#COVID19 Baada ya Kukubali Chanjo, na Rais Samia Kuchanja, Kiongozi yeyote anayepinga Chanjo hadharani ni 'Insubordination' na usaliti

#COVID19 Baada ya Kukubali Chanjo, na Rais Samia Kuchanja, Kiongozi yeyote anayepinga Chanjo hadharani ni 'Insubordination' na usaliti

Mkuu Micho , kwanza naunga mkono watu kuwa open minded na kuhoji kila kitu ili wajiridhishe ndipo wachanje, hilo jukumu la kuhoji liachwe kwa sisi wananchi wa kawaida, kwenye uongozi kuna kitu kinaitwa a Collective Responsibility, mkiisha kubaliana jambo, jambo hilo linakuwa ni jambo lenu wote, kama wewe hukubaliani nalo, una two options, ama unyamaze kimya uendelee kuwa mmoja wao, au ufanye kitu kinachoitwa à fall back position, kwa kujitoa ndipo upinge hadharani. You can't est your cake and have it. Gwajiboy lazima achague upande, its either with us or against us, he can't have both!.

"tunaokolewa kwa imani" kwa kuamini tunachoambiwa na Viongozi tunao waaminia. Samia ndie kiongozi wetu Mkuu, amechanja na ametushauri tuchanje kwa hiyari, tuchanje.

Kwa vile tunamuaminia Samia, na amechanja, kitendo cha Gwajiboy kupinga chanjo hadharani na kuhamasisha watu wakatae chanjo ni insubordination, ni kumsaliti Samia. Kitendo hicho ni dhambi ya usaliti, ni dhambi mbaya, hivyo soon wote tutashuhudia karma ya dhambi hiyo ya usaliti.
P

Kwahio akichanja Raisi maana yake ni salama kwani yeye kaitengeneza si kashauriwa tu, hujawahi kusikia Raisi kashauriwa vibaya. kuna msemo unasemwa... mwanasiasa akikuambia jua nje linawaka toka ukaliangalie....yeye mwenyewe amesema chanjo ni imani una haki ya kuiamini au laah.. hakulazimishi na hajalazimisha mtu

Gwajiboy ana kofia mbili naamini ana haki ya kusemea kondoo wake kitu anachokiamini na kondoo wana haki ya kumsikiliza au laah..they have got a mind of their own..

Mkanganyiko ni mkubwa kwa wananchi tulishaambiwa na viongozi hao hao km chanjo bado tusubiri kwanza hazifai tena wakatupa sababu kwanini hazifai na tukamuamini mwendazake sababu mwenyewe alikuwa ni mkemia anaingia lab anajua machemical reactions wakatuambia hii chanjo teknolojia yake inamaswali mengi haijakaa vizuri inaingia kwenye cell za mwanadamu..siku chache baadae zinafaa na viongozi hao hao waliosema hazifai nini kimebadilika aisee na ninaamini kuna scientist hapa nchini ambao hawaamini kwenye hii chanjo lakini hawawezi kusema..Sasa Gwajiboy km anaona watu wamebanwa mbavu na yeye ana ubavu let him stand out na aseme anachokiamini ni hiari kuchanja hajafunga mtu mikono asiende...

By the way efficacy ya chanjo bado scientist wanaihoji vaccinated people are still getting infected and some wanapoteza maisha...stay healthy good people..
 
