#COVID19 Baada ya kumaliza Maombolezo ya kumuaga mpendwa wetu Magufuli, tujiandae na maambukizi mapya ya COVID-19

#COVID19 Baada ya kumaliza Maombolezo ya kumuaga mpendwa wetu Magufuli, tujiandae na maambukizi mapya ya COVID-19

Kuna watu wanapenda sana Tanzania ipatwe na majanga ila dua la kuku halimpati mwewe

Msiba wa maalim Sefu mlisema hivyo na hadi Leo watu wanadunda tu Pemba hawana COVID19 wala COVID20
 
Labda wewe ila mtaani shughuli zinaendelea kila siku na hakuna vifo wala maiti kuzagaa mitaani,

Iyo corona mnayoipamba kwa ngonjera kila siku utazani mmelipwa kuihubiri Mtaani hatuioni, kawambie na waliokutuma kwamba huku maisha yanaendelea kwa furaha.

% kubwa ya watanzania wote wanatumia daladala kama sehemu ya usafiri, wana banana humo kama walivyokuwa uwanjani.

Kwa hesabu ndogo tu, Daladala zinazobeba watu tena wakiwa wamebanana Tz kwa siku moja ni Mara 5 ya hao walokwepo hapo uwanjani tena wakiwa wanatoka maeneo tofauti tofauti, ayo maafa unayohubiri yangekuwa yameshaonekana kitambo tu

Ombi langu kwa watu kama wewe, Acheni kutisha watu kwa mihemko yenu.
Well said, ukweli ni asili mia ndogo ya watu wanao kufa kutokana na ugonjwa wa kovid - takwimu zinaonyesha kwamba asilimia 98.5% ya watu walio ambukizwa kovid wanapona, wanao kufa mara nyingi ni wale wenye matatizo ya kiafya waliyo kuwa nayo kwa siku nyingi.

Makampuni yanayo zalisha chanjo za kovid ndio wanatia chumvi mno kwa lengo la kuleta taharuki Duniani ili waweze kuuza chanjo zao zenye walakini mkubwa - ingekuwa kovid inaua kila mtu Duniani anaye ambukizwa na kugonjwa huo, hapo kweli Dunia inge ogopa sana - lakini mambo hayako hivyo hata kidogo, ukiangakia utakuta watu wengi actually wana maambukizi ya mafua kuliko kovid - tusitishane, ugonjwa wa kovid hupo kweli lakini si kwa kiwango kinacho kuzwa na media za magharibi kwa lengo la kuzipigia debe chanjo zao ili ziuzike kirahisi.
 
Kwa kile nilichokishuhudia uwanja wa uhuru jana na leo, na kile kinachokwenda kufanyika Dodoma, Zanzibar, Mwanza na Chato cha watu kutokuchukua tahadhali ya ugonjwa wa Corona. Tutarajie nchi yetu kukumbwa na maambukizi mapya ya COVID-19.


View attachment 1731117

Ninasihi sana viongozi wetu tuchukue tahadhali kabla taifa halijaingia kwenye hatari huko mbeleni. Corona ipo na haina utani kabisa.
Nzi wa kijani watapungua sana
 
Unawajua Watz wewe hata akitoa tamko watu hawatavaa barakoa,si tuko nao huku tunawaona.Hata hiyo Covid hawaizungumzii kabisaa watu wanaendelea na mambo yao tuu
 
Inamana ww Babu zako, Bibi zako walikufa kwa Corona au bado wapo hai? Hakuna kiumbe Kitachobaki Duniani... Usipokufa kwa Corona utakufa kwa Ajali, Usingizini, Malaria, Ukimwi, Cancer etc.
Ndipo upeo wako ulipokomea? Yale mabango ya tahadhari ya corona yaliyowekwa na serikali kila kona wadhani ni mapambo? Akili zenu mwazijua wenyewe!!
 
Kwa kile nilichokishuhudia uwanja wa uhuru jana na leo, na kile kinachokwenda kufanyika Dodoma, Zanzibar, Mwanza na Chato cha watu kutokuchukua tahadhali ya ugonjwa wa Corona. Tutarajie nchi yetu kukumbwa na maambukizi mapya ya COVID-19.


View attachment 1731117

Ninasihi sana viongozi wetu tuchukue tahadhali kabla taifa halijaingia kwenye hatari huko mbeleni. Corona ipo na haina utani kabisa.
Kwa ujazo huu ilitakiwa zoezi lifanyike usiku na mchana kama wakati wa kumuaga Hayati baba wa Taifa Nyerere
 
Usiiamini sana barakoa, usiiamini sana chanjo ila jali afya yako kwa kuhakikisha Kinga yako iko vizuri na mwamini Mungu.
 
Mi na familia yangu si wajinga kama nyie wapuuzi miloenda jazana uwanjani bila tahadhari
Nakuunga mkono kwa asilimia 100.wanacheza na huu ugonjwa.wamejazana kila sehemu kana kwamba tunaishi mbinguni na sio duniani.Nchi nyingi hata za jirani zimeanza kutususa na kututenga.we nenda Nairobi tu,wakikujua Mtanzania wanakukimbia.
 
Back
Top Bottom