Uchaguzi 2020 Baada ya kauli ya Mwigulu Nchemba kuhusu kuficha takwimu za maambukizi ya COVID-19, Kitila Mkumbo asema kauli hiyo ni ya mtu mjinga

Uchaguzi 2020 Baada ya kauli ya Mwigulu Nchemba kuhusu kuficha takwimu za maambukizi ya COVID-19, Kitila Mkumbo asema kauli hiyo ni ya mtu mjinga

Kinyang'anyiro cha ubunge October 2020 huko Singida kimechukua sura mpya leo baada ya Kitila Mkumbo kumpiga kijembe cha wazi hasimu wake Mwigulu Nchemba dhidi ya kauli yake ya jana kuhusu kuondoa transparency kwenye utoaji wa takwimu za maambukizi ya virusi vya korona Tanzania.

Tukumbuke watu hawa wawili (mmoja akiwa ni kipenzi cha baba huku mwingine ni "outcast") wanatajwa kuwania jimbo moja la ubunge huko mkoani Singida.

Movie imefika patamu, baki hapo hapo usiondoke kwenye screen.

Nilimdharau sana huyu Dr kama mtu mwenye elimu ya PHD hapa Tz anaweza ku reasons kama mtoto wa kindergarten .......elimu yetu ni janga kubwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
nadhani mwigulu hajaeleweka ila ana hoja nzuri,nilichomuelewa ni kwamba anahisi walioambukizwa ni wengi hivo anaona ni bora tutangaze vifo na waliopona kutokana na kwamba hatupimi watu wote
naweza nisiwe sahihi lakini kwa nilichoelewq
Wakiwa wengi na kutangazwa si tutajua ukubwa wa tatizo?urais unamsumbua Mwigulu
 
Mwigulu amezoea kuficha taarifa.. anayo mengi ameyaficha. Hili ni namna anavyojionyesha ni mtu wa namna gani.

Hatimaye amejifunua. Karma is a .....na bado.

Sent using iphone pro max
 
kwanini usiandike hoja yako kama ni kueleweshana tueleweshane ? tatizo la members wengi humu hamjui kujenga hoja,jf ipo kwa ajili ya watu kutoa mijadala na kuelimishana na kukosoana
nachokiona hapa unajidai wewe ni muelevu lakini hakuna unachokijua mkuu,soma comment yangu nimesema kabisa kwamba nilichokisema sina uhakika kabisa kwamba ni sahihi
Huna uhakika ndio nimekuambia " kama " ingekuwa mtihani Dr Mwigullu Nchemba angekupa sifuri.

Nchemba aliongea kwa ufasaha kabisa pale bungeni na hata ukifuatilia comments humu utajikuta wewe peke yako ndio una uelewa tofauti!
 
Umkate mwiguru umuweke kitilia??

Itakuwa ni kitonga ya kushuka hii sio kupanda.

Na kwa dalili hizi kitila ameshapoteza tayari.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tangia Jana nilisema Mwigulu ni mtu asiye na sifa za uongozi, sijui alifikaje level za uwaziri
Kujipendekeza hakujawai kumuacha mtu salama, dunia nzima inatoa takwimu, sisi ni nani? Yawezekana zikawa kweli au si kweli lkn wananchi kupata takwimu ni haki yetu zinatusaidia kuchukua tahadhari zaidi
 
Kwani hapa Tz kazi ni ubunge tu.

Maana Mwigulu yuko sahii wanauomwa wako 1000+ vifo viko 37 mwigulu anaona kuhusu Ugonjwa wanaficha sana. Bora kuficha iwe halali
 
Kwani hapa Tz kazi ni ubunge tu.

Maana Mwigulu yuko sahii wanauomwa wako 1000+ vifo viko 37 mwigulu anaona kuhusu Ugonjwa wanaficha sana. Bora kuficha iwe halali
Mkuu hao wanao kufa na kurona ni kuku au...!, kuna ndugu yako amekufa na corona hajatangwaza maana hutajisikia mtu anasema baba yangu alikuwa na corona kafariki na hajatangazwa...!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa kauli hiyo pia Mkumbo ana ujinga wa aina fulani. Hajitambui kwa nafasi yake ni nani ktk serikali: mtendaji wa wizara yeoyote wa kiwango hicho na nafasi hiyo hawezi kimbilia twitter kuandika maneno kama hayo ambayo ni ya binafsi kabisa!
hajaongea kama mtumishi wa idara ya maji kaongea kama kitila

Sent using Jamii Forums mobile app
 
N
Kinyang'anyiro cha ubunge October 2020 huko Singida kimechukua sura mpya leo baada ya Kitila Mkumbo kumpiga kijembe cha wazi hasimu wake Mwigulu Nchemba dhidi ya kauli yake ya jana kuhusu kuondoa transparency kwenye utoaji wa takwimu za maambukizi ya virusi vya korona Tanzania.

Tukumbuke watu hawa wawili (mmoja akiwa ni kipenzi cha baba huku mwingine ni "outcast") wanatajwa kuwania jimbo moja la ubunge huko mkoani Singida.

Movie imefika patamu, baki hapo hapo usiondoke kwenye screen.

Nipo hapa ktk flat screen yangu nacheki hili picha ndugu zangu,ila vumbi jingi sana sura bado hazionekani vizuri.
 
Hii ndio PhD ya ukweli bhana!
PhD ya upuuzi ilyonunuliwa kwa cheo na kuisaliti demokrasia. Hawa wote ni wa Ma PhD ya majalalani tu.
Halafu huyu si ndiye mtetezi mkuu wa PhD hafifu ya bwana yule dhidi ya Ben Saanane!!!
Kwani PhD ya Mwigulu Ni ya chuo kipi? Kama Ni UDSM basi Ben akifufuka tutajua mengi yamhusuyo Kitila Mkumbo!!!
 
Kuna Uzi moja unaohusu siasa za jimboni mwao niliwaambia tatizo ni kabila lao
Ona Leo wanamzodoa mwenzao siwangemwita pembeni wamwambie kinyiramba?

Iza mkunza mbwanee we
 
Back
Top Bottom