Baada ya kubainika ufisadi wa kutisha, anataka kujifichia kwenye Mradi Bandari ya Bagamoyo?

Ukweli ni kuwa ukifanya comparison analysis ukiwa objectively kabisa kati ya mikataba iliyoingiwa wakati wa JK na ile ya wakati wa JPM utaona mikataba karibia yote ya wakati wa JK ilikuwa ya kipigaji kuliko ya wakati wa JPM.
Unaoweza kuorodhesha mikataba angalao 3 ya wakati wa JK iliyokuwa yabkipigaji, na angalao mikataba mitatu ya wakati wa marehemu ambayo ilikuwa mizuri? Na kila upande ukaelezea ubaya na uzuri wake?
 
Mkataba wa Bandali Bagamoyo

Mkataba wa kinyonyaji wa Gesi yetu mtwara, Sisi uzalishaji wetu uishie 40% tu, hiyo nyingine ni ya mwekezaji

Richmond

Huyo ni Mzee wa msoga!!
 
Eti, Raisi hakushauriwa vizuri kuhusu mradi wa ujenzi bandari ya Bagamoyo, Wakati huohuo yeye ndiye mshauri mkuu wa serikali, alikuwa wapi?

Raisi wetu amefariki ndo kunampa mwanya wa kumwandama na kumkandia kila Neno Baya, sasa tunataka mtwambie kama Kweli kazi yenu ni kuishauri serikali na kuisimamia

Kabla ya tamko lako Jana kuhusu ujenzi na uwekezaji wa bandari ya Bagamoyo, uliwahi pia kutamka kwamba, mradi huo ni hasara Kwa Serikali Kwa jinsi Mkataba wake ulivyokaa, na kama ndivyo, wewe ndiye umetufanya kama Taifa tuchelewe kuwa na mradi huo, unapaswa kujibu hili

Sasa Sisi tushike lipi?

Najiuliza, Yeye kama mkuu wa mhilimili huo, anaongoza chombo chenye kazi ya kuishauri na kuisimamia serikali, Alikuwa wapi, mbona alitaka Raisi aongezewe muda wa kutawala? Si ni yeye jamani au ni mwingine!! Je, hakuwa analiona tatizo la ufisadi uliokuwa unaendelea?

Kwa tarifa ya CAG imeibua madudu makubwa na ufisadi wa kutisha, badara ya yeye na mawaziri wote kama sio Bunge loote kuwajibike Kwa kushindwa kuisimamia serikali anaibuka na Jambo la ajabu tu ili kutuondoa kwenye Hilo la ufisadi, hivi mnaaibu kweli nyinyi watu!

Tukionyesha hasira zetu wananchi tuliowatuma kwenda kusimamia rasilimali zetu mnatutumia wasiojulikana, ni Sawa Kwani kufa ni kutangulizana Tu

Tunalitaka Bunge liwajibike katika hili, la sivyo mtuambie ni Kwa nini mlitaka Raisi aongezewe muda

Tunataka pia, mradi wa Ujenzi bandari ya Bagamoyo, Mkataba wake uwekwe mezani tuambie yaliyomo na Kisha Bunge loote livunjwe, Kwani ni hasara tupu!!

Acha tupige [emoji2484][emoji2484][emoji2484]

Kumbe hamuaminiki tena!!
Hii nchi yaan
 
Unaoweza kuorodhesha mikataba angalao 3 ya wakati wa JK iliyokuwa yabkipigaji, na angalao mikataba mitatu ya wakati wa marehemu ambayo ilikuwa mizuri? Na kila upande ukaelezea ubaya na uzuri wake?
Fanya research kama uko interested;

Kukupa tip kidogo pitia Richmond, Bandari ya bagamoyo japo haikuwahi kusainiwa.
 
Bunge litunge sheria ambazo zitaruhusu mikataba yote kupitiwa na Bunge na Kisha kupelekwa tena Kwenye Chama cha wanasheria Kwa ushauri zaidi ndipo kuruhusiwe kufanywa Kwa mradi huo, Maana sasa tumechoka na madudu yanayotokea baada ya mikataba kufanyika
 
Kuna namna watu wanatafuta maslahi upande wa pili na mpango maalum wa kuonyesha madudu ya aliyepita ili watu wajue alikuwa mbaya na wao wapate nafasi kufanya kazi under no pressure
Na kama kila serikali ikija na mpango mkakati wake hakika kufika mbali itakuwa ngumu sana kila anayekuja anaona aliyetangulia ni mbaya
 
