Baada ya kubainika ufisadi wa kutisha, anataka kujifichia kwenye Mradi Bandari ya Bagamoyo?

Baada ya kubainika ufisadi wa kutisha, anataka kujifichia kwenye Mradi Bandari ya Bagamoyo?

Binafsi Bunge loote sina Imani nalo tena, ni Bora waondoke wote tuanze upya
Turudi kwenye uchaguzi? Wabunge wa CCM hawajipendi? Hawatakubali. Wengine waliingia mjengoni kwa mbeleko ya JPM.
 
Kama unatarajia mazuri kutoka ccm hakika utasubiri sana!
 
Turudi kwenye uchaguzi? Wabunge wa CCM hawajipendi? Hawatakubali. Wengine waliingia mjengoni kwa mbeleko ya JPM.
Mkuu, tumechoshwa na ubutu wao, wanaleta hasara tupu, ni Bora Bunge likavunjwa
 
Huyu Speaker wetu nadhani Haijapata kutokea wa namna hii toka Dunia hii iumbwe.. "Huyu Huyu Ndie alikuwa anasema Mwendazake Hatake Hasitake Hataongezewa Muda" Wenye ile Clip ebu tuwekeeni. Ni aibu sana Kwa CCM maana hii nafasi huyu mtu wetu Inampwaya sana...

Hiyo hapo
 
Hili la bandari mtamuenea tu speaker , pamoja na kwamba simpendi Ndugai lakin kwa hili hapana alishawahi liongelea bungeni kuwa huu mradi una faida nyingi kuliko hasara ,gafla mwenda zake akaanza kebeh juu ya mradi huo ,basi kwakuwa mkubwa ni mkubwa ikabid akubaliane nae tu kishingo upande lakin kwa hil job hakuweka unafki kabisa.

Hata Kama mtu Ana mapunguf basi asibebeshwe lawama pale anaposema ukwel ,job yuko sahihi kbs na kwahil ntampambania kabisa tofaut na wengine ambao hawakuwah sema lolote kipind uchwara akiwa hai
Uko sahihi kabisa mkuu, aisome Pslmp
 
Naona anatafuta fursa ya kupiga pesa.
Yeye kasema ameenda China na kakutana na jamaa Hao wanataka kuwekeza. Tutajuaje kama yeye ameshaahidiwa pesa au percent humo ili ashinikize serikali iingie mkenge.
Aisee miaka 99 bado watu wa naona faida na manufaa. Wajue kuwa wachina ndio mizecho yao wanakopesa au jenga project. Pesa zisipo rudi. Wanachukua ardhi moja kwa moja.
Watanzania msishangae kuona kila mbunge akija na aidea ya mradi wake ili kupata fursa ya upufaji.
Kwa nini tusi focus na miradi ambayo haujaisha. Tumalize ndio tuanze mipya?
 
Mh Raisi, ni wakati muafaka sasa kulivunjilia mbali Bunge hili ambalo ni hasara tupu kwa Taifa , na likiachwa hivihivi, tutakuja tena kuandika hayahaya kipindi chako, maana hili Bunge halitimizi wajibu wake,
Mkuu umesahau hili ndilo bunge lililovunja record tangu vyama vingi vianze, "limeshinda kwa kishindo" hili ndilo bunge pendwa la CCM, mzee Meko aliyapenda haya ujue.
 
Hilo bunge lote sasa halina maana tena, wabunge ni binadamu kama sisi tu. Walichotuzidi ni kadi za vyama tu. Mimi nilimsikiliza wakati anaelezea kuhusu mradi wa Bandari ya Bagamoyo. Hata body language yake ilionyesha kabisa kwamba hata tunaingizwa mkenge
 
Ukweli ni kuwa ukifanya comparison analysis ukiwa objectively kabisa kati ya mikataba iliyoingiwa wakati wa JK na ile ya wakati wa JPM utaona mikataba karibia yote ya wakati wa JK ilikuwa ya kipigaji kuliko ya wakati wa JPM.
Naomba tuwekee Hio Mikataba.
 
Kwa kumbukumbu zangu Ndugai alisema bungeni akiwa ktk kiti cha spika kwamba mradi wa Bagamoyo ni wa faida sana ameupitia kwa kina Mpaka huko China.

