Baada ya kubainika ufisadi wa kutisha, anataka kujifichia kwenye Mradi Bandari ya Bagamoyo?

Baada ya kubainika ufisadi wa kutisha, anataka kujifichia kwenye Mradi Bandari ya Bagamoyo?

Kusema kweli kipindi kile hakukuwa namna mnaomlaumu mnamuonea tu hata Kama ungekuwa wewe Mugufuli alikuwa hakubali ushauli na alishasema ukijaribu kumshauli ndio umeharibu kabisa so tumsamehe anafamilia na anasomesha
 
Kama vipi Rais avunje Bunge turudi kwenye uchaguzi wa wabunge tu.
Kwa Mujibu wa katiba yetu Rais Akivunja bunge tunarudia Uchaguzi wa Rais na Mbunge sasa Samia haezi kubali hayo Bado hajajitengeneza na kujiimarisha vizuri kisiasa Ajaweka Alama yake bado so Anaeza akazaragazwa kwenye Uchaguzi wa Marudio So Hapo hakuna jinsi Tusubiri 2025 au lolote litakalotokea katikati ya Hapo
 
Ttz mwendazake alikuwa muongo muongo sana
Kwa kumbu kumbu zangu Ndugai alisema bungeni akiwa ktk kiti cha spika kwamba mradi wa Bagamoyo ni wa faida sana ameupitia kwa kina Mpaka huko China.

Baada ya muda mfupi Hayati akaukandia kwa kutoa nukuu ya vipengele kadhaa vya kiunyonyaji ambavyo sisi wananchi hatujui kama ni kweli au sivyo.Hapo ndipo Ndugai ikabidi atumie kanuni ya The boss is always right

Binafsi Siamini yale yaliyosemwa na JPM juu ya mradi huo wala yanayosemwa na wanaoutaka sasa Mpaka nipate "bahati"ya kusoma mkataba huo.

Serikali iruhusu mikataba yenye mivutano kama huu upelekwe bungeni kwa mjadala hapo sisi wananchi tutajua mbivu na mbichi

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Turajuwaje Sisi, Kwa nini aseme Mkataba wake haufai tena? Yeye Hana msimamo? Tutajuaje, je kama aliahidiwa lupia ili aupige Kampeni bungeni??

Hapa ni Mkataba kuwekwa mezani Kwa kuchambuliwa basi
Unasema Hana msimamo ,ivi wewe unaweza bishana na boss wako au kiongoz wa nchi?

Je na sisi wananchi tunaowaza mbali Zaid tutajuaje huenda rais nae aliona mradi ule hawez pata 10percent Kama wapatavyo kwenye mirad mingine ndio maana akauponda?

Kijana zinduka usimwamin mwasiasa yeyote yule ,wote ni wapigaji dili tu ,awe jiwe kashatuliza sana tena sana ni vile rais hajadiliw lakin watu wana mafail yake mengi .

Mayanga construction unajua ni ya Nan ,
Unajua mashart ya ule mkataba yalikuaje ? Ukiona mtu anapinga mradi Fulani ujue haufaidishi yeye Kama yeye na ukiona unaupambania jua huo mrad unamfaidisha binafs either kwa kuweka kampuni yake kwa mlango wa nyuma au kupata asilimia fulan.

Ni mpumbavu tu atamwamin jiwe kuwa ule mrad ulikuwa na madudu mengi ,vipi atcl yake iliyoingiza hasara ya 155b kwa miaka mitano tu .

Unajua huyo jiwe kapiga kias gani kwenye hii miradi ya ujenz wa barabara na mirad mingine ?

Unaweza kuwa sahihi kwamba huenda spika alihongwa chochote ili aupigie debe lakin pia upande wa pil unaweza kuta yeye aliona kabisa hapat kitu Kama ganji kwa hao jamaa kwa hasira aliamua kuukataa ,yote yanawezekana so usiwe upande mmoja
 
Kwa kumbu kumbu zangu Ndugai alisema bungeni akiwa ktk kiti cha spika kwamba mradi wa Bagamoyo ni wa faida sana ameupitia kwa kina Mpaka huko China.

Baada ya muda mfupi Hayati akaukandia kwa kutoa nukuu ya vipengele kadhaa vya kiunyonyaji ambavyo sisi wananchi hatujui kama ni kweli au sivyo.Hapo ndipo Ndugai ikabidi atumie kanuni ya The boss is always right

Binafsi Siamini yale yaliyosemwa na JPM juu ya mradi huo wala yanayosemwa na wanaoutaka sasa Mpaka nipate "bahati"ya kusoma mkataba huo.

