Baada ya kufika Moscow leo nimeamua kufuatilia saga la Dr. Shika, kumbe anasema ukweli

Baada ya kufika Moscow leo nimeamua kufuatilia saga la Dr. Shika, kumbe anasema ukweli

Haiwezi fahamika tena na Dr. amekwambia hao Polisi walienda kumpekua na walikuta na bank statement ya Kampuni yao sijui ya Dr which had alot of Money... na wakaondoka nayo na baada ya kukukotoa amesema the statement tu kwenye akaunti moja ilikuwa na hela equivalent na 20 Billion na akasema TRA wanted only 3Bill plus sasa kwa nini tunaendelea kujiuliza muonekano wake na ukweli wa kazi yake.

Pia kwenye mahojiano amesema aliweza kuwatoroka watekaji japo aliteswa sana .. Kwa aina ya uteswaji aliofanyiwa mtu pekee ambaye anaweza kutoroka ni Mtu mwenye mafunzo ya hali ya juu ambayo Dr ameyapitia. kwa hiyo na ukiangalia anavyoongea yupe well organized na anaakili zake zote timamu na kwa utani tu aliwatania kuwa Kapuku kwa lengo la kuwakejeli.
Maisha ya Spy siyo Maisha ya akina Bashite .. Spy wa kweli hajikwezi , na moja ya sifa kuu zao hawapendi kupitwa na taarifa yoyote na kama umemsikia na kufuatilia mienendo yake yeye na kijiwe cheenye magazeti ni uji na Mgonjwa. Bado kuna watu wenye vichwa ngumu kwenye hiloo.....

Hiyo ni hazina tosha ambayo Nyerere pekee ndiye anayejua thamani yake ila sisi wachumia tumbo tutaendelea kuwaza na kumuwaza na kumuwazua kwa kuwa hatujui misingi ya Usalama wa Taifa
umeongea maneno mazuri na haitadhuru
 
Hata
Lancefort Ltd ni kampuni iliyosajiliwa nchini Russia miaka kadhaa iliyopita, na kwasasa haifanyi kazi kwa kipindi kirefu baada ya watendaji wake kupotea gafla kwa mazingira ya kutatanisha,
Kutoka mjini Rostov on don napokaa mpaka Moscow ni mwendo mrefu kidogo ambao ni km 1200 na zaidi, kwa mwendo wa trein ni 5hrs,
nimefika mjini moscow na kuanza kuuliza hasa legality ya kampuni hiyo ndani ya moscow na Urusi kwa ujumla, nimefanikiwa kupata maelekezo ya kukutana na Mtanzania mmoja (Elibariki Dishon) anaisha mtaa wa Tverskaya Street, ambaye kanikaribisha na kuanza kufanya uchunguzi wangu, nikaamua kwanza nipate hifadhi ndani ya hotel ya Sputnik.

Baada ya kwenda kwa watanzania wanaoishi uku nimegundua huyu mzee alipata matatizo kwa kuhisiwa ni spy wa marekani, ambaye kapandikizwa kutokea Africa, na amekuwa akitaftwa na kufuatiliwa nyendo zake zote kuanzia kwenye kampuni yake na nyumbani alipokuwa anaishi,
mke wake bi Luisa Kvonkov ndo alibanwa na kueleza kwao ni Tanzania Magu, Lakini inasemekana kwamba kuna kampuni kubwa la kimarekani aidha shirika la upelelezi ambalo liko nyuma ya kampuni ya Lancefort, ndio chanzo cha kutiwa msuko suko uko alikokuwa anamiliki kampuni hiyo,

Shirika la Lancerfort limekuwa likimilika asset kubwa nchini urusi na kwingineko duniani wakati chanzo cha hela yao hakijulikani, hivyo moja kwa moja kuhisiwa ni miongoni mwa mashirika ma spy ambao wafadhiri wake ni wamarekani ambao wana uhasama wa mda mrefu na urusi,

wametelekeza mali nyingi kukiwemo na priovate jets na maghari ya thamani,

Kupitia wapelelezi wa ndani ya urusi ambao walilichunguza shirika ambalo inasemekana rais wake ni Dr Luis Shika kwa kipindi kile, waligundua mawasiliano ya karibu na baadhi ya mashirika yafuatayo AMNESTY INTERNATIONAL, CIA, FBI , HGRE, OKLE, ambayo mara nyingi huwa ni waanzilishi wa upelelezi katija nchi nyingi,

