Nani mjinga atakayeweza ku-PM "chuma ulete".sasa hivi watu tunaishi kwa kamshahara kaliko katwa katwa sanaaa, Bodi ya mikopo 15% , ukigeuka huku nao postal bank wanakata rejesho lao.na kule sacoss kila siku wanikumbusha kwamba nimechelewesha marejesho.na zile posho zote sijui zimepotelea wapi jamani.sasa hii sh 173,174 iliyobaki ndiyo inabidi itoshe kila kitu including kodi pamoja na ada ya mwangu Mudi ya sh 10,000 kila mwezi pale chekechea.Ijapokuwa imebidi nihamie chumba cha giza yaani kisicho na umeme angalu kodi imepoapoa.usichukulie poa, mimi ni graduate afisa wa serikali ofisi nyeti.
Halafu mtu ananiambia ati ni PM
Wacha niendelee kukuita shemeji