Baada ya kufika Moscow leo nimeamua kufuatilia saga la Dr. Shika, kumbe anasema ukweli

Baada ya kufika Moscow leo nimeamua kufuatilia saga la Dr. Shika, kumbe anasema ukweli

Aiseee, hii ni njia ya kumrudisha barabarani tena Dr. Shika
Pole sana aisee!
 
Dr luis Shika akashika korodani na wale mbwa hawakubweka
Nb:muda ni mwalimu mkuu
 
Waandishi wa habari hawajui Ku peak up story. Hii ingekuwa story nzuri sana na western media wangezidi ku raise concern na condemnations to Russian gvt. Just wengi ni makanjanja.
Ningekuwa mwandishi ningemuhoji nakubaliana na dr kuhusu mapato na Dr na kupata story kamili nauza
 
Duuuh..., haya ndio aliyaeleza Dk. Shika, japo alisema kwamba waliomteka na kumkata vidole walikuwa wanataka dollar milioni 1.5 na sio kwamba walimtuhumu kwa uspy. Usalama wa taifa Tanzania wanakula pesa za bure tu, hii kazi uliyoifanya ilibidi wao ndio waifanye
Unajuaje jamaa pia ni miongoni mwao!??
 
Natamani mwandishi mwenye weredi kama Tido Mhando afanye nae mahojiano ya maswali ya kichunguzi. Tunaweza gundua mengi zaidi. Ila kuna kitu ndani yake anakificha na bahati mbaya wanaomhoji amewazidi sana akili so anacontrol maongezi anavyotaka yeye na wanashindwa kumchimba
 
kama vile ni agent wa CIA nikiunganisha dots

maana tuliambiwa/kuna uzi ulisema ubalozi wa tanzania ulimtelekeza lakini ubalozi wa marekani ulimtembelea akiwa hospitali kama sijakosea
Watu kama akina Dr ni hatari sana. Si wa kuchukulia poa
 
Lancefort Ltd ni kampuni iliyosajiliwa nchini Russia miaka kadhaa iliyopita, na kwasasa haifanyi kazi kwa kipindi kirefu baada ya watendaji wake kupotea gafla kwa mazingira ya kutatanisha.

Kutoka mjini Rostov on don napokaa mpaka Moscow ni mwendo mrefu kidogo ambao ni km 1200 na zaidi, kwa mwendo wa trein ni 5hrs,
nimefika mjini moscow na kuanza kuuliza hasa legality ya kampuni hiyo ndani ya moscow na Urusi kwa ujumla, nimefanikiwa kupata maelekezo ya kukutana na Mtanzania mmoja (Elibariki Dishon) anaisha mtaa wa Tverskaya Street, ambaye kanikaribisha na kuanza kufanya uchunguzi wangu, nikaamua kwanza nipate hifadhi ndani ya hotel ya Sputnik.

Baada ya kwenda kwa watanzania wanaoishi huku nimegundua huyu mzee alipata matatizo kwa kuhisiwa ni spy wa Marekani, ambaye kapandikizwa kutokea Afrika, na amekuwa akitafutwa na kufuatiliwa nyendo zake zote kuanzia kwenye kampuni yake na nyumbani alipokuwa anaishi.
Mke wake bi Luisa Kvonkov ndo alibanwa na kueleza kwao ni Tanzania Magu, Lakini inasemekana kwamba kuna kampuni kubwa la kimarekani aidha shirika la upelelezi ambalo liko nyuma ya kampuni ya Lancefort, ndio chanzo cha kutiwa msuko suko uko alikokuwa anamiliki kampuni hiyo.

Shirika la Lancerfort limekuwa likimiliki asset kubwa nchini urusi na kwingineko duniani wakati chanzo cha hela yao hakijulikani, hivyo moja kwa moja kuhisiwa ni miongoni mwa mashirika ma spy ambao wafadhili wake ni wamarekani ambao wana uhasama wa mda mrefu na Urusi.

Wametelekeza mali nyingi kukiwemo na private jets na magari ya thamani.

Kupitia wapelelezi wa ndani ya urusi ambao walilichunguza shirika ambalo inasemekana rais wake ni Dr Luis Shika kwa kipindi kile, waligundua mawasiliano ya karibu na baadhi ya mashirika yafuatayo AMNESTY INTERNATIONAL, CIA, FBI , HGRE, OKLE, ambayo mara nyingi huwa ni waanzilishi wa upelelezi katiKa nchi nyingi,

Baada ya kugundua hayo walitekwa na kuwekwa mateka na wawili kuuwawa, mmoja wapo akiwa mkenya Edward Koinange na mwingine wa Siera Leone Yunusu AKhbu, Na wawili kukimbilia Tanzania lakini Rais wao akapelekwa hospitali baada ya kuwatoroka akiwa ameumizwa vibaya, hakutibiwa Urusi alitoroshwa kinyemela mpaka mjini Dnipro Ukraine, na kutoroshewa Tanzania,
Baada ya kufika Tanzania hakuenda moja kwa moja kwao akajificha mjini Dar es salaam, (Haya ni maelezo kwa mujibu wa mtu wake wa karibu)
Baadae kutorokea Uhispania Mjini Malaga , amekaa malaga miez 8 Na kurudi Tanzania,