Serikali iruhusu mikataba yenye mivutano kama huu upelekwe bungeni kwa mjadala hapo sisi wananchi tutajua mbivu na mbichi
Mkuu, umefanya vizuri kwa kuweka kumbukumbu sahihi ju ya Ndugai, umekua pia huna upendeleo kwasababu karibu wote humu hatuji kilichopo ndani ya ule mkataba. Swali langu tu la kimantiki, ambalo sio lazima wewe ujibu, yeyote tu mwenye mapenzi mema kwa nchi yetu; hivi ni busara kujenga bandari nyingine mpya kabisa ili hali zipo bandari 3 zinazofanya kazi kwa bahari hiyo hiyo? Bagamoyo hadi Dar kuna umbali gani? Bila kujali uzuri au ubaya wa kilichopo kwenye huo mkataba, binafsi sioni umuhimu wowote wa bandari ya Bagamoyo; tuachanae na wana siasa kina Ndugai ambao wao wanajua bila UNAFIKI watoto wao hawawezi kwenda chooni, sisi tusio na maslahi ya kiuongozi tunasemaje kuhusu mradi huo?
 
Unadhani IPO shida??

Ni Mkataba kupelekwa bungeni basi
 
Prof. ASSAD alishauri tujeneg taasis na mifumo imara na siyo watu- mbona yanasemwa mengi? alipokuwepo tulikuwa tunaunga juhudi!! mitano migine - atakeasitake tutamlazimisha!! haahaha huku ndio kuzinguana anakosema SAMIA
 
Mkuu, umefanya vizuri kwa kuweka kumbukumbu sahihi ju ya Ndugai, umekua pia huna upendeleo kwasababu karibu wote humu hatuji kilichopo ndani ya ule mkataba. Swali langu tu la kimantiki, ambalo sio lazima wewe ujibu, yeyote tu mwenye mapenzi mema kwa nchi yetu; hivi ni busara kujenga bandari nyingine mpya kabisa ili hali zipo bandari 3 zinazofanya kazi kwa bahari hiyo hiyo? Bagamoyo hadi Dar kuna umbali gani? Bila kujali uzuri au ubaya wa kilichopo kwenye huo mkataba, binafsi sioni umuhimu wowote wa bandari ya Bagamoyo; tuachanae na wana siasa kina Ndugai ambao wao wanajua bila UNAFIKI watoto wao hawawezi kwenda chooni, sisi tusio na maslahi ya kiuongozi tunasemaje kuhusu mradi huo?
Maneno kuntu kabisa haya!!

Sipika pia aliwahi kuitengua kauli yake mwenyewe Kwa kukubaliana na mhimili wa serikali kuwa Mkataba huo ni wa kinyonyaji, sasa, Kwa nini leo???

Tukumbuke pia huyu alienda Hadi China na akafika ktk ofs zilipo za wawekezaji hawa, Tunajua walichokiongea huko?

Kwa nini baada tu ya kifo cha Rais arudi kulekule kusema mradi ni mzuri na Rais alikosa washauri wazuri??

Hapo Pana tatizo kubwa, kweli wa Africa ni laana, ingawa tunalipinga hili Duniani na mbinguni
 
Unadhani IPO shida??

Ni Mkataba kupelekwa bungeni basi
Mikataba mingapi ishawah pelekwa Bungeni ? Tuanzie hapo .
Watu wakitaka mkataba huu wa bagamaoyo upelekwe bungen litakuwa Jambo zuri ambapo wengine pia watahitaji mikataba yote sasa iwe waz kuanzia ununuz wa ndege ,ujenz wa uwanja wa ndege wa chato ,mikataba ya sgr .

Hapa Sasa ndipo utaona nyeti za watu wazwaz kuwa kumbe huyu hamna kitu huyu alikuwa sahihi.

Narudia tena hakuna mwanasiasa msafi hasa hawa wa tz ,nawashangaa sana wanaomwimba jiwe kuwa alikuwa shujaa ,yaan nashangaa sana sijui ni kutojua mambo yanavyoenda .
Jk ,mkapa ,na jiwe wote ni wez waliotukuka tena Bora hata jk alikuwa anaiba lakin anakumbuka na wananchi kidogo ila sio huyo jiwe ni alikuwa fisad wa kutupwa pia akawatesa wananchi wake kwa kujificha nyuma ya neno uzarendo ,kmmk
 
Mkuu, Kwani na wewe ni wale mlioahidiwa vipasenti Vya wachina?