Mimi Hadi nimeingiwa na wasiwasi pia na mkaguzi wa Hesabu za serikali

Yeye ni mkaguzi wa fedha tu na kushauri namna Bora ya matumizi ya fedha

Anapokuja na swala la Stendi ya Magufuli eti itasababisha msongamano, hii tunaweza kuita ni kujaribu kuzima yoote mazuri ya JPm
 
Tunataka pia, mradi wa Ujenzi bandari ya Bagamoyo, Mkataba wake uwekwe mezani tuambie yaliyomo na Kisha Bunge loote livunjwe, Kwani ni hasara tupu!!
Bunge la sasa halina tija yoyote. LiVUNJWE tuu, au ndugai aondolewe
 
Anapokuja na swala la Stendi ya Magufuli eti itasababisha msongamano, hii tunaweza kuita ni kujaribu kuzima yoote mazuri ya JPm
HAPANA, ni kazi yake.. vinginevyo atakuwa Kama roboti
 
Mimi Hadi nimeingiwa na wasiwasi pia na mkaguzi wa Hesabu za serikali

Yeye ni mkaguzi wa fedha tu na kushauri namna Bora ya matumizi ya fedha

Anapokuja na swala la Stendi ya Magufuli eti itasababisha msongamano, hii tunaweza kuita ni kujaribu kuzima yoote mazuri ya JPm
Mambo mengine yana shangaza kidogo - hivi tangu lini mkaguzi wa fedha za serikali akawa Engineer wa ujenzi?Mambo ya kusema eti ujenzi wa stand ya mabasi utasababisha msongamano wa magari, huo utafiti aliufanya lini akiwa na lengo gani kama hiyo sio kujiingiza katika masuala ambayo hayamuhusu ie hana taaluma nayo.
 
Nilikuwa nadhani supika (spika )ni mtu mkubwa sana na ana access ya kuomba kuonana na mh rais muda mwingi na kama ndio hivyo je alishindwa hata kumnong'oneza? aah jamani yaani uso wa mbuzi watu wanauchuna
 
Ki ukweli kwa namna mambo yanavyokwenda mh. Rais na mama yetu muombe Mungu saaaana tena saaana

Sisi watanzania tuko nyuma yako lakini nawea sema ni u kiumbe pekee kuwahi kutokea na sidhani kiumbe kingine kama wewe kitakuja kutokea kwenye huu uso wa dunia
Kwa nini niseme hivi?

Sababu ni hizi....
1. Umebahatika kuishi katika maisha ya kuanzia kesho kuja leo.
Yaani umebahatika kuishi maisha yajayo kuja yaliyopo na kumalizia yaliyopita kwenye ardhi hii.

Hapa utagundua Mungu kakuonyesha maisha yako yajayo kwa wakati huu uliopo.
Yaani umepata kioo cha kuyaangalia maisha yako yajayo.
Waza haya ya mtangulizi wako waliomzunguka kumbe ndio wasiompenda jifunze hili.

2. Umepewa fursa ya kuwasoma wasaidizi wako watakavyokuwa siku muda ukifika.

3. Umepewa maono ambayo wengine hutokewa kama ndoto lakini kwako umeletewa wewe ushindwe kudhibitisha.
Pamoja na nguvu na sauti kubwa ya hayati lakini CAG kaja na haya. Hatusemi kwamba mwenda zake alikuwa fisadi kwamba hizi pesa zooote alikula yeye hapana, anaubeba mzigo huu kwa sababu yeye ndio alikuwa kiongozi
Yanayotokea kwa JPJM usifikiri kwako haiwezekani.

Bora JPJM kwa wanyonge ana sala zao ila wewe unakokwenda asee likitokea la kutokea watu wanaweza iba mpaka nyumba yako ya milele.

Cha kufanya
Usijiteteee na ukajaribu hata kidogo kuwaridhisha wanasisiemu nikwambie baada ya hii ripoti watu yale mabango ya raisi marehemu watu wameyapamba ndani na wengi wameyageuza kama matandiko ndani mwao.
CCM haikubaliki tenaa na ili kujiokoa na wewe fanya maamuzi magumu.

Yes fanya maamuzi magumu tena magumu mnooo. Hapa fanya maamuzi magumu
Unamachaguo mawili tuu...

1. Aseeee vunja baraza loooote la mawazili na sio kutia vilaka na kuzungusha wale wale.
Hapa nafahamu madhara yake kwanza unakiuka katiba, ndio vunja tuu kwani serikali chini ya ccm katiba imevunjw mnoo na sasa vunja kwa maslahi ya umma.
Pili. Ni gharama nafahamu kulivunja kutatumia gharama kubwa lakini amini wa tz tuko tayari kuvuja jasho kwa kwani tushajifunza na niseme tushazoea.

