Habari
Nipo na umri huo yaani mwezi huu ndio nimetimiza 30
Maisha yanaanza palee unapojitambua/unapopata akili timamu, haijalishi unaanza kujitambua ukiwa una umri gani? Hata ukiwa na miaka 5, 8,9 au 45 , 50 , 70 yaani palee unapoanza kujitambua ndio maisha yako yanapoanza maana utajua ufanye nini? Au uache nini? Haijalishi una mali kiasi gani? Au hauna kabsa ila unapoanza tu kujitambua ndio utajua position yako, ukae wapi? na Nani? Ufanye shughuli gani? In short upunguze pupa ya kuangaika na mambo ya ovyo na ufanye vitu vyenye mustakabadhi wa maisha yako haijalishi unapata nini? Kidogo au kikubwa ni vilee tu unajua upo kwenye njia sahihi ya maisha yako
Kujitambua ; unatakiwa uweje? Kwenye mahusiano, kishughuli zako, nani? ufatane naye na kwa sababu gani? Uongeze elimu ya namna gani? Nini unatakiwa ujue zaidi na kitakusaidia kwenye upande gani? Lini uwe wapi? Uishi vipi? Na wazazi, walezi wako ndugu na marafiki, kipi kibaya uache kipi kizuri ukifate, ulee vipi? Watoto wako na wewe ujiongoze vipi? Mambo yakikushinda ufanye nini? Nan? Wa kumuomba ushauri, uvumilie nini? Na kipi uache kuvumilia, u focus kwenye vitu gani? Na vitu gani? Uache kufocus navyo, eitha umeanza kujitambua na kuna vitu ulishaharibikiwa navyo ufanyeje uviweke Sawa, labda sifa yako unapoishi na nk, yaani ni mstakabadhi wako wa maisha kiujumla unyooke yaani mtu akitajiwa jina lako hasiweze kuweka kasoro zozote ajue huyo mtu amenyooka hana kona kona na jina lako linapotajwa kwenye makundi ya watu lisiwe na vipengele vingi walizungumzie kwa mazuri mengi na mabaya machache yasiyo na madhara
Short
Unaanza kuishi maisha palee unapoanza kujitambua yaani palee unapojitambua ndipo unapopata akili timamu na ndipo utaanza kuyainjoy maisha utakula na kuvaa kile unachopata, utalala unapoweza kulipa mpaka palee utapopata kikubwa cha kukuwezesha kupanda juu zaidi, hautamdhulumu wala kuiba cha yeyote, utavumilia situation zako zote na kuziweza kuzi endo, hauwezi kuwa mjinga kamwe
Kwenye ibada zako muombe M/Mungu akupe utambuzi binafsi, utazidi kumshukuru utajua ufanye nini? Kwa wakati gani? Ili ufanikiwe