Eti, Raisi hakushauriwa vizuri kuhusu mradi wa ujenzi bandari ya Bagamoyo, Wakati huohuo yeye ndiye mshauri mkuu wa serikali, alikuwa wapi?
Raisi wetu amefariki ndo kunakupa mwanya wa kumwandama na kumkandia kila Neno Baya, sasa tunataka mtwambie kama Kweli kazi yenu ni kuishauri serikali na kuisimamia
Kabla ya tamko lake Jana kuhusu ujenzi na uwekezaji wa bandari ya Bagamoyo, aliwahi pia kutamka kwamba, mradi huo ni hasara Kwa Serikali Kwa jinsi Mkataba wake ulivyokaa, na kama ndivyo, yeye ndiye ametufanya kama Taifa tuchelewe kuwa na mradi huo,
Sasa Sisi tushike lipi?
Najiuliza, Yeye kama mkuu wa mhilimili huo, anaongoza chombo chenye kazi ya kuishauri na kuisimamia serikali, Alikuwa wapi, mbona alitaka Raisi aongezewe muda wa kutawala? Si ni yeye jamani au ni mwingine!! Je, hakuwa analiona tatizo la ufisadi uliokuwa unaendelea?
Kwa tarifa ya CAG imeibua madudu makubwa na ufisadi wa kutisha, badara ya yeye na mawaziri wote kama sio Bunge loote kuwajibike Kwa kushindwa kuisimamia serikali anaibuka na Jambo la ajabu tu ili kutuondoa kwenye Hilo la ufisadi, hivi mnaaibu kweli nyinyi watu!
Tukionyesha hasira zetu wananchi tuliowatuma kwenda kusimamia rasilimali zetu mnatutumia wasiojulikana, ni Sawa Kwani kufa ni kutangulizana Tu
Tunalitaka Bunge liwajibike katika hili, la sivyo mtuambie ni Kwa nini mlitaka Raisi aongezewe muda
Tunataka pia, mradi wa Ujenzi bandari ya Bagamoyo, Mkataba wake uwekwe mezani tuambie yaliyomo na Kisha Bunge loote livunjwe, Kwani ni hasara tupu!!
Acha tupige [emoji2484][emoji2484][emoji2484]
Kumbe hamuaminiki tena!!