Baada ya Kukamatwa na TAKUKURU Shaffih Dauda ajitoa kugombea Ujumbe TFF

Baada ya Kukamatwa na TAKUKURU Shaffih Dauda ajitoa kugombea Ujumbe TFF

Hana Elimu yoyote ya Uandishi wa Habari na Utangazaji ila Kitaaluma ' Jamaa ' ni ' Mbobezi ' wa masuala ya IT akiwa kafanya Degree yake ya Computer Science pale IFM kisha Post Graduate yake kafanya Finance na Accounting isipokuwa huku katika Media alijiongeza tu ' Kiaina ' hasa kipindi kile alipoanza ' Kuchambua ' mipira baada ya kuwaiga ' Wakongwe ' akina Dk. Leakey Abdallah na Yule Sapi Mkwawa.

Aliyemtambulisha na kumfunidisha masuala ya Utangazaji na hadi kumpigania ale ' Shavu ' Clouds Media Group ni aliyekuwa ' Mshikaji ' wake wa siku nyingi Mtangazaji na Mchambuzi wa Michezo wa Efm Ibrahim Masoud ' Maestro ' ambaye hata hivyo sasa wawili hao ni ' Maadui ' wakubwa japo penye Watu huchekeana. Chuki yao kubwa ilitokana na Kitendo cha Shaffih Dauda kumuibua Bwana Said Selemani a.k.a Mbwiga wa Mbwiguke na kuanza kumtumia katika Kipindi cha Michezo cha Sports Extra na kumtambulisha katika ' Fursa ' zingine kitendo ambacho kilimfanya Mbwiga akubalike haraka kitu ambacho kilimkera mno ' Maestro ' ambayo ni Mtu mwenye hulka ya kupenda ukubwa na kutukuzwa.

Chuki za ' Maestro ' kwa Mbwiga Mbwiguke zilizidi kiasi kwamba Shaffih Dauda hakupendezwa nazo hivyo pakatokea sintofahamu kidogo hali iliyosababisha ' Maestro ' kususa na kuomba likizo kumbe huku nyuma alikuwa anafanya mipango ya kuhamia Radio ' hasimu ' ya Efm.

Moja ya ' dharau ' kama siyo ' roho mbaya ' ambayo Ibrahim Masoud ' Maestro ' alikuwa akimfanyia Mbwiga ni kila ambao Timu ya Mpira wa Miguu ya Clouds ilipokuwa ikienda kucheza mechi za Kirafiki alikuwa akimnyima namba kwa ' makusudi ' Mbwiga na kama hiyo haitoshi hata katika zile ' Posho ' Mbwiga alikuwa hapewi hata senti tano hali ambayo ilipelekea sasa si tu kumuudhi Shaffih Dauda bali hata ' Watangazaji ' wengine wa hicho Kipindi ndipo ikaonekana kwamba ' Maestro ' hatoweza kuishi vizuri hapo na wenzake na kuamua ' Kusepa ' zake Efm.

Kadri ambavyo ' Maestro ' alivyokuwa akimchukia ' Mbwiga ' ndiyo kwanza alikuwa kama vile anamfanya akubalike na Wasikilizaji na Watu wengi hasa kutokana na ' hulka ' yake ya kupenda ' Kuchekesha ' na ' Kutania ' sana hali ambayo huwachanagamsha wengi. Na kama mtakumbuka hata ile siku tu ambapo ' Maestro ' aliondoka rasmi CMG ' Mbwiga ' alisikika redioni akisema namnukuu " Woyooooooooooo Paka sasa kaondoka na Panya tunatawala.....Unamchezea Mzaramo Mbwiga Weye........Woyooooooooooooo.....tema mate kushoto unafukia kulia " mwisho wa kumnukuu Mbwiga.
Kwa kweli Ibrahim masoud Mimi sikuwa namkubali kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama neno ' Pumbavu ' ni neno Kali nadhani leo hii Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu ( 3 ) Mzee Benjamin William Mkapa ' Genius ' angeshashtakiwa na hata kuhukumiwa kwani ni neno ambalo hulipenda kulitumia sana kwa ' Wapumbavu ' wenzako ila mpaka leo ' anadunda ' zake tu. Kama haitoshi neno hilo hilo la ' Pumbavu / Pumbafu ' limetumika na Mwenyezi Mungu katika Kitabu chake Kitakatifu cha Biblia mara 22 hivyo najivunia kuwa siyo neno baya kwakuwa hata aliyetuumba amelitumia vilivyo.

Kuniuliza kwamba ama Dauda alitoa Rushwa au hapana naona ni muendelezo wako ule ule wa ' Upumbavu ' niliouona Kwako kabla kwani kama ungekuwa una ' akili ' au ' IQ ' kubwa tu usingeuliza hili swali Kwangu wakati unajua fika kwamba tayari TAKUKURU / PCCB wanalifanyia Uchunguzi na Kisheria / Kimamlaka wao ndiyo wenye dhamana nzima ya kutuambia ukweli wote wa mambo Sisi Watanzania na hasa Wadau wa Michezo.

Halafu nikiwadharau kuwa hamjui ' Kufikiri ' mnanikasirikia na kuninunia.

Mwisho kwa faida yako tu ni kwamba........

Mjinga / Ngumbaru huwa anafundishika
Mpumbavu / Popoma hafundishiki ng'o hadi Kiama

Kila la kheri.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] noma sana
 
Bila watu sahihi kuingia mabadiliko yatakujaje,
Hata juzi tu katika moja ya posts zangu kuna mahala nilimlaumu sana Shaffih Dauda kujiingiza rasmi katika kutaka ' Uongozi ' ndani ya Soka la Bongo ambalo binafsi siogopi kusema kwamba limejaa Uhuni na lina Wahuni wengi ambao hata uwezo wao wa ' Kufikiri ' ili kulinusuru Soka la Tanzania ni mdogo mno.

Tatizo Dauda alidanganywa sana na Rafiki yake ' Mjanja Mjanja ' Kiongozi wa DRFA Bwana Almasi Kasongo kuwa ajikite TFF wakati ukweli ni kwamba huyo Bwana Kasongo kuna ' mteremko ' fulani wa ' Kimaslahi ' alikuwa anautaka na ameshaanza pia kuupata kupitia ' Ndondo Cup ' hivyo muda mwingi akawa anamuhadaa Shaffih Dauda.

Sasa mambo yameshaharibika kama hivi huku ' Credibility ' yake ikiwa tayari imeshaathirika leo ndiyo anaamua kujitoa katika Kinyang'anyiro. Kwa Mtu mwenye Elimu kubwa na nzuri kama ya Dauda na Mtu ambaye anajitambua kamwe hawezi kuthubutu kugombea Uchaguzi ndani ya TFF hii iliyojaa Wahuni na Mchwa watupu.

Hili liwe fundisho kwa wengine!


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom