Poleni sana Watanzania wenzangu kwa kuondokewa na Rais wetu kipenzi. Mungu amlaze mahali pema peponi, Amina...
Kwa hiyo kuwa makamu wa rais ni kujenga madaraja, majengo na mabarabara??
 
One of the best statement nimewahi kusoma hapa.. umeongea jambo Pana Sana..binafsi Mimi hupenda kujiuliza ni nini zilikua dira za viongozi wa Zamani kama vile Nyerere na Karume katika kutekeleza mipango KAZI Yao?...
Kati ya vitu vilivyosababisha uchumi kuyumba ni kulazimisha kuhamisha Serikali Dodoma
 


Mizengo Kayanza Peter Pinda: Huyu ni Waziri Mkuu wa kumi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Alichukua wadhifa huo akiipokea kutoka kwa Mheshimiwa Edward Ngoyai Lowassa aliyejiuzulu. Aliteuliwa tarehe 7 Februari, 2008 na kuthibitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 9 Februari, 2008.


Maisha
Alizaliwa tarehe 12 Agosti 1948 Mpanda vijijini katika mkoa wa Rukwa (sasa Katavi) kama mtoto wa kwanza wa mkulima wa kawaida. Alisoma shule ya msingi Kakuni na seminari ya Kaengesa mwaka 1957-1964. Alijiunga na sekondari ya Pugu kuanzia mwaka 1965 hadi 1968 na baadaye alijiunga shule ya sekondari ya Musoma kwa masomo ya kidatocha tano na sita. mwaka 1969-1970. Alitunukiwa shahada ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1974.​

Ajira na uongozi
Mwaka 1974 baada ya kuhitimu Chuo Kikuu, alijiunga na utumishi wa serikali kama Wakili wa serikali katika Wizara ya Katiba na Sheria. Mwaka 1978 akahamia ofisi ya Usalama wa Raia Ikulu, kwanza chini ya Julius Nyerere, halafu chini ya Ali Hassan Mwinyi. Kuanzia mwaka 1982 akaendelea kuwa Katibu Mnyeka Msaidizi wa Rais hadi mwaka 1992. Kuanzia mwaka 1996 hadi 2000 alikuwa Katibu wa Baraza la Mawaziri.

Aliiingia Bungeni mwaka 2000 kama mbunge wa Mpanda Mashariki mkoani Rukwa akawa Naibu Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa. Mwaka 2006 akapandishwa cheo kuwa waziri kamili. Baada ya kujiuzulu kwa Waziri Mkuu Edward Lowassa, Pinda aliteuliwa na Rais Jakaya Kikwete na kuthibitishwa na bunge kwa kura 279 za ndio katika jumla ya kura 283 zilizopigwa.

Baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 aliendelea na wadhifa huo. Mwaka 2015, alikuwa ni mmoja kati ya makada 38 wa Chama Cha Mapinduzi ambao walichukua fomu kuomba kukiwakilisha chama chake katika kinyang’anyiro cha urais katika uchaguzi mkuu. Pinda alikuwa ni mmoja wa vigogo walioondolewa kwenye mchakato huo katika hatua za awali. Alibakia kuwa mwaminifu katika chama. Hayati Rais Magufuli alimteua kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM.​

Alama alizoziacha akiwa Waziri Mkuu

Alihimiza Kaulimbiu ya KILIMO KWANZA na kuitekeleza kwa vitendo.

Alisimamia matumizi ya fedha katika Halmashauri na kuwataka viongozi waguswe na matatizo ya wananchi.

Alisimamia matumizi bora ya fedha katika Serikali Kuu kwa kukataza ununuzi wa magari ya kifahari.

Alianzisha vita dhidi ya mauaji ya vikongwe na walemavu wa ngozi (Albino).


Kwanini anaweza kuteuliwa kuwa Makamu wa Rais
  • Ni mtu mzima, ana umri wa miaka 72 Umri ambao unafaa kabisa kama mshauri mkuu wa Rais na kama nguzo kati ya Rais na Waziri Mkuu. Kumbuka Rais Samia ana miaka 61 na Waziri Mkuu Majaliwa ana umri wa miaka 61. Kwa umri wake wa miaka 72 hawezi kuwa na tamaa ya kuunda makundi ya matamanio ya nafasi ya Urais, yeye atazingatia kazi tu.
  • Atakuwa kiungo kati ya CCM asilia (ya Kiktwete) na CCM mpya kwani ana elements za makundi yote hayo mawili. Hivyo ataleta umoja katika chama.
  • Ana uzoefu katika kuendesha serikali kama Waziri Mkuu kwa miaka 8.
  • Ni mwamasheria ambaye anafahamu umuhimu wa utawala wa sharia.
  • Mwisho, ingawa si kwa umuhimu yeye ni Mkristo (mkatoliki). Kumbuka Rais ni Mwislamu na Waziri Mkuu ni mwislamu. Utaratibu wa k- balance dini kuu si wa kikatiba ila ni utamaduni wetu.
 