Wanabodi,

Hii ni mada mwendelezo wa mada hii ya wiki iliyopita

View attachment 1881240
Kwa vile zoezi la chanjo ya Uviko linaendelea, Kwa Maslahi ya Taifa inaendelea kujikita kwenye chanjo, leo nikiangazia hoja ya uhiari wa Chanjo. Japo chanjo ni hiari, hiari ya chanjo ni hiari ya consent kama ilivyo kwenye mahusiano ya ndoa, ndoa ni hiari, na sio ule uhiari wa choice kama kwenye uchaguzi, mtu uko huru kujiandikisha kupiga kura, au kutokujiandikisha, na hata ukijiandikisha, bado uko huru kupiga kura au kutokupiga kura, hiyo na uhiari wa choice, lakini uhiari wa chanjo ni uhiari wa consent, kama ulivyo uhiari wa kuingia kwenye mahusiano ya ndoa, ukiisha ridhia kuingia kwenye ndoa, uhiari wa ndoa unaishi hapo, kinachofuata ni wajibu, kuihudumia ndoa sasa inakuwa sio hiyari tena, ni wajibu, mwanaume lazima awajibike kumhudumia mkewe, sio hiri ni wajibu, na wanandoa hao wana wajibu wa kuihudumia ndoa, ndia maana kwenye ndoa za kiafrika kuna baadhi ya malalamiko ya wanawake wa kizungu, huku kwetu huwezi kuyasikia. Wenzetu wazungu, hata baada ya kuingia kwenye ndoa, ili mwanandoa kupata huduma za kindoa, lazima aombe tena ruhusa, aridhiwe ndipo akubaliwe, hivyo hiari inaendelezwa hadi kwenye huduma wakati ni wajibu.

Hivyo ndivyo ulivyo uhiari wa kwenye hii chanjo ya Uviko, kwa vile lengo la chanjo ni kinga, kuzuia kuenea kwa uviko, una chanja ili kujikinga wewe na kuwakingi wengine, mtu unapokataa kuchanja, sio tuu unahatarisha maisha yako, bali una hatarisha kuwaambukiza wengine, hii ya kuwakinga wengine sasa sio choice, ni wajibu. Ili kupata chanjo ile hiari ni kwenye kuridhia tuu, yaani ku consent, na sio hiari ya choice kuamua uchanjwe au usichanje, hivyo baada ya nchi kukubali chanjo, na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na Amiri Jeshi Mkuu, wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Mhe Rais Samia Suluhu Hassan Kuchanja, akifuatiwa na viongozi, kitendo hicho japo ni hiari, hiyo ni silent marching order, amri ya kimya kimya, hivyo viongozi wote wa umma, wana wajibu wa kuchanja, sio hiari!. Jee viongozi wetu wote wa umma, wanajua, kuwa baada ya nchi kuibali chanjo na Rais Samia na viongozi wakuu kuchanja, kiongozi yoyote wa umma, anayeipinga chanjo hadharani, kitendo hicho ni Insubordination?. Tunamuomba Mhe Rais Samia, "Please stop this nonsense !"

True Story Yangu na Insubordination.
Mimi nilikuwa mtumishi wa umma pale TBC, enzi hizo TVT, nikiendesha vipindi vya siasa, "Ulingo wa Siasa", tayari nchi yetu ilikuwa ndani ya mfumo wa vyama vingi, hivyo mtu kuwa mtumishi wa umma, hakuna ulazima kuulizwa uko chama gani. Wakati Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2000, katika vipindi vyangu niliwakaribisha wanasiasa. Kwa vile CCM ndio chama tawala na Tanzania tunaingia chaguzi zote huku CCM ikiwa tayari na uhakika wa ushindi, hivyo nikiwaalika wagombea wa CCM kwenye urais, wanakuwa busy, after all si uhakika wa ushindi upo, ila ukiwaita wapinzani ni fasta.

Baadhi ya watu wakajenga dhana kuwa huyu mwendeshaji wa kipindi, Pasco Mayalla ni pro-oppostion, anawapendelea wapinzani!. Hawajui kuwa ukiwaalika CCM, wanakuwa busy. Nikaenda kupiga kambi Zanzibar, huko nako hali ni ile ile kwenye wagombea urais.

Baada ya uchaguzi, ikafanya tathmini, na wafanya tathmini, ikaonekana Pasco Mayalla ni kama alipendelea upinzani!. Wakatumwa watu kutoka huko walikotumwa, wakaja pale TBC, nikaitwa ofisini kwa Mkurugenzi, nikatambulishwa kwa wageni, na kuulizwa mimi ni chama gani?. Kwanza nilishangaa swali gani hili?!, kwani kuwa mtumishi wa umma, kuna takwa la chama?!. Nikawajibu watu wale ukweli wangu kabisa kuwa mimi Pasco Mayalla sina chama chochote!. Kumbe jibu hilo ni kama kosa!. Mahojiano yakaishia hapo. Baada ya muda, nikaletewa barua ya summary dismissal kwa kosa la insubordination!. Barua ya termination kabla haujakabidhiwa, yule mtu wa despatch anaanzia getini, anapewa FFU wawili wenye silaha, na kuja huku wameshika silaha standby!. Ndipo unakabidhiwa barua, kisha askari hao wanakusindikiza hadi kwenye meza yako. chukua kilicho chako, kabidhi ofisi, kisha unasindikizwa hadi nje ya geti!. Kiukweli nililia!.

Kesho yake nikaenda Utumishi kuuliza hiyo summary dismissal imekaaje, ndipo nikajulishwa kwa mujibu wa utumishi wa umma, ukifukuzwa kazi kwa insubordination, hata kama ni majungu, hakuna popote pa kwenda, you just pack and go!.

Kiongozi wa Umma Kupinga Chanjo Hadharani Sio Tuu ni Usaliti, Bali Pia ni Insubordination!.
Kwenye vita yoyote ya kitaifa, kama ilivyo vita ya Corona, ili kushinda vita, viongozi wote, lazima wasimame pamoja na kuwa kitu kimoja na kuzungumza kwa kauli moja. (must stand as one). Tanzania kama Taifa likiisha kubali Chanjo ya Covid Ndio Maslahi ya Taifa, Viongozi wote wa umma, wanakuwa bind na a collective responsibility clause, they must support, msimamo wa serikali.

Na kama kuna kiongozi yoyote wa umma, hukubaliani na chanjo, hakubaliani na msimamo huo wa serikali, wa kuhimiza Watanzania tuchanje, then kiongozi huyu unapaswa kunyamaza kimya. Kama rais anesema tuchanje, anahimiza Watanzania tujitokeze kwa wingi kwenda kuchanja, sio tuu ili kujikinga sisi wenyewe, bali kuwakinga wengine na kulikinga taifa, kitendo cha kiongozi yoyote wa umma, kujitokeza hadharani, kuwapotosha Watanzania tusichanje, huku ni kwenda kinyume cha rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ni highest order of insubordination ambayo haipaswi kuvumiliwa au kufumbiwa macho.

Kitendo cha kupingana na msimamo wa serikali wazi wazi ni usaliti, mtu wa aina hii anatakiwa kushughulikiwa haraka iwezekanavyo kama wanavyoshughulikiwa wasaliti wengine wote, na jinsi kosa la insubordination linavyoshughulikiwa na hatua ya kwanza ni kiongozi wa aina hiyo, kuachia ngazi kama mtumishi wa umma.

Kama mtu aliweza kupewa summary dismissal kwa kudhaniwa tuu kuwa sio mwenzetu, jee mtu anayepingana na rais wazi wazi katika jambo lenye maslahi kwa taifa, anaachajwe kuendelea kuipotosha jamii?!. Au Tanzania tuna watu wa aina mbili, the touchables, na untouchables?. Tunakuomba sana Mhe, Presidaa SSH, P'se Stop This Nonsense!.

Wasalaam

Paskali
Kabla sijachangia uzi huu, naomba nikuulize wewe Mayalla, je umesomea shule ya seminary gani?
 
Binafsi sina tatizo na fikra au mawazo yako haya. Na in fact kuhusu "insubordination" hilo halina ubishi, ni kweli kutotii na kufuata "order" ya aliye juu yako ni kosa kubwa lenye adhabu kali...

Lakini hebu tujiulize, kuwa, Je ni kweli kila kitikacho kwa mkubwa huyu ambaye ni binadamu tu aliye sawa na wewe kwenda kwa subordinates wake ni kamili/sahihi/,ukweli na hakina kasoro au hatari yoyote...?

