GE2025 Baada ya kuliwa kichwa na Tume, Luhaga Mpina aibukia Mahakama Kuu kwenye kesi ya Lissu

GE2025 Baada ya kuliwa kichwa na Tume, Luhaga Mpina aibukia Mahakama Kuu kwenye kesi ya Lissu

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Haiingii akilini hata kidogo, kwenye ushindani sawia haipo sawa hata kidogo.
Eti mgombea wa nafasi ya uraisi anateua mkurugenzi/mwenyekiti wa the so called "tume huru ya uchaguzi" halafu anaenda kushindanishwa na wengine, sio haki wala sio sawa!
Hii nchi ina mambo ya ajabu sana shida ni katiba mbovu iliyopo
 
Muheshimiwa mwenyekiti wetu NTU WA DILI ,kachukua ushuru kwenye chombo ya kanali afu 20 kuniziba mie n' domo kanipa afu tatu ,kataaa brazaa kataaaa!!
 
kwenye kuoendekeza majina hapo kuna watu watachomeka watu wao
Nazani mara baada ya serikali na mihimili mingine ya nchi kukubari reform wanadai reform watapendekeza njia nzuri na sahihi wanayoitaka ya kupata tume huru
 
kwenye kuoendekeza majina hapo kuna watu watachomeka watu wao
Kuna njia zaidi ya milioni ya kumpata mtu sahihi,

Tunaweza kufanya hivi sheria iweke wazi kwamba lazima majina yasiwe na uhusiano wa moja kwa moja na chama chochote cha siasa (mfano: mtu asiyewahi kushika nafasi ya uongozi ndani ya chama kwa miaka 10 iliyopita).

Au Majina yanapendekezwa hadharani, wasifu na rekodi zao ziwekwe wazi ili wananchi wafuatilie.

Au badala ya Jaji Mkuu peke yake kuteua majina, kamati ya iNEC iwe na wawakilishi wa vyama vyote vya siasa, mahakama, asasi za kiraia, na vyombo vya dini.
 
rushwa ni kitu chenye nguvu sana mkuu hata tume ikiwa huru kuna ukandamizaji utendelea kwa wasiokuwa na nguvu ya kiuchumi
 
rushwa ni kitu chenye nguvu sana mkuu hata tume ikiwa huru kuna ukandamizaji utendelea kwa wasiokuwa na nguvu ya kiuchumi
Rushwa tu? Tunaweza kuipunguza kwa kiwango kikubwa mno. Tatizo nchi yetu ina viongozi wenye tamaa sana na bahati mbaya zaidi hata wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama kashfa ya ubadhilifu wa fedha, rushwa na ufisadi vinawaandama.

Kuna njia nyingi za kupunguza rushwa kisheria na zikafanya kazi. Tunaweza kufanya kama Finland na Denmark kwao serikali inagharamia kampeni kwa vyama vyote ili kuwe na usawa wa rasilimali. Pia wameweka Mipaka ya matumizi ya kampeni (mfano: mgombea haruhusiwi kutumia zaidi ya kiwango fulani cha fedha) Wagombea watoe hesabu za pesa walizotumia hadharani, zihakikiwe na mdhibiti.

Wakikiuka hiyo sheria, Adhabu kali za rushwa ya uchaguzi zifuate mkondo wake.. Si faini tu, bali kufutwa mgombea (Au afungiwe lifetime asigombee tena), au hata kifungo cha gerezani.
 
Bora ajitoe kwenye hilo genge la wahuni kwani muasisi wa ACT Wazalendo na mwanamtandao Zitto Kabwe anamuombea kura mgombea wa CCM Samia Suluhu.
 
Bora kuwa na Chama kimoja na Nchi iongozwe kifalme tu

Maana kama haupo kwenye circle yao, huwezi kupata nafasi ya kuongoza
Tungekuwa na Jeshi lenye watu wazalendo ilitakiwa Jeshi lichukue nchi na kuvifuta vyama vyote na baada ya miaka mitano ndiyo viandikishwe vyama vingine chini ya usimamizi wa Jeshi. Tumechoka huu upumbavu wa kikundi kidogo cha wanamtandao kuibagaza Tanganyika yetu.
 
Back
Top Bottom