Mwaka 2012 wakaidhinisha malipo kutoka marekani ambayo bado yapo kwenye mlolongo wa
kukamilisha mchakato,

WITO KWA BALOZI ZETU TUNAOMBA MUWASAIDIE HAWA WATANZANIA WANAOKUWA NA MATATIZO MUWASAIDIE

Tukiachana na Shika wapo watanzania wengi wanaokosa msaada wa karibu sana kutoka Kwa balozi zetu hizi ,

Ukisoma ukatafakari haitadhuru

Tufanye nimemaliza

KUNA MENGI SITAYAANDIKA HAPA KUTOKANA NA KUJUA KWAMBA KUMBE HII ISHU NI CRUCIAL , NA KULINDA USALAMA WA DR,

PIA YATAENDELEA KUWA KUMBUKUMBU ZANGU NA KUZIPELEKA MAALI ZITAITAJIKA KWA KUMSAIDIA DR,

USIKURUPUKE KUKOPI HABARI HII, MAANA CODES ZOTE NINAZO MIMI UTASHINDWA KUITETEA,MTU PEKEE MWENYE UWEZO WA KUWEKA EVIDENCE NI MIMI, IKITOKEA UKAKOPI SEMA UMEITOA WAPI,

Britanicca
Naona kama siyo tetesi vileee...!!! Naona ni hali halisi
 
If all is true then nafikr maisha yake yamekuwa hatarin zaid kuliko mwanzo.
Ni kweli na amefanya kosa kuji expose...Warusi watamuwinda upya...

Katika hali ya kawaida ni ngumu kwa mtu wa kawaida kuweza kuvumilia mateso aliyopewa na bado akamudu kuwatoroka watejaji tena anaosema ni KGB...

Huyu mzee ni zaidi ya anavyojinasibu...

I am sorry ila kunauwezekano mkubwa sana Dr. akawa ni special agent ambaye ni well trained ila kwa sababu tusizozijua bado akili yake imetwist kidogo...
 
siwezi sema ni mbinu za ccm, ila mm niachotaka kusema hapa..huyu shika, ni mtu makini sana na ambaye anatumiwa na watu wasiojulikana kwa mission isiyojulikana hadi sasa.

Kwa website aliyoitaja jana , ukiingia huko huwezi amini ukubwa wa kampuni yake ambayo kwa maelezo yake anasema iko nchi nyingi. Pia, pale chini kwenye hyo website kuna address yao..sina hakika km huko Moscow nako wanatumia P.O.BOX... Anyway.. kwa ufupi kuna maswali mengi kuliko majibu.

Ila hyo mission ilikuwa pia planned na hao YONO.. kwani walianza kutoa warning kuwa atakaye vuruga huo munada atawajibishwa kisheria..walijuaje km siyo kuwa nao walikuwa part of the mission?? Anyway itafahamika tu..km babu wa loliyondo. Time will tell.

System yao ya adress
 

Attachments

  • IMG_20171115_201731.png
    IMG_20171115_201731.png
    36.6 KB · Views: 55
  • IMG_20171115_201810.png
    IMG_20171115_201810.png
    36.3 KB · Views: 51
Sorry off topic:
Kumbe Britanicca unakaa Rostov on don, sijui umeanza kuishi hapo lini, maana kuna kashemeji chako Fulani, kutoka Tanga, Tanzania, kamepiga medicine yake hapo kwa miaka 7, kiukweli nilikapenda sana, ila tatizo kwa kanda yatu ya Ziwa, kusubiri miaka 7, niliona ni mingi!.

Paskali
Funguka Mkuu kuhusu huyo shemeja!!! Sbb namfahamu binti wa ki Tanga anaesomea huko jina lake linaanzia na herufi J ndo huyo Mkuu!??
 
Aisee, maneno mengi yanaungana na ukweli, ila in reality unawezaje kuwatoroka KGB kindezi ndezi kama alivyosema yeye?
Hapo ndio ujue kwamba dr.shika inawezekana sio mtu wa kumchukulia poa,

Wewe mtu kakatwa vidole na kupondwa lakini kaweza kutoroka unafikili mchezo!
 
Kwa maneno hayo tu, inaonesha Dr. Luis siyo wa mchezo, hasa hilo la kubana kengele ukimwona mbwa na kutomwangalia aliyelala.
Mkuu ulikuwa bize'nini! Katoa masomo mengi tu mbona
Hili la kutuliza mbwa wakali kwa kushika pumbuiz, haukusikia?
 
Back
Top Bottom