Hana Elimu yoyote ya Uandishi wa Habari na Utangazaji ila Kitaaluma ' Jamaa ' ni ' Mbobezi ' wa masuala ya IT akiwa kafanya Degree yake ya Computer Science pale IFM kisha Post Graduate yake kafanya Finance na Accounting isipokuwa huku katika Media alijiongeza tu ' Kiaina ' hasa kipindi kile alipoanza ' Kuchambua ' mipira baada ya kuwaiga ' Wakongwe ' akina Dk. Leakey Abdallah na Yule Sapi Mkwawa.
Aliyemtambulisha na kumfunidisha masuala ya Utangazaji na hadi kumpigania ale ' Shavu ' Clouds Media Group ni aliyekuwa ' Mshikaji ' wake wa siku nyingi Mtangazaji na Mchambuzi wa Michezo wa Efm Ibrahim Masoud ' Maestro ' ambaye hata hivyo sasa wawili hao ni ' Maadui ' wakubwa japo penye Watu huchekeana. Chuki yao kubwa ilitokana na Kitendo cha Shaffih Dauda kumuibua Bwana Said Selemani a.k.a Mbwiga wa Mbwiguke na kuanza kumtumia katika Kipindi cha Michezo cha Sports Extra na kumtambulisha katika ' Fursa ' zingine kitendo ambacho kilimfanya Mbwiga akubalike haraka kitu ambacho kilimkera mno ' Maestro ' ambayo ni Mtu mwenye hulka ya kupenda ukubwa na kutukuzwa.
Chuki za ' Maestro ' kwa Mbwiga Mbwiguke zilizidi kiasi kwamba Shaffih Dauda hakupendezwa nazo hivyo pakatokea sintofahamu kidogo hali iliyosababisha ' Maestro ' kususa na kuomba likizo kumbe huku nyuma alikuwa anafanya mipango ya kuhamia Radio ' hasimu ' ya Efm.
Moja ya ' dharau ' kama siyo ' roho mbaya ' ambayo Ibrahim Masoud ' Maestro ' alikuwa akimfanyia Mbwiga ni kila ambao Timu ya Mpira wa Miguu ya Clouds ilipokuwa ikienda kucheza mechi za Kirafiki alikuwa akimnyima namba kwa ' makusudi ' Mbwiga na kama hiyo haitoshi hata katika zile ' Posho ' Mbwiga alikuwa hapewi hata senti tano hali ambayo ilipelekea sasa si tu kumuudhi Shaffih Dauda bali hata ' Watangazaji ' wengine wa hicho Kipindi ndipo ikaonekana kwamba ' Maestro ' hatoweza kuishi vizuri hapo na wenzake na kuamua ' Kusepa ' zake Efm.
Kadri ambavyo ' Maestro ' alivyokuwa akimchukia ' Mbwiga ' ndiyo kwanza alikuwa kama vile anamfanya akubalike na Wasikilizaji na Watu wengi hasa kutokana na ' hulka ' yake ya kupenda ' Kuchekesha ' na ' Kutania ' sana hali ambayo huwachanagamsha wengi. Na kama mtakumbuka hata ile siku tu ambapo ' Maestro ' aliondoka rasmi CMG ' Mbwiga ' alisikika redioni akisema namnukuu " Woyooooooooooo Paka sasa kaondoka na Panya tunatawala.....Unamchezea Mzaramo Mbwiga Weye........Woyooooooooooooo.....tema mate kushoto unafukia kulia " mwisho wa kumnukuu Mbwiga.