye usafiri wa mabasi ndani ya DRC , je wewe mtanzania mjasiliamali mdogo mwenye mtaji wa kuunga unga ufanye nini Congo.
Tuigawe congo katika pande kuu nne kwa milango minne ya kupitia Tanzania.
1. LUBUMBASHI-
Hapa mpambanaji utaingilia Tunduma kwenda kasumbalesa then utavuka lubumbashi sasa lubumbashi wewe pambana upeleke vitu vifuatavo kwanza viatu raba, ukiweza nenda pale kariakoo david sports wear ongea nao wale jamaa wakuuzie bei chini zaidi beba pea kadhaa nenda nazo huko, vitambaa vya suti na batiki wewe beba tu utaenda kuuza, Kama uko vizuri peleka Nyama ya ng’ombe na mchele tani zozote unazoweza jua utaenda kuuza tu

2.KISANGANI-
Hapa mpambanaji utapitia Uganda kuelekea Bwera to Kasindi Border kwa ufupi hapo utakamata basi za link utapita Beni halafu kasindi mnatoka jioni mtaenda kulala Mambasa hapo utamkuta Said mnyamwezi wa Tabora aliyelowea huko ukisema wewe mbongo pale utaelekezwa mambo yote sasa huku kuna vyuo vingi huku stationaries, bidhaa kama nguo ambazo utachukulia tu kampala maana bei rahisi, kwa ufupi wanamahitaji mengi mno lakini hata maduka ya vifaa vya muziki , yaani vinanda na magita wanapenda sana hapo unaweza kufanya utafiti ukawa unabeba gita hata nne au tano ambazo ni kali za type yao nahakika ukiwauzia vizuri utkuja kupata order makanisa yao yote usuply hizo vifaa vya bendi na muziki,

3.-GOMA
Hapa mpambanaji utapitia Rusumo, utaingia Rwanda kigali pale utaingia nyabugogo kigali utapanda costa za kwenda Gisenyi baadhi ya makampuni ni Virunga na Volcano hapo utavuka kuingia goma na bidhaa nyingi zinaingiliana lakini kwa chap chap bidhaa za chakula hapo unaweza kupeleka dagaa wa ziwa victoria wale kauzu kuna jinsi ya kuwaandaa wanakua wa chumvi au unaweza kujitupa mafia, unguja au pangani ukibahatika kubeba wale dagaa nyama ukafikisha goma au lubumbashi kule juu mambo yako yatakua sio mabaya.

4.-UVIRA NA KALEMIE , MOBA
kwa ufupi sana hapo unaweza kupitia Kigoma, au Burundi ili kufika uvira na kalemie na moba huko utapitia sumbawanga njia rahisi huko sasa peleka mbuzi, nyanya, ndizi za kupika, viazi mviringo, mawese, dagaa wote hasa wale wa ziwa victoria Mnaita kauzu, batiki, hapa namzungumzia mpambanaji kama mimi asie na mtaji yaani vitu vya kukimbiza chap kukuza mtaji wako.

Kwa ufupi DRC unaweza kuuza chochote unachokijua kwa mfano ukifungua garage huko kwa mafundi ni pesa tupu, ukienda kuuza vifaa vya umeme kama solar onterior parts zao utauza , ukifungua hardware uuze vifaa vya ujenzi ni wewe najua wakenya watavamia hii ya hardware kama ilivowanufaisha sudan kusini, mafuta ya kula haya korie sijui masafi huko ndio penyewe, ukijenga ukumbi mzuri wa sherehe congo utapata pesa ni wewe kusoma location, haya maduka ya spare za magari na lubricants hapo kuna fursa ni wewe ukasome soko then ujiongeze, wazee wa kupimp magari ndio mahala pake.
Sawa lakini tatizo hakuna amani huko mkuu
 
Wabongo wanasema kuna vita!!. Vipi kwa wataalamu kama manesi, madaktari, wafamasia, waalimu, waahasibu nk wana soko huko?

Fursa ni nyingi upande huo wabongo kadhaa hasa wataalamu wa afya walipenya Botswana tu napo sio wengi huko DRC ukitafuta sehemu hata mkifungua dispensary, pharmacy au duka la madawa na mkawa vizuri mnajipigia tu pesa au ukienda kama mtaalamu kuna hata hospital na vituo vya afya vya mashirika ya umoja wa mataifa hasa maeneo yenye au yaliyoathirika na vita kazi zipo
 
Waha wamanyema usiwataje kwa sababu ni sehemu ya kongo, yaani blood brother kama masai TZ na Kenya au mjaluo TZ na Uganda na Kenya kwa kifupi huko ni kama kwao.
Hio fursa inakuwampya kwa makabika mengine kigoma walianza muda mrefu sana kufanya biashara huko ila changamoto ilikuwa usalama.
Mtoa mada amesahau fursa ya Usafiri wa majini na sabuni.
Kongo wanategemea sabuni TZ.
Lakini kuna kilimo, nasikia wana ardhi yenye rutuba sana.
Serikali ya Kongo ituhakikishie usalama tu kwa sababu wakongo aka banyamurenge hupora mali za Watanzia.

Waha naowazungumzia ni wale wa Kasulu wale ndio hardworkers kwenye kila kitu, wale waswahili wa kule mjini wamanyema, wabwali, wagoma wale sio hardworkers wana tamaduni kama watu wa maeneo mengine ya pwani uvivu uvivu lakini men muha wa kasulu trust me those guys
 
Hivyo vyote ulivyosema hata hapa bongo vinauzika na pesa ipo.
Formula ni ile ile, biashara inahitaji akili kubwa ili kuifanya. Kama bado akili sio kubwa hata ukienda huko utachemsha tu kwa kuwa sio kwamba wewe ndio unakua wa kwanza kuuza hvyo vitu.
Wauzaji wapo wengi, kufanikisha ni Kama nilivyosema

Kwenye kila population ya watu watahitaji mahitaji lakini Congo wanauhitaji wa hivo vitu kwa ukubwa sana na unapiga bingo kwenye chenji yaani inakulipa mara mbili kuliko ungeuzia bongo
 
moja ya kazi na jukumu la felix ilikua hili la kujiunga drc.ili kutanua uwanja wa fursa

niliandika humu mambo muhimu ambayo felix atafanya pindi akiingia ikulu moja wapo ni hili la eac
 
Hapo utawakuta wachaga, wapare, wanyakyusa, wakinga na waha hayo makabila wanatembea weka na mkulya, sasa waliowengi hawatembei eti wanaogopa kufa wakati hata akiwa kwao au kitandani atakufa tu
Kazi wanabakia humu wanaishia kulialia mara Sijui January, mgao umeme
Wanaulizia pesa za msaada
Vijana Sahv wamekuwa lonyalonya sana

Ova
 
hahahaha.
Wakati wa biashara ya skrepa bongo kuingiza huku ilikuwa Haina kwere
Tulipuyanga sana kongo na zambia
Nlikutana na mwana mmja yeye alikuwa anaenda na team yake anaxhinja machine za 1hz gari za UN zile anarudi na injin zake

Sasa watoto Sahv wao wanataka watafuniwe tu badala ya kupambana
Kivyao

Eti huko kuna machafuko kwani utaish milele

Ova
 
Back
Top Bottom