Baada ya kugundua hayo walitekwa na kuwekwa mateka na wawili kuuwawa , mmoja wapo akiwa mkenya Edward Koinange na mwingine wa siera leone Yunusu AKhbu, Na wawili kukimbilia Tanzania lakin rais wao akapelekwa hospitali baada ya kuwatoroka akiwa ameumizwa vibaya, hakutibiwa urusi alitoroshwa kinyemela mpaka mjini Dnipro Ukraine, na kutoroshewa Tanzania,
Baada ya kufika Tanzania hakuenda moja kwa moja kwao akajificha mjini Dar es salaam, (Haya ni maelezo kwa mujibu wa mtu wake wa karibu)
Baadae kutorokea Uhispania Mjini Malaga , amekaa malaga miez 8 Na kurudi Tanzania,

Mwaka 2012 wakaidhinisha malipo kutoka marekani ambayo bado yapo kwenye mlolongo wa
kukamilisha mchakato,

WITO KWA BALOZI ZETU TUNAOMBA MUWASAIDIE HAWA WATANZANIA WANAOKUWA NA MATATIZO MUWASAIDIE

Tukiachana na Shika wapo watanzania wengi wanaokosa msaada wa karibu sana kutoka Kwa balozi zetu hizi ,

Ukisoma ukatafakadhi haitadhuru
mods mkiuacha uzi huu itapendeza

Tufanye nimemaliza


Britanicca

Hili la kuteswa naanza kuliamini! Inasemekana Dr.Shika anamakovu yakutosha mwilini.
 
passport yake imeandikwa dr ,uhamiaji wanahoji hata ukisema wewe ni msanii? passport inasema kazaliwa 1969 by 1978 yupo mbeya anafanya kazi kama medical doctor kabla ya kupata scholarship ya Russia..Nooooo
Kitu kimoja hapa ni kwamba,huyu mzee ni genius wa zamani ila kachanganyikiwa kidogo,akili za uweledi zimebaki humohumo,ana hallucinate sana,hna tofauti na yule lecturer wa cbe aliyegeuka kichaa lakini ukikutana naye anatema madini hatari
Mkuu huyu Mzee hajachanganyikiwa hata Chembe moja ..... Yaani hapo nitapingana na wewe Ukimsikia alivyowabana Polisi mpaka wameshindwa kumtuhumu na kuendelea kukaa naye mbali zaidi wamekubali ajidhamini bado unatia shakaa hapo????
 
Serikali ina mbinu nyingi za kuzima migogoro inayoendelea nchini kwa kuzua matukio yatakayokaa vichwani mwa watu.
 
[QUOTE="...
WITO KWA BALOZI ZETU TUNAOMBA MUWASAIDIE HAWA WATANZANIA WANAOKUWA NA MATATIZO MUWASAIDIE

Tukiachana na Shika wapo watanzania wengi wanaokosa msaada wa karibu sana kutoka Kwa balozi zetu hizi ,

Ukisoma ukatafakadhi haitadhuru
mods mkiuacha uzi huu itapendeza

Tufanye nimemaliza
Britanicca
Kwa taarifa chache nilizonazo ni kuwa balozi zetu nyingi hazifanyi kazi zake inavyotakiwa hata raia wakipata shida ama kure-quest chochote huweza kuchukua miaka mingi bila kusikia majibu yoyote toka kwao. Ni kama zipo kwaajili ya mambo fulani fulani machache tu. Nadhani tunahitaji seriousness katika hili.[/QUOTE]
Kama hii ya SA kazi yao ni kukusanya mapato......tuuu
 
Back
Top Bottom