ndege JOHN
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 25,030
- 61,298
Weekend tarehe 23 iliyopita nilitembelea sehemu moja karibu na mji wa kupang ila ni vijiji vya nchi ya Timor-Leste nikiwa na rafiki yangu kwao palikuwa na kama kumbukizi ya mwaka mmoja wa kifo cha babu yake nikamsindikiza kuna tukio moja liliniacha na maswali mengi sana kuhusu mambo ya tamaduni na akili ya binadamu. Nilikuta baadhi ya ndugu zake watatu wanapenda sana kula nyama ya mbwa.
Mimi sikuigusa kabisa, niliishia kula nguruwe ilikuwepo na vyakula vingine. jioni kama saa moja hivi tukaanza kukaa nje tunavuta sigara na kunywa pombe.
Mara Ghafla mmoja wa wajomba zake akaanza kutoa ulimi nje na kuhema kama mbwa anavyofanya akiwa amechoka.
Mwanzoni nilidhani ni utani, lakini alifanya kwa muda hadi nikaanza kupata wasiwasi. Kadri usiku ulivyoenda mbele mida ya saa 5 usiku kaka wa rafiki yangu naye akaanza kutoa sauti za kulia kama mbwa. Siyo kubweka kabisa, ila ilikuwa sauti inayofanana sana na ya mbwa anayelia.
Mimi labda nilifikiri ilikuwa ni sehemu ya utani wao baada ya kunywa pombe ila nilipouliza nikaambiwa kula nyama ya mbwa kunamfanya mtu awe na tabia za mbwa na sio mara ya kwanza kufanya hivyo.