#COVID19 Baada ya Kukubali Chanjo, na Rais Samia Kuchanja, Kiongozi yeyote anayepinga Chanjo hadharani ni 'Insubordination' na usaliti

#COVID19 Baada ya Kukubali Chanjo, na Rais Samia Kuchanja, Kiongozi yeyote anayepinga Chanjo hadharani ni 'Insubordination' na usaliti

Kiongozi wa Umma Kupinga Chanjo Hadharani Sio Tuu ni Usaliti, Bali Pia ni Insubordination!.
Futa eneo hilo paskali, hakuna anayepinga chanjo.

"NDIYO au HAPANA" nachagua/sichagui kuchanja, hiyo ni sehemu ya mkataba wako pale unapoamua, although serikali imetoa uhuru.

Unapokuja na andiko la kuwakumbusha wakuu kuwa upo, ulipaswa kukumbuka kuwa serikali hiyo hiyo inakuruhusu kupinga au kutopinga chanjo kwa njia ya kutopata chanjo.
 
Hatukumchagua... na huo Usaliti ni kwenu Nyie Wazanzibari... Kwahiyo akiwaambie Mslumu muwe kama yeye katika uislam mkakataa nao pia ni Usaliti...

Pasco always mpumba wa vu
 
Nakubaliana na wewe kwa asilimia zote kaka Pascal Mayalla . Ni tabia mbaya kupingana na kiongozi wako ndani ya chama chako na serikali yako.
Msiwe wachonganishi, kunatofauti kati ya kupinga na kutofautiana mawazo. Unaweza ukawa na wazo mbadala kwakua una experience zaidi au ya tofauti katika jambo hilo na kiongozi; je inamaanisha umempinga?

Watu wa jinsi yenu ni watu wasiowastaarabu tena hamfai kwa jua wala kwa mwezi kwakua hamna leadership skills; kiongozi mzuri ni yule anayeweza ku embrace diversity na akawa na empathy katika maamuzi yake.

Mh. Rais ameonyesha high skills katika leadership isipokuwa nyie wapambe nuksi mnaoendekeza worshiping kwa watu ambao watawapa lift katika maisha yenu.

Watu hatari kwa maendeleo ya jamii yeyote ile ya kistaarabu na yenye kujua ku engage wenzao....Mnaonyesha kutoku pevuka kwa fikra zenu tena ni ma dikteta wabaya wasiojali hisia za wenzao.

Mwandishi katika hili ni mmoja wa watu wa jinsi hiyo..Acheni kuwa makuwadi wa wenzenu, work hard earn respect, never force!
 
Kwamba msimamo wa Rais ni msimamo wa serikali! Kupinga msimamo wa 'serikali' ni usaliti! Just based on your so called insubordination!

Mpigeni risasi na huyo.
Huyo hajitambui...Anatafuta yake kwakujipendekeza asipopendeka; teuzi zimeisha rudini mtulie mkafanye kazi
 
Na hasa kama mtumishi mwenyewe ni mbunge.

Mbunge ana jukwaa pana la kushauriana na wizara ndani au nje ya bunge.

Kama hukuridhishwa na majibu ya Waziri na watalaam wake, na kama mbunge husika anatokana na chama kilichounda serikali (chama tawala) ana njia mbili, kujiondoa kwenye uongozi au kunyamaza.

Kupiga kelele nje ya jukwaa husika ni jaribio la kuhamasisha uma kuikataa serikali.
 
Magaidi yana umoja mno .

Anayeangushwa na konyagi alafu akasingizia amepigwa na wasiojulikana ni gaidi tu.

Kuna kirusi kipya cha Corona kimegundulika huko Peru
 
Lazima mwandishi wa habari mkongwe kama wewe aweze kutofautisha kati ya kupinga na kutoa elimu. Wapo watu wengi sana wanaisema chanjo na faida zake,na wapo wachache sana wanaisema chanjo na hasara zake. Sisi tusiojua lolote tunapata wapi nguvu ya kusema huyu yupo sawa na yule anapotosha?

Kazi yetu sisi ni kuangalia ni upande upi umeuelewa zaidi chukua mlengo huo fanya maamuzi. Ni kwa nini mnataka kushinikiza watu wasioelewa la kufanya wapewe elimu moja tuu ya uzuri wa chanjo?

Kwanini kila anayefungua kinywa kutaja hasaza zake tunamuona msaliti?