Itakuwa ni ujinga na upumbavu wa hali ya juu kama mtu anakubali na kutii chochote toka kwa binadamu mwenzake na kisha kukitenda bila kwanza kukiweka au kuliweka jambo hilo vipimo vya kiusalama wa kwanza ROHO na kisha MWILI...!

Nimalizie comment yangu kwa kusema hivi;

Kwamba, hii ishu ya chanjo ya UVIKO 19 ni vita ya katika falme mbili wa MUNGU YEHOVA na wa SHETANI/IBILISI. Ni vita/mgogoro wa kiimani. Ni majira ya kubagua kondoo na mbuzi...

Ni ishu ya mtu binafsi kufanya uchaguzi awe au afuate upande upi kwa maslahi na usalama wake wa sasa na wa baadaye...

It's a big challenge. Lakini wenye misuli ya imani katika Kristo Yesu watashinda...!

Asante
Asilimia95 ya watu wote duniani hawana ufahamu wa kinachoendelea kuhusu wao, agenda hizi mimi nazifahamu tangu nilipoanza kua Conscious mwaka 2012.
Na utimilifu huo unakwenda kutimia, na watakuwa wameisha chelewa sana.
Kupiga chanjo ni suala la kufa na kupona..
Waliochanja na hawaonyeshi kupata madhara wanadhani wapo salama, but time will tell! Sio kwamba watakufa la hasha, ila dunia nzima wakichanjwa na kuisha...mitambo ikiwashwa na kuwa connect wote waliochanja kwenye global computer wataanza kuona vitu vipya inside their brain kama ujio wa .....
 
Kwani hizo aspirin, chloroquine, Antibiotics hatukuletewa? Tumepewa chanjo nyingi tu, kwani hizo mlitengeneza ninyi wamatumbi? Acheni ujinga ninyi malofa, hakuna kitu Tanzania ilichoweza kutengeneza kuanzia sindano za kushona, hadi njiti za kibiriti kila kitu mmetengenezewa tu. Halafu mnajifanya mnajua....Ebu acheni ujinga na upuuzi ninyi watu. Tukubali tu hakuna tunachokijua hata kimoja, Niambie kitu gani waafrika au watanzania tumegundua? Kila kitu kina side effects zake, hata huo wali na ugali tunaokula unapitishwa kwenye ini ili ichujwe sumu. Hata usipokula dawa au kuchomwa chanjo, mwili unakuwa na madhara yake ndani kwa ndani kwa hiyo nyamaza tu kwani hujui chochote.

Unaongea nini wewe

Kwahio km hujui ndio usiulize maswali, utumie tu sababu umeletewa, umesoma ili iweje...inavyotengeneza antibiotic ndio sawa inavyotengenezwa chanjo..Chanjo ni dawa?!
 
Hili sakata la Gwajiboy na Gwajigirl linaendelea. Gwajiboy anamdharau Mama Samia, anamdhalilisha Waziri, shemeji yake, na sasa anawadhalilisha Wanyiramba wote. Japo Kanda ya Ziwa wanadharau sana wanawake, lakini hili la Gwajiboy kumdharau hadi rais wa nchi na Mwenyekiti wa chama chake CCM ni dharau iliyopotiliza!.
Akiendelea kuachiwa tuu atafikia mahali atakuwa ni unstopable na itakuwa too little too late.
P
 
mtahangaika bure tu kushawishi watu wachanjwe kiukweli watu wengi sn hawana imani kbs na hayo machanjo yenu hilo ni jambo la kwanza

jambo la pili wanasikilizia hao wachache waliochanjwa watapatwa na madhara gani baada ya miaka fulani ili wajue kilichomo ndani

jambo la tatu linalowashangaza sana wananchi inakuwaje baadhi ya watu waliochanjwa baada tu ya kuchanjwa hawachukui siku si nyingi wanakufa badala ya kuwakinga ?!!...hapa kuna mifano mingi ya watu hao kufa baada siku chache tu kuchanja