Mizengo Pinda mwenye miaka 72 ateuliwe na awe chini ya Raisi mwenye miaka 61! . Kati ya watanzania zaidi ya milioni 20 na zaidi walio watu wazima amekosekana mtu wa kuteuliwa kuwa makamu wa Raisi eti akafuatwe mstaafu!. Hata kama ni kampeni naona haina macho au namna ya kufikiri iko tofauti kidogo.
 
JANUARY MAKAMBA MAKAMU,DR CHARLES KIMEI AWE WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA NA KITAFUTWE KICHWA KWA AJILI YA KUSHUGHULIKIA MAHUSIANO YA KIMATAIFA Prof MIJICHO APIGWE CHINI
ATAPIGWAJE CHINI WAKATI NDIYE MAKAMU WA RAIS MTARAJIWA?
 
Nitafurahi sana kama Mama atakua na sifa 1 kuu niliyoipenda toka kwa Rais wangu

John alikua hatabiriki,hata kwenye nafasi ya ku point waziri mkuu watu wali guess sana

ila Jina la Kassim likatoka likawa surprise,mambo mengi sana John alikua mpindua meza

mtahisi hivi au vile yeye anakuja na njia ingine kbsa,Natamani sana Rais wangu huyu nae awe

na sifa hiyo,acha sisi huku nnje Tu BET kadri tuwezavyo yeye kazi yake iwe n kuhakikisha mikeka yetu inachanika

Akiwa rais ambae watu wanaweza hisi move zake,akiwa rais ambae kila wanaobashiri wanapatia Kwangu atakua kakosa sifa kubwa

ninayoitamani Rais wa sasa awe nayo,Tanzania n nchi inayohitaji Rais asitabrike maamuzi yake,yani n mwendo wa surprise

mwanzo mwisho,Rais wangu Mama Samia natamani uwe hivyo,Uwe msiri msiri msiri msiri Yani wasijue hata unapigaga mswaki saa ngapi.

Tubaki tu tunashangaa shangaa imekuaje kuaje,YES namuamini MAMA moyo wangu upo kwake,Sina mashaka na Mama,namuelewa💪
 
Napinga japo mimi niko mrengo wa vyama vya upinzani. Kazi ya vyama hivi ni kutoa sera mbadala na vitashindwa kufanya hivi kama vitaingia serikalini. Cha msingi vyama hivi vipewe nafasi ya kufanya shughuli zao kwa mujibu wa sheria na tuwe na Tume Huru ya Uchaguzi.
 
Ndugu zangu watanzania,poleni sana kwa msiba huu mzito ambao ni uzoefu wetu wa kwanza kabisa tokea tuanze kujitawala.

Pamoja na msiba huu mzito,nchi inaingia kwenye mabadiriko ya uongozi katika ngazi ya Urais na makamu wake.

Kwa mujibu wa katiba yetu,inampa mamlaka Makamu wa raisi kuwa rais wa nchi.

Baada ya kuapa,nafasi ya umakamo inabaki wazi,hivyo mimi kama mtanzania nimekuja na orodha ya watu kadhaa ambao ninafikiria kwamba,wakichukua nafasi ya umakamo watamsaidia mama yetu na nchi ikapiga hatua kwenda mbele.

1😛ro Mark Mwandosya huyu ni mzee mwenye hekima,mtulivu,msomi,ana msimamo pia amewah kugombea nafasi ya uraisi mara mbili .2005 alingia top 3,2015 alingia top 10 hivyo chama pia kina imani nae.

2.wilium Lukuvi huyu mzee ni mtulivu sana katika maamuzi,wizara yake ameitendea haki mno,ana busara,msimamo nk

3.
4.
5.

Tuendeleze wengine hapo
 
Tuzidi kusali wale wanaham ya kiti cha umakamu wa Rais tafadhali soma heading. End
 
Uko sahihi mkuu [emoji122]Jk na Mama ni watu wanao elewana sana
 
Sawa, tuwe na subira
Amani na Upendo vitawale.
 
Wanajamvi naandika haya nikijielewa na akili timamu Ndugu Humphrey Polepole ndiye atakuwa vice president wa Tanzania.

Nimesogezewa hii habari nyeti na rafiki yangu yupo kitengoni sitamtaja (very very reliable sources) due to the sensitivity of the matter.

Na kama hatajaguliwa basi watakuwa wamesitisha uteuzi huo kwasababu imevuja.

Naombeni mniamini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…