Baada ya muda mfupi Hayati akaukandia kwa kutoa nukuu ya vipengele kadhaa vya kiunyonyaji ambavyo sisi wananchi hatujui kama ni kweli au sivyo.Hapo ndipo Ndugai ikabidi atumie kanuni ya The boss is always right

Binafsi Siamini yale yaliyosemwa na JPM juu ya mradi huo wala yanayosemwa na wanaoutaka sasa Mpaka nipate "bahati"ya kusoma mkataba huo.

Serikali iruhusu mikataba yenye mivutano kama huu upelekwe bungeni kwa mjadala hapo sisi wananchi tutajua mbivu na mbichi
Ni kweli Ndugai aliuongelea huu mradi toka siku nyingi akazimwa kuwa huenda kapewa Rushwa China.
 
Turajuwaje Sisi, Kwa nini aseme Mkataba wake haufai tena? Yeye Hana msimamo? Tutajuaje, je kama aliahidiwa lupia ili aupige Kampeni bungeni??

Hapa ni Mkataba kuwekwa mezani Kwa kuchambuliwa basi
Tutajuaje usahihi wa JPM? Kwa nini JPM alipoongea hayo tulimuamini 100%? Kwa nini tusingepiga kelele mkataba uende bungeni tujiridhishe? Nadhani sasa tunaanza kuona makosa tuliyokua tunafanya ya kupiga vigelegele kila aliloongea JPM. Hii ilimfanya akawa anaongea kila analopenda kwa sababu hakukuwa na wa kumpinga.
 
Hawa wachumia matumbo wasitake kumchanganya yoyote ni miradi ya MATUMBO YAO. Huyu alikuwa mstari wa mbele kusifu na kuitia NDIYO kwa mambo yote aliyosema Hayati Rais wetu Magufuli. Leo anakuja na upuuzi wa kuitaka Bandari ya Bagamoyowakati wa mjadala wake wakati ule Bungeni alikiri kuwa ni MRADI WA HOVYO. leo anauona ni mradi mzuri; na anasimamndani ya chombo kitakataifu kama Bunge na kuanza kusemasema maneno ya UONGO. ASHINDWE NA ALEGEE na Wanamtandao wenzake.

Nimemsikia pia kuhusu ndege za Air Tanzania! Huyu mtu VIPI!? Anaanza kupiga U-TURN hata yule aliyekuwa akimuunga mkono, hatujamsahau!? Kweli hawa watu vipi!? U - ndio na U - yes kwa Hayati umeisha mapema hivi? Kweli hakujua kuwa Air Tanzania kuna matatizo, hadi CAG aseme ndio na yeye atie neno, ubabaishaji gani huu?

Tusubiri tutawaona wengi wakipiga U-TURN na KUGEUKA MAWE kwa maslahi na matumbo yao wenyewe. Ila wakumbuke CCM bado ni imara na itasimamia maslahi mapana ya Taifa hili.
 
Wakati anapigiwa kelele kutokana na uongozi wa kibabe bungeni mlimtetea kwa nguvu kubwa.Leo anapomponda meko kidizaini mnachanganyikiwa Mwenzenu kapiga U turn na kuamua kwenda na salamu mpya ya mama..Hata kudai mkataba wa Mradi wa Bagamoyo upelekwe bungeni ni upuuzi.Wakati wapinzani wakidai mikataba ya SGR,Ndege,Mradi.wa umeme Rufiji na mingine mingi ipelekwe bungeni mlisema mnacheleweshwa kufanya maendeleo.Kikombe hiki hakiepukiki.

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
 
Ni kweli Ndugai aliuongelea huu mradi toka siku nyingi akazimwa kuwa huenda kapewa Rushwa China.

Ndugai na Wanamtandao wenzake wanajua fika kuwa huo mradi wa Bandari ya Bagamoyo ni wa KIUNYONYAJI, vipi leo anapata wapi ujasiri wa kusimama Bungeni na "kugeuka jiwe" na kuanza kuunadi na kuutetea mradi wa hovyo na wa kiunyonyaji kama huo? AU Wachina wamemweka :"sawa"?
 
Hata angestaafu bado yangemkuta haya haya maana yeye ndio aliyaasisi dhidi ya viongozi wengine.

Tena ashukuru hajashuhudia maumivu ya kusemwa vibaya kama alivyokuwa anawasema wengine
 
Back
Top Bottom