Baada ya Kifo cha Rais Magufuli: Nani anafaa kuwa Makamu wa Rais Tanzania?
Habari wana Jamvi,

Katika fikra na matamanio yangu ni kumwona huyu bwana Dk. Assad aliekuwa Mkaguzi Mkuu Wa Serikali kurudishwa ndani ya system. Huyu ukiachilia mbali elimu na uwezo aliokua nao, amedhihirusha sana kuwa anafaa kushika nyadhifa za juu katika serikali.

Miongoni mwa sifa ni;

1) Msomi wa hali ya juu na anaeitendea haki elimu yake ya Phd (Sio mtapia tumbo kama wateuliwa wengine wenye Phd zao).

2) Amedhihirisha kusimamia vizuri na kwa weledi mkubwa sana matumizi ya hela za wananchi ambazo serikali inatumia. Kufikia hatua alikua tayari kupoteza kazi yake kwa kusimamia msimamo wake na kukataa kutumia/kuamrishwa na mihimili ya nchi.

3) Amediriki kuikosoa serikali na bunge pindi lilipoji umauma juu ya matumizi ya Sh Trillion 1.2 na lilipotaka kuficha baadhi ya makosa ya matumizi ya pesa za umma.

4) Muadilifu, Mkweli na Muwazi.

5) Msimamizi mzuri wa hela za umma.

6) Hana maswala ya kuwa na team (Hayupo team CCM MPYA wala CCM KONGWE). Team hizi sasa hivi zinapambana kuona mtu wao anashikilia hicho kiti, na team itakayo shindwa basi itakufanyia hujuma kuelekea 2025 kuliko hujuma za vyama vya upinzani.

7) Hana makuu wala kujionesha (CAG alikua akiendesha Toyota IST).

8) Hana sifa ya kutumia cheo chake kukandamiza watu au kujipatia hela (Waliokua watendaji wake katika Ofisi Za CAG wanamjua na kusikitika kumpoteza).

9) Hana Kashfa wala figisu wala chuki (Hana visasi na utanijua mimi nani).

10) Anajua kazi zake kwa hali ya juu (Mafisadi ndani ya serikali watachemka matumbo na kuharisha huyu bwana akirudi serikalini, maana hakuna wakumdanganya kwenye swala la mahesabu na matumizi -Bunge nalo lijipange kwake huyu mtu, hawana cha kumdanganya).

11) Miradi alioacha Marehemu Magufuli ni mingi sana, bila msimamizi mzuri katika mahesabu na matumizi ya hela basi ufisadi utakithiri kupita kiasi.

12) Kuna tetesi za hela kuibiwa mara baada tu ya Rais kufariki dunia, kwa kigezo zimetumika katika ununuzi wa mashine za kumtibu Rais, huyu mtu atahakikisha UKWELI JUU YA HILI - Risiti za manunuzi au pesa zitawatokea katika tundu lolote wanaosadikiwa kuzichota hizo hela.

Tafakari ushauri huu, utani shukuru baadae moyoni mwako. Huyu mtu ni muhimu sana kwetu wananchi kama msimamizi wa hela zetu za kodi na atakua mshauri bora sana kwako.

Wako mtiifu,
Alexander The Great
Je ni kada?
 
No offense, ingawa sioni impact kwangu mimi binafsi ila naamini hawawezi weka muoslamu hapo. Nafasi ya mkristo hiyo...wanajua wakiweka muislamu piga ua kuna topic za kuligawa taifa hazitakua zinakwepeka...they are not dumb to let this topic drags on...
Kwanini unafkiri ni nafasi ya mkristo?

Uliloandika linasapotiwa na katiba?

Kwamba rais akiwa muislamu makamu wake lazima awe mkristo

Au ni hisia zako tu.

Kikwete ni muislamu na makamu wake ghalib bilal alikua muislamu hapa napo unasemaje?
 