Binafsi naona mh.rais ameishatimiza wajibu wake wa kuhakikisha kila mtanzania anapata anachokihitaji kwa hiari yake,

aliyechagua kuchanjwa achanjwe kwa kujua ni kwa nini anachanjwa,na atakayeamua kutochanjwa naye aelimishwe ni kwa nini asichanjwe
na tuiheshimu hiari ya wahusika.

"Kwa kisukuma maana ya mayala ni njaa'' mwisho wa kunukuu.
 
Wanabodi,
Kwa vile zoezi la chanjo ya Uviko linaendelea, Kwa Maslahi ya Taifa inaendelea kujikita kwenye chanjo, leo nikiangazia hoja ya uhiari wa Chanjo. Japo chanjo ni hiari, hiari ya chanjo ni hiari ya consent kama ilivyo kwenye mahusiano ya ndoa, ndoa ni hiari, na sio ule uhiari wa choice kama kwenye uchaguzi, mtu uko huru kujiandikisha kupiga kura...
Hiari maana yake ni nini? Je, ''insubodination'' ndio lugha gani?
 
Wanabodi,
Kwa vile zoezi la chanjo ya Uviko linaendelea, Kwa Maslahi ya Taifa inaendelea kujikita kwenye chanjo, leo nikiangazia hoja ya uhiari wa Chanjo. Japo chanjo ni hiari, hiari ya chanjo ni hiari ya consent kama ilivyo kwenye mahusiano ya ndoa, ndoa ni hiari, na sio ule uhiari wa choice kama kwenye uchaguzi, mtu uko huru kujiandikisha kupiga kura
wewe naye huongozwi na akili zako.
 
Binafsi sina tatizo na fikra au mawazo yako haya. Na in fact kuhusu "insubordination" hilo halina ubishi, ni kweli kutotii na kufuata "order" ya aliye juu yako ni kosa kubwa lenye adhabu kali...
Hizi story za insubordination ndo zimetufikisha hapa tulipo kama taifa.

Kila mtu anatakiwa atofautishe aina za maboss.

Kuna maboss ambao wameanzisha kampuni zao za kufanya wanachokifanya kwa pesa zao wenyewe

huyu akikuajili,lolote atakalosema lazima uunge mkono maana mwenye maono ya kampuni ni yeye

na ukiona huyaelewi maono yake inakubidi wewe uondoke.

Hali ya hapo juu ni tofauti na viongozi wa kitaifa.Ikumbukwe viongozi hawa, taifa wamelikuta na kimsingi wananchi ndo maboss, ndo maana anatuomba ridhaa kutuongoza, iweje nikimkosoa useme ni insurbordination?

Taifa likiangamia wewe kama mtanzania unahamia wapi? Tofauti na boss mwenye kampuni kampuni ikiporomoka kwa kuwalazimisha kufuata mawazo yake mnarudi majumbani kwenu.

Ushauri wangu ni kwamba kwenye mambo ya kitaifa tuangalie hoja zinazotolewa na si vigezo kama kilichotajwa hapo juu(Insurbordination).

jambo hili limezaa unafiki kwa viongozi kisa kuogopa kutoa mawazo mbadala wasionekane wasaliti na hivyo kutuletea matatizo makubwa kama taifa.
 
Nakubaliana na wewe kwa asilimia zote kaka Pascal Mayalla . Ni tabia mbaya kupingana na kiongozi wako ndani ya chama chako na serikali yako.
Kwa hiyo kiongozi akiiba na wewe uibe sababu usipomuiga mkubwa wako Ni insubordination!!!

Akioa wake wanne na wewe unatakiwa kumuiga usipoiga Ni insubordination?
Au kusema sioi wake wanne kwenye dini yangu hairuhusu inakuwa insubordination? Hata kama mnajikomba kwenye hili mko wrong wewe na mleta mada tafuteni pointi zingine za kujikomba sip hiyo
 
Nimepapenda hapo uliposema "wana wajibu wa kuwalinda wengine" tatizo linakuja huu wajibu utatekelezwa vipi?

Wakati mwingine itabidi utekelezwe kwa lazima, na ukifanya hivyo wajinga watazidi kupata sababu ya kuwadanganya wenzao wasichanjwe sababu zina "matatizo", hili litazidi kurudisha nyuma juhudi za kuwachanja watu....
Hahaha kuwalinda wengine kivipi jamani jamani wakati kuta kuwa na makundi mawili waliochanjwa "walio salama" na ambao hawajachanjwa sasa ambao hawaja chanjwa wanawaweka kwenye hatari kina nani sasa

Sent from my SM-G570F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom