Baada ya kauli ya Mzee Kikwete ningekuwa Mbunge wa Mbeya ningefanya haya

Kilimanjaro na sasa Chato mamlaka gani inawafanya wajenge nyumba Bora na nzuri?
Kwani wasimamizi wa Mipango miji Kilimanjaro, Chato, Mbeya n.k ni walewale? Ni sawa na kufananisha utendaji kazi wa mamlaka za maji safi na taka toka maeneo tofauti.

Mfano angalia hapa anatajwa nani?
 
Mbeya ni kijiji kikubwa
 
Mbeya ni kijiji kikubwa
Na ndio definition halisi ya mji, manispaa na majiji.

Eneo kulifanya Jiji hawaangalii Sanga kajenga ghorofa ngapi au fulani hapendi. Kuna vigezo vya chini.

Shida watanzania akisikia sehemu fulani inaitwa jiji anataka ifanane na New York au mji anaoukubali yeye. Mbona hata darasani wanafunzi wanafunzi wanaosemwa wamefaulu sio wote watafanana marks bali watakuwa wamefikisha kiwango cha chini cha alama za kufaulu. Ondoa dhana ya kuweka kigezo cha mji kwamba mji husika wapaswa kufanana na mji fulani uupendao ili hilo eneo likidhi hadhu ya kuitwa jiji.

Tunatumia vigezo tulivyojiwekea kama minimum requirement.
 
Sio lazima kuwa na Ardhi kubwa Lord Denning... cha msingi ni kwamba hiyo waliyopewa wataitumiaje... siku hizi madarasa hufanyika hata mitandaoni, wajenge tu magorofa sehum hiyo ya ekari 50 hata ikibidi design ya lile gorofa la Dubai, watoto watasoma tu.. hii habari ya kutaka ekari zaidi ya 100 ni uchuro mtuou wa namna yake... hivi wanakwenda kusoma au kupunga hewa? wanataka wawe na misitu halafu mabinti waendelee kutoa kinyama ugomvi ili hali Salma kikwete mwenyewe amesema hakubaliani na wajawazito kurudi shuleni ? Kauli ya Kikwete ni kukataa kiana au kinamna jinsi ya kuendeleza campus ya Mbeya kwa kisingizio hafifu.. si wakubali tu hizo 50 na waendelee kuongeza kadri ya mahitaji au shida iko wapi?
 
Una ushauri mzuri ila uwasilishaji wako una walakini, umejaa kejeli na tambo zisizo na maana yoyote. Mbaya zaidi una hasira na mbeya na wanambeya.

Mbeya inalisha mikoa mingi na nchi jirani kwa mazao yake adhimu kabisa. Mbeya watu wake ni wakarimu mno tofauti na upotoshaji wa mleta uzi.

Kuhusu miundombinu kama hiyo barabara anayosema ni kweli ina njia moja lakini kwa sasa imeboreshwa kwa sasa kuna njia 3 na sio mbili tu kama uyo jamaa alivosema. Ni kama baadhi ya barabara nyingi za dsm zenye foleni kiasi zilivyo.

Barabara za mitaani ni full mkeka, eti hawajui kujenga daah we jamaa una chuki na mbeya sio bure na nadhani ulikuja ukakaa wiki tu ukasepa.

Kwa mfanyakazi alieajiriwa kwa mashahara wowote ule basi mbeya ni mahali sahihi kwako kuishi, utaenjoy mnoo.
 
Hata yeye ni tatizo pamoja na ndugu zangu CCM
 
Njoo tuishi mbeya baby tule maparachichi
 
Ukweli mchungu...

Tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...
 
Kwa Rais kabisa au kwa mawaziri ambao wizara zao zinamiliki maeneo makubwa mjini bila kuyaendeleza
 
Lord denning mada yako ni ya kipuuzi sana na Mbeya hujui japo unadai umekaa na kufanya kazi kule.

Mbeya unayoiponda ni Moja kati ya mikoa 5 yenye GDP ya juu katika mikoa 26 ya Tanzania. Kwa taarifa yako hakuna mwanachi wa Mbeya anayekufa njaa. Hakuna omba omba waliopo mikoa yote Tanzania.

Kuhusu miundombinu kuwa mibovu, usiwalaumu watu wa Mbeya kwa vile wao jukumu lao ni kutoa kodi na kuzalisha uchumi. Wa kumlaumu ni Serikali ya CCM kutofanya maboresho hasa kipindi cha JK 2005-15 kwa vile waliona watampa umaarufu Mwandosya aliyekuwa mmoja wa wagonbea watarajiwa wa uRais. Na miaka 2015-20 Magufuli aliapa kuwa hapeleki maendeleo kwenye majimbo yenye wabunge wapinzani.

Bado status ya watu wa Mbeya iko juu kuliko wa Dodoma wanaojengewa jiji au wa Chato waliopelekewa miundombinu mikubwa
 
Mbaya kutokuwa na njaa hakuondoi ukweli kuwa ni sehemu ambayo watu wengi hawajui namna ya kujenga nyumbq Nzuri na Bora!

Hakuondoi ukweli Pia kuwa watu wa Mbeya hamjui maana ya mipango miji na mkoa wenu umejaa uchafu na ujenzi holela na wa hovyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…