Baada ya Kikwete sasa kiongozi wa EAC ni Kenyatta

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
7,823
Reaction score
10,857
Baada ya Kikwete kuondoka kiongozi wa EAC kwa wenzetu wanamwona ni Kenyatta. Magu jitahidi kuchukua nafasi hii Kenyatta akiondoka. Kikwete alijitahidi na kuheshimiwa sana. Sasa mambo ya nje tumebaki na vikwazo kila siku hakuna hata statement ya kinachoendelea

 
Maisha kwa zamu Kaka. Nakumbuka jinsi jk alivyokuwa mashughuri nje ya nchi. Jk hakuwa Kiongozi wa mfano EAC tu..jk alikuwa Africa nzima. Yaani Rais wa china ameingia tu madarakani 2012 ziara ya Kwanza ameifanya Tz. Tanzania tulipokea maraisi wa 3 siku 1.. Rais Obama..na Bush one day. Jk alikuwa anaonewa Wivu hadi na wenzake Africa Mashariki. Mungu akupe maisha marefu jk..
 
Halafu Magufuli akimshinda Kenyata ndo aweze kukupata? Mara ya mwisho demu alinifanyia hivyo nilimpiga chini, mambo ya kuchonganisha Wanaume wawili eti mshindi akuchukuwe nilikataa, na mara nyingi unakuta demu mwenyewe anayechonganisha Wanaume wala siyo mzuri.
 
Ila huu ni ujinga sana. Kila mara Kenyatta akienda US hakanyagi red carpet . Sijui kunashida gani.

Mi nazani kuna haja ya kumuelimisha. Hilo rsd carpet ni lake sio la trump na mkewe.
 
Kipimo cha kuwa "kiongozi" ni kutangatanga, kujikomba, kuwa mnafiki na kuwazunguka viongozi wenzako?

Hicho kipimo cha uongozi kitakuwa na hitilafu kubwa.

"Prayer Breakfast"...hizi hizi zilimtoa kimasomaso Robert Ouko! Hivi pale Nyayo hamuwezi mkafanya breakfast na kusali hadi kufunga safari za kila mwaka?
Watu wa ajabu sana!
 
 
Ila huu ni ujinga sana. Kila mara Kenyatta akienda US hakanyagi red carpet . Sijui kunashida gani.

Mi nazani kuna haja ya kumuelimisha. Hilo rsd carpet ni lake sio la trump na mkewe.
Ndiyo maana Magufuli hua haendi...huu ni udhalilishaji kabisa.
 
Sasa nawe umeandika nini hapa? Hoja hujaipitia vizuri?
 
Kenyatta akienda duniani lugha ina mwagika tu, akija kwetu kimatumbi kinamwagika tu. Kenyatta abarikiwe.
Ndie kiongozi smartest kuliko wote EAC kuanzia speech,public speaking,reasoning,speech zisizochosha,civilized mwenye exposure
 
Kama kawaida, hukuelewa nilichoandika. Badala yake unazunguka porini na maneno chungu nzima!.

Niliandika wapi kuwa Tanzania isiwe na mahusiano mazuri na nchi ziingine?
 
Kuna wengine wameweka utamaduni wa kupinga kila kitu. Tuwasifie Kenya na kuiga mazuri kwa faida ya nchi yetu. Yaani Kenya hawako kwenye list wakati wana vita na magaidi wa somalia. Sisi ni malumbano tu tuangalie kwa mapana tusipoteze muda kulumbana bila sababu. Hapa kuna mpaka usalama wa taifa 😂 eti na wenyewe wanajifanya wanajadili! Kwa manufaa ya nani taifa?. Usalama wa taifa unatakiwa kusaidia nchi ambayo inawezekana kabisa kuongia pabaya baada ya chaguzi na sio kushinda kwenye mitandao kuwinda Watanzania. Usalama mnajijua na watu wanawajua hapa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…