Baada ya kumsafirisha mke najisikia amani, furaha na wepesi wa kutosha. Ndoa inahitaji umakini usiomithilika

Baada ya kumsafirisha mke najisikia amani, furaha na wepesi wa kutosha. Ndoa inahitaji umakini usiomithilika

ubahili ndiyo unaomsumbua huyu. Hiyo tigopesa anapata vipi fedha kama hakumpa password mwenyewe?

Hayo ya watoto kutoa matusi alitakiwa na yeye awe na msimamo asiruhusu hivyo vitu.
Daah unaongea vitu kirahisi kama hivyo vitu havipo huyo jamaa kaongea ukweli na wengi wapo kwenye hiyo kadhia wewe unajifanya yeye ndio kakosea...
 
Naona akili zako zimemezwa na papuchi
Sio mimi mkuu, huyo mleta mada aliwaza papuchi ndio maana akaoa.
Angeangalia vigezo vingine nje ya papuchi naamini asingemuoa huyo mkewe hasa kwa hizo tabia za mkewe alizoziainisha yeye mwenyewe hapa.

Mimi nimemuonya tu kuwa huko alikompeleka hata hicho kigezo kilichomfanya amchague huyo mke wake(papuchi) kinaenda kutumika.
Tena kinaenda kutumika na watumiaji wenye matumizi mabovu. "Hawajali!
 
Hili ni libahili ukionaga majitu hayanaga shukrani ujue haya.

1. Libahili
2. