Baada ya DR Congo kuingia EAC, sasa changamkieni fursa kama ifuatavyo

Baada ya DR Congo kuingia EAC, sasa changamkieni fursa kama ifuatavyo

vita viko ukraine huko,drc hkn vita

watanzania wamezoea bure.ndo maana nchi inapiga sana mizinga (mikopo)

wananchi wamekalia porojo za simba na yanga.ccm na cdm

zikija fursa sababu zinaanza
Diamond harmonise kafanya nini

Waache uwoga na porojo

Utakuta mtu unampa ramani anabakia mwaka mzima anauliziaa kukoje huko
Badala ya kwenda akaone mwenyewe hali halisi

Ova
 
Wakati wa biashara ya skrepa bongo kuingiza huku ilikuwa Haina kwere
Tulipuyanga sana kongo na zambia
Nlikutana na mwana mmja yeye alikuwa anaenda na team yake anaxhinja machine za 1hz gari za UN zile anarudi na injin zake

Sasa watoto Sahv wao wanataka watafuniwe tu badala ya kupambana
Kivyao

Eti huko kuna machafuko kwani utaish milele

Ova
hahahaha. wanaogoqa kufa? dah dunia ya leo unaogopa kufa?

kwenye vita.mapigano.vurugu niko kule mashariki .wao waje katanga km vp
 
Mkuu Nina mtaji wa 3M hapo katanga nitafanya biashara ngapi kaka?
mkuu umesoma uzi vzr? drc kila kitu wanaagiza nje, kwanza nenda ukafanye tafiti ndogo

kwa mtaji huo kwa mfn unaeza peleka hata toilets paper.kule hawatumii maji chooni.kifupi unaeza uza chochote. huo ni mfn
 
Ona sasa mtu anaulizia vita
Hawajui kwenye machafuko kuna neema

Ova

Tuko nyuma sana mkuu ujue mtu wa namna hiyo anatafuta sababu ya kutotoka kwenda kutafuta chochote kitu nchi za watu
 
Achana na Wakenya wenye elimu yenye tija walioanza kuwekeza kwenye mabenki na IT na kuanza kutafuta masoko ya bidhaa zao za viwandani na wamewekeza kwenye madini.

Achana na Watanzania wa taqwa na classic waliowekeza muda mrefu kwenye usafiri wa mabasi ndani ya DRC, je wewe Mtanzania mjasiliamali mdogo mwenye mtaji wa kuunga unga ufanye nini Congo.
Tuigawe congo katika pande kuu nne kwa milango minne ya kupitia Tanzania.

1. LUBUMBASHI
Hapa mpambanaji utaingilia Tunduma kwenda kasumbalesa then utavuka lubumbashi sasa lubumbashi wewe pambana upeleke vitu vifuatavo kwanza viatu raba, ukiweza nenda pale kariakoo david sports wear ongea nao wale jamaa wakuuzie bei chini zaidi beba pea kadhaa nenda nazo huko, vitambaa vya suti na batiki wewe beba tu utaenda kuuza, Kama uko vizuri peleka Nyama ya ng’ombe na mchele tani zozote unazoweza jua utaenda kuuza tu

2. KISANGANI
Hapa mpambanaji utapitia Uganda kuelekea Bwera to Kasindi Border kwa ufupi hapo utakamata basi za link utapita Beni halafu kasindi mnatoka jioni mtaenda kulala Mambasa hapo utamkuta Said mnyamwezi wa Tabora aliyelowea huko ukisema wewe mbongo pale utaelekezwa mambo yote sasa huku kuna vyuo vingi huku stationaries, bidhaa kama nguo ambazo utachukulia tu kampala maana bei rahisi, kwa ufupi wanamahitaji mengi mno lakini hata maduka ya vifaa vya muziki , yaani vinanda na magita wanapenda sana hapo unaweza kufanya utafiti ukawa unabeba gita hata nne au tano ambazo ni kali za type yao nahakika ukiwauzia vizuri utkuja kupata order makanisa yao yote usuply hizo vifaa vya bendi na muziki,

3. GOMA
Hapa mpambanaji utapitia Rusumo, utaingia Rwanda kigali pale utaingia nyabugogo kigali utapanda costa za kwenda Gisenyi baadhi ya makampuni ni Virunga na Volcano hapo utavuka kuingia goma na bidhaa nyingi zinaingiliana lakini kwa chap chap bidhaa za chakula hapo unaweza kupeleka dagaa wa ziwa victoria wale kauzu kuna jinsi ya kuwaandaa wanakua wa chumvi au unaweza kujitupa mafia, unguja au pangani ukibahatika kubeba wale dagaa nyama ukafikisha goma au lubumbashi kule juu mambo yako yatakua sio mabaya.