jambo la nne linalostaabisha kbs ni hili la watu kukomaliwa kwa kila namna hata kwa pesa wachanjwe kuna nini cha siri hapo ?!!! huo uchungu wa huruma kwa wanadamu imekuwaje umekuja leo ?!!...mbona miaka nenda rudi watu wanakufa sana kwa magonjwa mengi tu huruma hii haijawahi kuonekana!!!!...miaka nenda rudi wanasayansi wanagundua kinga nyingi tu watu hawatafutwi kwa udi na uvumba kama kipindi hiki juzi tu hapa tumeona kampuni ya moderna imetangaza majaribio ya kinga ya HIV watu 56 tu wanahitajika tena hawabembelezi hata kidogo wakati ukimwi pia unaua mamilioni ya watu kama covid tu

kuna mambo mengi sana ya kujiuliza kabla ya kuamua kuchanja ...hivi karibuni pia tumeona chama cha republican cha marekani kiliibua masuala tata sana juu ya ushiriki wa marekani na china kwenye hili jambo la uviko kuwa hizi nchi mbili zilishirikiana kwa siri sana juu ya gonjwa hili sasa bado haijulikani ilikuwaje hivi virusi wakaviachia kwenye maabara zao za siri na mwisho wa siku mmarekani anataka kumuachia msala mchina jambo ambalo naye hataki kusikia ukaguzi tena wa WHO baada ya ule ukaguzi wa kwanza wa kupangwa kubuma
 
Mkuu Ngalikihinja , hiari, ni consent, yaani lazima uridie wewe mwenyewe, mwisho wa uhuru wako ni pale ambapo hautaingilia uhuru wa mwingine, hivyo unapokataa kuchanjwa ni hiyari yako, lakini pia una wajibu wa kuwalinda wengine, hivyo usipochanjwa, wewe ndio utawaharisha wengine kwa kuwaambukiza, hivyo hata kama wewe hutaki chanjo, lakini kwa ajili ya wengine, hiyo chanjo inageuka wajibu.
Ndani ya chama CCM na ndani ya serikali, kuna kitu kinachoitwa uwajibikaji wa pamoja, a collective responsibility, mkiisha kubaliana jambo, then wote mnasimama pamoja, kama wewe hukubaliani nalo, unanyamaza, ukiamua kulipinga hadharani, unapaswa kwanza u fall out, then pinga!.

Rais wako na Mwenyekiti wa chama wako, awahimiza Watanzania tuchanje, halafu wewe ni mwanachama, kiongozi, unawaambia watu wasichanje!, hiyo ni insubordination na usaliti.
If you have your cake and you love it, you have only two options, if you love it so much and you desire to eat it, una mawili, ama control your desires usiile hiyo keki ubaki ukiiangalia tuu na itakuwepo, au tamaa ya kula keki imekuzidia, ukaila hiyo keki, then its gone!, you can't have both, you cant eat your cake and still have it.
P
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] yaani unachekesha kweli ....yaaani mtu amechanjwa hlf tena mimi nisiyechanjwa niwe kihatarishi kwa aliyechanjwa?!!!...aisee kuwa serious ....narudia tena yaani mimi niwe hatari tena kwa aliyechanjwa?!! ...huoni hiyo chanjo ni useless kama inashindwa kumkinga mchanjwaji ina maana gani sasa?!!...hapo hkn kinga bali kuna kitu kingine tu ndani yake kinachotafutwa kupitia mgongo wa chanjo ...chanjeni wajinga wajinga
 
Public servants ni watu wote wanaolipwa by taxpayers money, ndani yao wapo watumishi wa serikali, wa wizara, wakala na idara zinazojitegemea, watumishi wa mashirika ya umma, na vyama vya siasa vinavyopokea ruzuku.

