Naumuona kabisa mheshimiwa Kikwete akimtia nguvu Mama na kumpa miongozo sahihi ya kutuvusha. nimeamini usiwatukane mamba kabla hujavuka mto.
 
Lukuvi na makashfa yote hayo , halafu ngumbaru...
 
Wazo lako liko sawa,ila haukuzingatia yafuatayo:
1.Gharama.
2.Nafasi ya kutekeleza.
3.Maslahi ya Chama kimoja kimoja.
NB: Kifo si nafasi ya kujinufaishia
R.I.P Magufuli,JP
Mkuu gharama sio kitu katika kurudisha nchi kwenye mstari,gharama ngapi tumeona zikitumika hata katika vitu ambayo havina maana?
Kusema msiba sio kutafuta ulaji au nafasi za uongozi ,ukisema sijaangalia maslai ya chama kimoja kimoja unakosea ,hapa ni taifa kwanza Mambo mengine badae, ccm ina watu vyama vya upinzani vina watu , Sasa kuwaleta pamoja ni kufanya hivyo.

Kuvunja bunge KWA rais ajaye hakiepukiki, ili kupata bunge imara la kumsaidia huyu mama, sio la Sasa ,narudia sio Hili, tunataka nchi mpya na mshikamano mpya Kama taifa ambao imevurugwa vya kutosha
 

Nchi ilifilisiwa mpaka kuuza TWIGA!! Madini kama Tanzanite yalikuwa yanaporwa kama watu walikuwa hawana akili nzuri; Dhahabu zilikuwa zinachukuliwa tu; pembe za ndovu zinaporwa tu!!! Uchumi ulikuwa wa watu kuuza madawa ya kulevya. Na huko ndiko wanakotaka kuirudisha nchi kwa kumuweka NCHIMBI kama makamu wa Rais.
 
Nchi ilikuwa vizuri na itaendelea kuwa vizuri. Hakuna awamu isiyo na chamgamoto.
 
Luna jembe 1 lipo kule mkuu wa mkoa wa Geita...ngoja kwanza apewe umakamu wa Rais alafu mtakuja hapa kunishukuru badae
 
Mnawaza vyeo na madaraka mwanzo wa msiba huu ni uchuro kwa watu wasio na maadili.

Ninyi chama tawala msipojitathimini kwa mtindo huu inawezekana mkapoteza uhalali wa kuungwa mkono mwaka 2025....hili ni onyo mkishupaza shingo mtavunjika mkijiona mchana kweupe huku hamuamini kilichotokea.
 
mataga ni nini mkuu, huwa naliona sana
MAKE TANZANIA GREAT AGAIN hichi ni kikundi cha vijana fulani walijipambanua kuwa watetezi wa Mh Magufuli kwa lolote lile, kwa staili yao ya kuatack kila aliyekwenda kinyume na Rais walijipatia fedha nyingi sana, wakawa viburi na jeuri, dharau zao hazikuwa na mipaka kwani walidharau mpaka vigogo wa chama kama mzee Kinana, Makamba na wengineo, nilisikia sehemu hata baadhi ya mambo ya utekaji na kudhuru walishiriki pia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…