4. UVIRA NA KALEMIE, MOBA
kwa ufupi sana hapo unaweza kupitia Kigoma, au Burundi ili kufika uvira na kalemie na moba huko utapitia sumbawanga njia rahisi huko sasa peleka mbuzi, nyanya, ndizi za kupika, viazi mviringo, mawese, dagaa wote hasa wale wa ziwa victoria Mnaita kauzu, batiki, hapa namzungumzia mpambanaji kama mimi asie na mtaji yaani vitu vya kukimbiza chap kukuza mtaji wako.

Kwa ufupi DRC unaweza kuuza chochote unachokijua kwa mfano ukifungua garage huko kwa mafundi ni pesa tupu, ukienda kuuza vifaa vya umeme kama solar onterior parts zao utauza , ukifungua hardware uuze vifaa vya ujenzi ni wewe najua wakenya watavamia hii ya hardware kama ilivowanufaisha sudan kusini, mafuta ya kula haya korie sijui masafi huko ndio penyewe, ukijenga ukumbi mzuri wa sherehe congo utapata pesa ni wewe kusoma location, haya maduka ya spare za magari na lubricants hapo kuna fursa ni wewe ukasome soko then ujiongeze, wazee wa kupimp magari ndio mahala pake.
Usiwastue waache waendeleee kulaumu Samia na Serikali 😀😀
 
Kazi wanabakia humu wanaishia kulialia mara Sijui January, mgao umeme
Wanaulizia pesa za msaada
Vijana Sahv wamekuwa lonyalonya sana

Ova

Kabisa mkuu kile kizazi cha watu wa Songea waliokua wanazamia machimboni msumbiji na kurudi kwao kujenga majumba hakipo au kile kizazi cha watu wa lindi na mtwara kilichokua kinavuka boda ya tangazo kupeleka ngano na redbull msumbiji kilishapotea saa hizi tuna walalamikaji wa Taifa, Ujasiri kwa watanzania umeisha kabisa
 
Wakati wa biashara ya skrepa bongo kuingiza huku ilikuwa Haina kwere
Tulipuyanga sana kongo na zambia
Nlikutana na mwana mmja yeye alikuwa anaenda na team yake anaxhinja machine za 1hz gari za UN zile anarudi na injin zake

Sasa watoto Sahv wao wanataka watafuniwe tu badala ya kupambana
Kivyao

Eti huko kuna machafuko kwani utaish milele

Ova

Acha kabisa malawi na zambia kulikua na vitu vya maana, wao ilikua landcruiser ikisumbua kidogo wanapaki yaani mafundi walikua hawana hivo wanauza kama chuma chakavu fasta wabongo waliotea hadi magreda huko, spare used ziliingia bongo kama chuma chakavu, respect kwa wana wote waliopuyanga enzi hizo
 
Wkt huo m23 wanacheka tu ihiii hiii hiiiiiiiiiii , wanasema waleteee

Nakupa hii hapa, niliwahi kwenda kuwauzia m23 buti za kijeshi nilizitoa kwenye mitumba nyeusi na zile za kaki kuzipitisha nilinunua udaga maeneo ya masumbwe tani kumi nikafunika vizuri nikazama rwanda, goma hadi maporini kwao vile viatu nilikusanya pea za kutosha hakuna iliyozidi elfu 30 jamaa walinunua kwa laki na 20 , kila pea nilikua navuka na kifuso kama napeleka udaga kumbe udaga kizugio tu sasa acha uoga dogo kapambane, nimekuthibitishia hata hao waasi watu tulifanya nao biashara
 
Kwani unafikiri watu hawajawahi onana nao
Nendeni acheni uoga kamateni fursa

Ova

Nimemuelezea chini kisa changu cha kuonana na hao waasi kwenye pori fulani mbele ya Goma, tatizo watu waoga sana basi tu
 
Sasa ndo uelekeze njia nzuri ni ipi ya kwenda .
Suala la usalamatwa mtu linatakiwa liwe kipaumbele Cha kwanza SIO FURSA.
HAKUNA maduka ya kuuza uhai
Vita ipo lakini sii maeneo yote yana vita ukianza kuwaza hivo hutovuka border
 
Back
Top Bottom