Baada ya kufika Moscow leo nimeamua kufuatilia saga la Dr. Shika, kumbe anasema ukweli

Kabisa
 
Huyu bwana ana akili timamu, hajarukwa akili kama wengi tulivyoamini.
Kabisa jamaa anajielewa sana sana sema Tatizo la watanzania wanapenda sana maisha ya kuiga....
Jamaa anaishi kwa utaratibu wake...ndivyo "alivyofundishwa" sasa wengine ukiishi hivyo oooh huna hela,kichaa...ila Mzungu akiishi hivyo hawamshangai sisi banaa....
 

Kwa maelezo haya (ikiwa yana ukweli) umekumbusha jambo moja muhimu sana: ‘Kwa kila jambo kuna majira yake…’

Nimejaribu kwenda mbali zaidi katika tafakuri (hasa kiimani), naamini kabisa kuwa kila jambo linalokutokea hutokea kwa lengo maalumu (haijalishi unajua au hujui).

Jambo ninaloamini kila siku ni kwamba Mungu anatuwazia mawazo ya amani, kutupatia tumaini katika siku zetu za mwisho.

1 Wakorintho 10:13 – “Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili.”

Inawezekana kabisa ya kwamba wakati huu unapitia majaribu mengi; kwa mfano magonjwa yameiandama familia yako, unazidi kufeli katika masomo yako, biashara yako imekwama kabisa, kukataliwa kila unakokwenda na kila unalofanya (au kama yaliyomtokea Dk. Luis Shika)… bado Mungu anakuwazia mema.

Kwa nini nimeandika ‘Kwa kila jambo kuna majira yake’? Moja ya mambo ambayo Mungu anayaangalia sana ni suala la Wakati, ndiyo maana anasema: “mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu.” – Efeso 5:16. Shida inakuja kwetu wanadamu katika suala la kutambua haya majira na kuwa na tahadhari.

Kwa kila jambo, yanayokupata ni majira tu na yanapita. Kila jambo linakuja katika maisha yako kwa lengo maalumu, ikiwemo kukua kiimani zaidi (kwa watu wa imani za kiroho).

Yusufu (mwana wa Yakobo) baada ya kupitia shida mbalimbali kutoka kwa ndugu zake na pia kule utumwani Misri, Mungu alimstarehesha na kumfanya kuwa wa muhimu sana katika taifa la Misri kwa sababu Majira ya kusumbuka kwake yalikuwa yamepita.

Urefu wa majira katika jambo litakalotokea katika maisha yako ni Mungu ndiye ajuaye, lakini mwisho wa jambo hilo upo… unachotakiwa ni kuwa mwenye Imani na Mvumilivu siku zote (kama ilivyokuwa kwa Dk. Shika – kwa mujibu wa jirani zake anaoishi nao).

Kwa kumalizia, imeandikwa katika: Mhubiri 3.1 – “Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu.”

Ninaamini kabisa kuwa hiki kilichotokea kwa Dk. Luis Shika kuhusu mnada wa nyumba za Lugumi, kukamatwa kwake na hizi habari zinazotolewa, ni jambo ambalo limetokea kwa kuwa kusudi lake limetimia ili Dk. Luis Shika apate haki yake.
 
Mmh kila jambo mnachomeka siasa tu.
Bwana wee sijui watu wamerogwa sijui mungu wangu Nani atawaondoa katika dhiki hii ya fikra. Leo nilikuwa airport exchange rate ya dollar ni kama zamani katika forex bureau lakini hapa JF ni vurulu vululu tu.
 
Wengi ni wazushi tu mitandaoni na ukute wanalipwa kwa kusambaza uongo.
Bwana wee sijui watu wamerogwa sijui mungu wangu Nani atawaondoa katika dhiki hii ya fikra. Leo nilikuwa airport exchange rate ya dollar ni kama zamani katika forex bureau lakini hapa JF ni vurulu vululu tu.
 
Mkuu aliokolewa na cia
 
Kwa maelezo ya britanicca ni kuwa hizo nyumba zimenunuliwa na CIA; Yono hili janga utakula na wa kwenu. Sisi hatumo kabisa, ohooo! Dr. Shika sio kighoma malima haya mie nimewambieni!

Kwa maana nyingine hizi ngeu ni kipigo ka cha lissu kutoka KGB sio?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…