Kwenye chanjo serikali imechemka big time.
Juzi wizara ya afya imesema kwa mwezi mmoja ama siku 32 watu 304,000 ndio walikua wamechanja, kwa maana kua ndani ya mwezi mmoja chanjo ni 33% tu zimetumika.
Kwa hesabu ya haraka chanjo milioni za msaada zitahitaji miezi 3 kumalizika wakati hizo chanjo haijulikani zilizalishwa lini hadi kufika Tanzania na hadi kumalizika zitakua na miezi mingapi, watu watapewa expired shots.
Iwapo mpango wa covax ni kutusaidia chanjo milioni 12, maana yake tutahitaji miezi 36 kuzimaliza hizo chanjo za covax, miaka 3 na ushee. Na wataalam wanashauri ili kujihakikishia ulinzi angalau uchanje 70% ya raia wako, kwa Tanzania ni kama milioni 40, hiyo tutahitaji miaka 10 kumaliza kuchanja 70% ya raia wote.
Hesabu za chanjo zinagoma, tumeingia mkenge wa kukubali kukopeshwa trilioni 2 za kununua madawa ya chanjo lakini iko wazi huu ni usanii.