Rais wa JMT ndio mtumishi no.1, akiishasema tuchanje, wewe mtumishi wa umma usiokubali chanjo, usichange ila jikalie tuu kimya, usianze kuhamasisha in public watu wakatae chanjo, hii ni insubordination, na kumsaliti bosi wako!.

Hata Jeshini, baada ya CinC kuchanja, huko ni amri, sio hiyari.

Uhiyari wa chanjo ni kwenye kupata tuu ridhaa, consent, kama ilivyo ndoa, ukiisha ridhia kuingia kwenye ndoa, huna mamlaka juu ya mwili wako kwenye kuihudumia ndoa, ukitaka huduma, lazima upewe, ule sasa unakuwa ni wajibu.

Kwa vile kutokuchanja, hakukuhatarishi wewe pekee bali wewe unayekataa kuchanja, unawahatarisha wengine, hivyo unawajibu wa kuwalinda wengine. Kama unavyowajibika kwenye ndoa, kuna siku mwanandoa mmoja hajisikii kuwajibika, yuko kwenye bad mood, au amechoka sana, lakini huduma inapohitajika hujikuta japo hataki lakini lazima ahudumu. Vivyo hivyo kwa wasiotaka chanjo, wana wajibu wa kuchanja ili kuwalinda wengine, hivyo ni hiyari yenye wajibu.

P
kwa hiyo mtu akae kimya asimuhabarishe ndg yke,mke wake,mtoto wake n.k juu ya madhara ya jambo fulani eti kisa bosi aseme hvyo na iwe hvyo !!! kwamba kama ni sumu kwa kuwa boss amesema basi wote mpokee sumu!!!...huu utakuwa ni utaahira wa ajabu kbs
 
Hakuna kitu unajua bw mdogo.
Acha kubwabwaja. Kama hataki angekaa kimya akatae yeye na familia yake. Kupinga au kutangaza mawazo tofauti hadharani au kanisani au kuhutuba watu chini ya mtu ni mti ndio insubordination kabla ya kujibiwa au nini ajiuzuli tu aachie ubunge.

Mtu aliyepishana na mamlaka wakati nadhani wewe Duniani ulikuwa haupo ni Edwin Mtei Gavana wa Benki kuu Tanzania aliyemvimbia Nyerere kwamba masharti ya IMF anakosea msimamo wake.

Nyerere alipokataa ushauri Mtei kaandika barua ya kujiuzulu.

Gwajiboy anatishia kujiuzulu na bla bla kibao, wakati yupo tofauti halafu anauma na kupuliza. Na anakunja mil11 kila mwezi.
kwamba nyie mna haki ya kuwaaminisha watu wote kwamba chanjo ni salama!!!!...halafu wengine hawana haki ya kuwaambia watu wote kuwa chanjo si salama?!!..nyie nendeni mkachanje mchukue muweke na za akiba kbs mbn ni rahisi sn makasiriko ya nini kwenye afya za wengine wasiotaka?!!
 
Hili sakata la Gwajiboy na Gwajigirl linaendelea. Gwajiboy anamdharau Mama Samia, anamdhalilisha Waziri, shemeji yake, na sasa anawadhalilisha Wanyiramba wote. Japo Kanda ya Ziwa wanadharau sana wanawake, lakini hili la Gwajiboy kumdharau hadi rais wa nchi na Mwenyekiti wa chama chake CCM ni dharau iliyopotiliza!.
Akiendelea kuachiwa tuu atafikia mahali atakuwa ni unstopable na itakuwa too little too late.
P
Mama yangu alinambia nisioe Wanyiramba, eti kwa kuwa wana roho mbaya, sijui kama kuna ukweli.
 
Nakubaliana na wewe kwa asilimia zote kaka Pascal Mayalla . Ni tabia mbaya kupingana na kiongozi wako ndani ya chama chako na serikali yako.
Upuuzi mtupu, yani mtu akubali tu kufuata vitu kisa mamlaka imesema?. Acheni kutetea ujinga kila mtu ana hiari ya kuchanjwa au Laa. Watanzania wengi wamechagua Laa.
 