Haipo kwenye katiba ila kuna busara hutumika tu kuepuka chochote ambacho kinaweza leta divisions ktk taifa...
Kuwa na rais muislamu, makamu wa rais muislamu, waziri mkuu muislamu italeta topics ambazo sio nzuri kwa muunganiko wa taifa.
 
Upuuzi wa assad ni upi?
Alichofanya kwenye mfuko wa pensheni umeishasahau....kumchotea Zitto hela za kutangaza vivutio vya utalii na kuanzisha Chama cha siasa ili kudhoofisha Ukawa!
 
Habari wana Jamvi,

Katika fikra na matamanio yangu ni kumwona huyu bwana Dk. Assad aliekuwa Mkaguzi Mkuu Wa Serikali kurudishwa ndani ya system. Huyu ukiachilia mbali elimu na uwezo aliokua nao, amedhihirusha sana kuwa anafaa kushika nyadhifa za juu katika serikali.

Miongoni mwa sifa ni;

1) Msomi wa hali ya juu na anaeitendea haki elimu yake ya Phd (Sio mtapia tumbo kama wateuliwa wengine wenye Phd zao).

2) Amedhihirisha kusimamia vizuri na kwa weledi mkubwa sana matumizi ya hela za wananchi ambazo serikali inatumia. Kufikia hatua alikua tayari kupoteza kazi yake kwa kusimamia msimamo wake na kukataa kutumia/kuamrishwa na mihimili ya nchi.

3) Amediriki kuikosoa serikali na bunge pindi lilipoji umauma juu ya matumizi ya Sh Trillion 1.2 na lilipotaka kuficha baadhi ya makosa ya matumizi ya pesa za umma.

4) Muadilifu, Mkweli na Muwazi.

5) Msimamizi mzuri wa hela za umma.

6) Hana maswala ya kuwa na team (Hayupo team CCM MPYA wala CCM KONGWE). Team hizi sasa hivi zinapambana kuona mtu wao anashikilia hicho kiti, na team itakayo shindwa basi itakufanyia hujuma kuelekea 2025 kuliko hujuma za vyama vya upinzani.

7) Hana makuu wala kujionesha (CAG alikua akiendesha Toyota IST).

8) Hana sifa ya kutumia cheo chake kukandamiza watu au kujipatia hela (Waliokua watendaji wake katika Ofisi Za CAG wanamjua na kusikitika kumpoteza).

9) Hana Kashfa wala figisu wala chuki (Hana visasi na utanijua mimi nani).

10) Anajua kazi zake kwa hali ya juu (Mafisadi ndani ya serikali watachemka matumbo na kuharisha huyu bwana akirudi serikalini, maana hakuna wakumdanganya kwenye swala la mahesabu na matumizi -Bunge nalo lijipange kwake huyu mtu, hawana cha kumdanganya).

11) Miradi alioacha Marehemu Magufuli ni mingi sana, bila msimamizi mzuri katika mahesabu na matumizi ya hela basi ufisadi utakithiri kupita kiasi.

12) Kuna tetesi za hela kuibiwa mara baada tu ya Rais kufariki dunia, kwa kigezo zimetumika katika ununuzi wa mashine za kumtibu Rais, huyu mtu atahakikisha UKWELI JUU YA HILI - Risiti za manunuzi au pesa zitawatokea katika tundu lolote wanaosadikiwa kuzichota hizo hela.

Tafakari ushauri huu, utani shukuru baadae moyoni mwako. Huyu mtu ni muhimu sana kwetu wananchi kama msimamizi wa hela zetu za kodi na atakua mshauri bora sana kwako.

Akikataa uteuzi, alazimishwe.

Wako mtiifu,
Alexander The Great
Hiyo Dini imetosha. Tubalance Ebho!

Assad atake asitake ni CAG Mpya "in CCM's VOICE"
 
Kwanini unafkiri ni nafasi ya mkristo?

Uliloandika linasapotiwa na katiba?

Kwamba rais akiwa muislamu makamu wake lazima awe mkristo

Au ni hisia zako tu.

