Hawa watu wanamuombea JPM kuliko hata Nyerere. Nadhani hii imekaa kimkakati ili kupandikiza hisia za udini katika jamii, hasa ukizingatia hawa jamaa huwa hawaridhiki nchi ikiwa na uongozi tofauti.
Kinamna wanawapanga waumini wao na wanataka kujigeuza jimbo la uchaguzi.
Busara ya kawaida tu inataka kwamba, baada ya taifa na familia kumaliza maombi chato, haingekiwa na haja ya hawa watu kuzinguka nchi nzim, kwa zamu, kwa unafiki, wakijifanya kufanya maombi, wakati ratiba ya Chato walikuwa nayo
View attachment 2939575
hili kanisa la mpinga Kristo, imagine, barua nzima inatangazwa na dhehebu kumuombea marehemu, lakini hawajaweka mstari wowote wa Biblia to back up their activity. ilitakiwa waseme, siku fulani tutamwombea marehemu fulani au misa kwa ajili ya mtufulani kwa mujibu wa kitabu fulani cha Biblia. kiufupi ni kwamba, hakuna mstari wowote kwenye Biblia unaoruhusu kuombea wafu au kuomba kwa wafu. Mtu akishakufa, kilichobaki kwake ni hukumu tu aidha aende motoni au uzimani, ninyi mlioko hapa duniani hata mumuombee namna gani mnapoteza muda wenu, yeye alitakiwa kutubu alipokuwa mzima.
hata akili ya kawaida tu, kama kungekuwa na kuombewa baada ya kufa uwekwe mahali pema, kusingekuwa na wito wa kuokoka au kumpokea Yesu, kwasababu hata ukifa na dhambi hasa wewe uliye maarufu au tajiri, ungeita tu padre akuombee usamehewe dhambi huko uendako. Yesu angesemaje sasa tukeshe na kuwa tayari? hata usipokuwa tayari si watakuombea ukifa?
Kanisa katoliki limepotosha wengi hadi hawataki kuokoka kwasababu wanalitegemea litawaombea wakifa. hili pia limefanya mapadre kuwa miungu watu, usipoenda jumuiya wanasema hatutakuzika, au hatutakuombea misa kama hizi, yaani wao ni kama wamejipatia mamlaka ya aidh akuingiza mtu mbinguni au kumzuia asiingie, jambo ambalo kwenye Biblia halipo. watu wengi wanashindwa kuokoka wakiogopa hawataombewa, mnapotoka.
Kanisa hili sio lile la mitume, shetani alishaingilia kati akalichuja. ukichukua kanisa la kitabu cha Matendo (ambalo ndilo kanisa la mitume) ukalinganisha na hili la sasaivi, hakuna hata vinavyolingana, siasa na serikali za wafalme wa dunia ziliingilia kati zikaliharibu kabisa. USHAURI WANGU KWENU WAKATOLIKI, nafasi ya uzima Mungu amewapatia, itumieni kwanza kabisa kwa kulikimbia hilo dhehebu, lipo kinyume na Neno la Mungu, pili, mnatakiwa kuokoka, Kitabu cha matendo chote kimeiimba kuokoka, muokoke ili msiende jehanum, dhehebu lenu limewaweka watumwa na mpo kifungoni, hamumuoni Mungu maishani mwenu na bado mnasali hapo, kwa kifungo cha kuzikwa na kuombewa mkifa, mnakataa wokovu na vipawa vyote vya Mungu, mnang'ang'ania dhehebu, Mungu anawaonya mbadilike, mngali na nafasi.
Ufunuo 14:13 inasema,
Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, andika, heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao, kwa kuwa matendo yao yafuatana nao.
hapo mwishoni anasema, "
matendo yao yafuatana nao", manake, yale uliyoyatenda duniani ndiyo yatakayokuchagulia wapi uende ukifa, motoni au uzimani.
Waebrania 9:27 inasema,
Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu.
Ndugu zangu, Biblia imeweka wazi, heri wafu wafao katika Bwana maana wataenda na matendo yao, Msipoteze muda kwenda kumuombea magufuli, siku ile anakufa ndio ilikuwa deadline yake hapa duniani ya kutengeneza na Mungu,kama alifanikiwa kutengeneza na Mungu kwa kutubu dhambi, heri yake, ila kama hakutengeneza, alienda na matendo yale yaliyoishia siku ile alipokufa. vivyo hivyo hata ninyi mkifa ndio deadline ya kutengeneza na Mungu. HAKUNA MWANADAMU ATAKAYEKUOMBEA ukifa usamehewe, hayupo, unasamehewa kwa kutubu dhambi, haujatubu unaenda na matendo yenu. hili suala la kuombea wafu ati Mungu awaweke pema, ni la kishetani na lengo ni kutaka watu wabaki katika dhambi wakitegemea kanisa litawasaidia kutubu dhambi wakifa, jambo ambalo ni la uongo na shetani amewakamatia hapo. ukifa unaenda na matendo yako, na baada ya kifo kinachofuata ni hukumu.