2. Vunja libunge aseee halina na halitakuwa na msaada kwako
Jifunze kwa mwenzio mbali na kula pesa zetu hakuna walichomsaidia zaidi ya kumuwekea mitego na akategeka kwani aliwaamini. Mama fanya haraka aseee la sivyo utakuja kushtuka ni too late.
Hapa pia ni gharama lakini ukifanya haya kwa maslahi ya taifa utakumbukwa kama shujaaa.
Ukumbuke asilimia kuuubwa ya hilo bunge hakuna alieingia humo kwa kampeni zake mwenyewe. Wengi waliingia kwa kuombwa kutoka kwa wanainchi na raisi alieondoka.
Hivyo alichagua wanaomfaa yeye na sera zake lakini naamini hawataweza kubadilika ghafla ili waendane na wewe.
Hawajui walichokwenda kufanya wengi waliingia ili watumwe na rais huyo.
Kwa kau ile
Nileeteni huyu halafu maendeleo mniulize mimi.

Watakusumbua mnooo

Na ikikupendeza hapa ni kama ukitaka na ninyongeza tuu

3. Unda tume huru ya uchaguzi ili kila anaingia humo awe anajua uchungu na ajue atawajibika kwa waliompeleka. Asijekuwa anathaminisha pesa alizotunia na watu.

Mwishoooni kabisa na wewe jiuzuru kwani itakuonyesha kuwa umewajibika.
 
Mambo mengine yana shangaza kidogo - hivi tangu lini mkaguzi wa fedha za serikali akawa Engineer wa ujenzi?Mambo ya kusema eti ujenzi wa stand ya mabasi utasababisha msongamano wa magari, huo utafiti aliufanya lini akiwa na lengo gani kama hiyo sio kujiingiza katika masuala ambayo hayamuhusu ie hana taaluma nayo.
Mkaguzi wetu ana maajabu boss
 
Eti, Raisi hakushauriwa vizuri kuhusu mradi wa ujenzi bandari ya Bagamoyo, Wakati huohuo yeye ndiye mshauri mkuu wa serikali, alikuwa wapi?

Raisi wetu amefariki ndo kunampa mwanya wa kumwandama na kumkandia kila Neno Baya, sasa tunataka mtwambie kama Kweli kazi yenu ni kuishauri serikali na kuisimamia

Kabla ya tamko lako Jana kuhusu ujenzi na uwekezaji wa bandari ya Bagamoyo, uliwahi pia kutamka kwamba, mradi huo ni hasara Kwa Serikali Kwa jinsi Mkataba wake ulivyokaa, na kama ndivyo, wewe ndiye umetufanya kama Taifa tuchelewe kuwa na mradi huo, unapaswa kujibu hili

Sasa Sisi tushike lipi?

Najiuliza, Yeye kama mkuu wa mhilimili huo, anaongoza chombo chenye kazi ya kuishauri na kuisimamia serikali, Alikuwa wapi, mbona alitaka Raisi aongezewe muda wa kutawala? Si ni yeye jamani au ni mwingine!! Je, hakuwa analiona tatizo la ufisadi uliokuwa unaendelea?

Kwa tarifa ya CAG imeibua madudu makubwa na ufisadi wa kutisha, badara ya yeye na mawaziri wote kama sio Bunge loote kuwajibike Kwa kushindwa kuisimamia serikali anaibuka na Jambo la ajabu tu ili kutuondoa kwenye Hilo la ufisadi, hivi mnaaibu kweli nyinyi watu!

Tukionyesha hasira zetu wananchi tuliowatuma kwenda kusimamia rasilimali zetu mnatutumia wasiojulikana, ni Sawa Kwani kufa ni kutangulizana Tu

Tunalitaka Bunge liwajibike katika hili, la sivyo mtuambie ni Kwa nini mlitaka Raisi aongezewe muda

Tunataka pia, mradi wa Ujenzi bandari ya Bagamoyo, Mkataba wake uwekwe mezani tuambie yaliyomo na Kisha Bunge loote livunjwe, Kwani ni hasara tupu!!

Acha tupige 🏋️🏋️🏋️

Kumbe hamuaminiki tena!!
Hakupenda kushauriwa na ameboronga vibaya mno bado mtaona uozzo.
 
Back
Top Bottom