Hivi unajua Kwa sasa hatuwaamini kina ndugai?? Tunataka Mkataba uende bungeni na wewe unaongez a maneeno, ya nini
 
Mikataba yenye utata kama hii, ni mhimu Sana iwekwe mezani na kuchambuliwa Kwa uwazi
Sasa kwa jinsi hawa wamegeuka 360 unauhakika gani mikataba ambayo watatuwekea wazi ni ile ile ya ukandamizaji kama lengo ni kumlaumu JPM? Maana nguvu nyingi zinatumika sana.
 
Sasa kwa jinsi hawa wamegeuka 360 unauhakika gani mikataba ambayo watatuwekea wazi ni ile ile ya ukandamizaji kama lengo ni kumlaumu JPM? Maana nguvu nyingi zinatumika sana.
Kwa huyu jamaa alivyogeuka, hili nalo linawezekana
 
Mkuu, Kwani na wewe ni wale mlioahidiwa vipasenti Vya wachina?

Hivi unajua Kwa sasa hatuwaamini kina ndugai?? Tunataka Mkataba uende bungeni na wewe unaongez a maneeno, ya nini
[emoji23][emoji23][emoji23]relax ndugu yangu ,mbona nimekuunga mkono kuwa ni Jambo jema mkataba ukajadiliwa Bungeni ili tujue ukwel wa haya mambo .

Lakin pia unaelewa swala la ununuz wa ndege watu wamepiga sana kelele Kama wapigavyo kuhus huu mrad wa bagamaoyo ,sambamba na uwanja wa chato ,Sasa kuepusha unafki mikataba yote hii iwekwe waz pale Bungeni watu waichambue alaf tutatoka na majibu sahihi ili kumaliza hiz sintofaham ,maana nakuona wewe unataka mkataba wa bagamaoyo ni Jambo jema ,lakin kuna mwingine atataka wa ununuz wa ndege na uwanja wa chato

Kama wewe unayo haki ya kutaka mkataba wa bagamoyo uende Bungeni jua pia kuna mwananchi atataka mkataba wa mirad mingine nayo iwe waz hapa Sasa ndio tutaujua ukwel wote na kumaliza hiz kelele za sisi wafuas wa wanasiasa ambao tupo kizan tunapiga tu kelele wakat ukwel wanao wao
 
Mleta mada lazima ujue kwanza wabunge humo bungeni wamo kwa hisani ya Jiwe.
Alituibia na kutuvuruvugia uchaguzj wetu ili kuweka bungeni watu aina ya Ndugai, wacha wamnyooshe hata kama yupo Kaburini
 
Mleta mada lazima ujue kwanza wabunge humo bungeni wamo kwa hisani ya Jiwe.
Alituibia na kutuvuruvugia uchaguzj wetu ili kuweka bungeni watu aina ya Ndugai, wacha wamnyooshe hata kama yupo Kaburini
Sawa mkuu, ulitaka kuhitimishaje
 
Kwani huu ufisadi ndio kusema kwamba umeshindikana kabisa na hatuna njia mbadala wa kuuondoa?
 
Ndugai watu wanataka terms za huo mkataba ...hawakatai bandari ila terms zake izo za kuuza nchi...
Na kwanini basi tusiendeleze bandari zetu za Dar ,Tanga na Mtwara badala ya kukomaa Na wachina Bagamoyo!?
Ndugai Na wenzako mmelipwa nini Na hao wachina!?
Sasa Bomba la mafuta linaenda Tanga kufanya nn ikiwa Bandari hiyo haina u muhimu kama ya Bagamoyo !?
 
Hakika MATAGA safari hii lazima mtoane macho maana kila mtu anajitahidi kukimbia kujitoa kwenye chumba chenye uchafu na uozo mlichokikalia kwa miaka 6.

Ndugaye yeye kesha wakimbia maana ana platform ya kujielezea na watu wakamsikia.
 
Je, ufisadi ni matokeo ya mfumo, au ni Chama husika, au ufisadi unakuwa kwenye Damu ya mtu?
 
Back
Top Bottom