Chanjo ni kama bange, mama Samia baada ya kudungwa jana kaanza kuwafananisha wanawake na wanaume, Gwaji girl kaanza kuleta story za kutestiwa kitandani, Spika kaanza kutaka wasiochanjwa wahojiwe.

Uzombi umeanza mapema kuliko tulivyo tarajia.
 
Upuuzi mtupu, yani mtu akubali tu kufuata vitu kisa mamlaka imesema?. Acheni kutetea ujinga kila mtu ana hiari ya kuchanjwa au Laa. Watanzania wengi wamechagua Laa.
Ukikubali kuwa mtumishi Basi hayo Ni baadhi ya matakwa ya hiari yenye ulazima
 
H
kwamba nyie mna haki ya kuwaaminisha watu wote kwamba chanjo ni salama!!!!...halafu wengine hawana haki ya kuwaambia watu wote kuwa chanjo si salama?!!..nyie nendeni mkachanje mchukue muweke na za akiba kbs mbn ni rahisi sn makasiriko ya nini kwenye afya za wengine wasiotaka?!!
Hujaelewa kabisa yaani Gwajiboy pamoja na Uaskofu wake kuwa wa ajabu kama kinyonga( angalia jana kasema kama yeye alimtafuna yule binti mrembo xccc)

Yaani angejiuzulu sio swala la haki. CCM ndio inatawala na Gwajiboy anakula m11 kupitia CCM hivyo aandike barua ya kujiuzulu kwanza lwa kupishana na maamuzi ya chama. Hapa hakuna ligi ya kubishana,bi kuelewa utaratibu ukoje.

Hakuna mtu anaechapwa viboko kulazimisha chanjo. Ila mwenye sauti ya kuongelea chanjo ni chama kinachotawala. Kama hutaki semea nje ya chama kwa kujiizulu kwanza.
 
Binafsi sina tatizo na fikra au mawazo yako haya. Na in fact kuhusu "insubordination" hilo halina ubishi, ni kweli kutotii na kufuata "order" ya aliye juu yako ni kosa kubwa lenye adhabu kali...

Lakini hebu tujiulize, kuwa, Je ni kweli kila kitikacho kwa mkubwa huyu ambaye ni binadamu tu aliye sawa na wewe kwenda kwa subordinates wake ni kamili/sahihi/,ukweli na hakina kasoro au hatari yoyote...?

Itakuwa ni ujinga na upumbavu wa hali ya juu kama mtu anakubali na kutii chochote toka kwa binadamu mwenzake na kisha kukitenda bila kwanza kukiweka au kuliweka jambo hilo vipimo vya kiusalama wa kwanza ROHO na kisha MWILI...!

Nimalizie comment yangu kwa kusema hivi;

Kwamba, hii ishu ya chanjo ya UVIKO 19 ni vita ya katika falme mbili wa MUNGU YEHOVA na wa SHETANI/IBILISI. Ni vita/mgogoro wa kiimani. Ni majira ya kubagua kondoo na mbuzi...

Ni ishu ya mtu binafsi kufanya uchaguzi awe au afuate upande upi kwa maslahi na usalama wake wa sasa na wa baadaye...

It's a big challenge. Lakini wenye misuli ya imani katika Kristo Yesu watashinda...!

Asante
Barikiwa.
 
Uzi mzuri ..

Pascal, I agree with you 100% especially serikali inavyopaswa kuwachukulia hatua watumishi wake wanaoiponda chanjo waziwazi..

Namna ulivyoondolewa TBC binafsi imeniuma but that's life..POLE kwa yote Brother.
Pascall unampa pole ya nini. Yule hakuwa mtu wa kuajiriwa tena ni brand heavy kali kupita wote akina millard, michuzi, kitenge n.k wote hao aliwatangulia kwa mbali. Alitakiwa awe na kituo chake anatoa ajira na hizi mada tunaongelea kwake.
 
Back
Top Bottom