Wanabodi,
Kama kawaida yangu ya kuwaletea trends mbalimbali, leo naomba niwaletee hii trends za kinachoendelea kwenye hii issue.
Baada ya IGA ya DPW na Bandari Zetu, HGA yake iko njiani inakuja!
Naomba kukiri nimekuwa inspired kupandisha bandiko hili kwa bandiko la mwana JF huyu.
Mkuu
utukufu mwanjisi , kwa ruhusa yako, naomba kuitumia hoja yako hii kama mbegu ya kuoteshea bandiko langu fulani.
Baada ya IGA ya DPW na Bandari zetu kusainiwa na Mhimili wa serikali yetu Tukufu, licha ya kuwa na mapungufu lukuki ya kisheria, ikiwemo illegality on the capacity of Dubai to contract an international Treaty, ikapelekwa Bungeni na kuridhiwa na Mhimili wa Bunge letu Tukufu, hivyo hivyo ilivyo without any reservations, na Mhimiliwa Mahakama ukatoa baraka zake za the Separation of Powers, bila Checks and Balance, ya kutoliingilia Bunge, kinachoendelea sasa ni maandalizi tuu ya HGA.
Kwa kawaida HGA zinakuwaga ni confidential, lakini kufuatia sintofahamu nyingi za hii IGA, tuiombe serikali yetu Tukufu, kufanya a maximum transparency kwenye hii HGA ya DPW na Bandari zetu, isiwe confidential as it used to be, iwe open ili wale wote waliopinga IGA kwa hoja za kisheria, waridhishwe kuwa hoja hizo zimezingatiwa kwenye HGA.
The chronology of events ni
1. Kikao kijacho cha Bunge, kitaibadili ile sheria ya Magufuli ya ulinzi wa Rasilimali za Taifa, ili to accommodate HGA ya DPW na Bandari.
Hizi HGA takes time, mfano mpaka sasa HGA ya mradi wa gesi wa LNG bado haijasainiwa, ila mnaweza kushangaa HGA ya DPW na Bandari zetu ikatoka fasta.
Wale wote mlioipinga hii IGA kwa hoja za kisheria, hoja zenu zote zitakuwa zimezingatiwa kwenye HGA.
The issue ni moja tu, jee HGA ya DPW na Bandari zetu itakuwa open kama hii IGA?.
Mungu Ibariki Tanzania.
Paskali