Kikwete ni muislamu na makamu wake ghalib bilal alikua muislamu hapa napo unasemaje?
Waziri mkuu alikuwa nan???

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
CAG hana mamlaka yoyote ya kuidhinisha kutolewa kwa pesa katika account yoyote ya serikali wala mifuko ya hifadhi ya jamii. Hio walitaka kumfanyia scandle ika fail.

Amka wewe.

Kweli mkuu nimechanganya na yule ambaye ni balozi sasa hivi! Msiba nzito huu!
 
Salaam Wananzengo

Kutokana na Nchi Yetu kuwa na Msiba ambao kimsingi umeleta hali ya tafakuri kubwa hasa ni nani atatosha kusaidiana na Mama Samia katika Kutuongoza.

Mimi Nashauri Wafuatao Wapewe nafasi.

1. Prof. Mussa Assad.

Kwanza ni Msomi Mzuri na pia amebobea sana kwenye eneo la uchumi..Lakini Pia Prof huyu Ana misimamo mikali sana hivyo ataweza kutusaidia sana.

2. Dr Mpango.
Kwa hawa watu wanaojulikana Mpango anaweza kuwa wa msaada sana. Kwanza ni Mzalendo amefanya kazi World bank na hivyo anajua uchumi wa Dunia na hapa kwetu na pia kwa kukaa kwake Wizara ya Fedha kumempa wigo mpana wa kuhusika na miradi Mikubwa hii pamoja na Makusanyo ya Serikali.

Dr Mpango pia hana kashfa wala sio muoga Kuchukua maamuzi.

Wengine wanaoweza hii nafasi katika wale tulionao wote wana makundi hasimu hivyo uteuzi wao unaweza kuleta mgawanyiko zaidi au kujenga Makundi hasimu zaidi.

Alamski.
 
We mpuuzi kweli ww! Zito unataka ndugu zako wacontrol serikali zote mbili eeh! Hautapata hiyo nafasi tena na utapeli wako! Huyo assad ndio nani kwanza asiye na adabu na uzalendo ambaye kama juha anakwenda kwa wazungu kuisema vibaya serikali na bunge letu kama anavyofanya tundu na zito afu unataka awe vp, we mgonjwa kweli ww! Labda kama vp kwa mambo yenu ya binafsi lakini kamwe siyo ya kitaifa! Huyo hana nafasi kwa serikali inayokwenda kwa kasi hii!
Badili fikra zako hayo mawazo zama zake zilishapita
 
Salaam Wananzengo

Kutokana na Nchi Yetu kuwa na Msiba ambao kimsingi umeleta hali ya tafakuri kubwa hasa ni nani atatosha kusaidiana na Mama Samia katika Kutuongoza.

Mimi Nashauri Wafuatao Wapewe nafasi.

1. Prof. Mussa Assad.

Kwanza ni Msomi Mzuri na pia amebobea sana kwenye eneo la uchumi..Lakini Pia Prof huyu Ana misimamo mikali sana hivyo ataweza kutusaidia sana.

2. Dr Mpango.
Kwa hawa watu wanaojulikana Mpango anaweza kuwa wa msaada sana. Kwanza ni Mzalendo amefanya kazi World bank na hivyo anajua uchumi wa Dunia na hapa kwetu na pia kwa kukaa kwake Wizara ya Fedha kumempa wigo mpana wa kuhusika na miradi Mikubwa hii pamoja na Makusanyo ya Serikali.

Dr Mpango pia hana kashfa wala sio muoga Kuchukua maamuzi.

Wengine wanaoweza hii nafasi katika wale tulionao wote wana makundi hasimu hivyo uteuzi wao unaweza kuleta mgawanyiko zaidi au kujenga Makundi hasimu zaidi.

Alamski.
Assad ni Mzenj, hawezi kuwa VP. Ila anastahili kuwa waziri au KM wa $$, ikishindikana kabisa awe CG wa TRA.

Mpango is tainted - has got too much MATAGA on him atamharibia rais mpya.
 
Back
Top Bottom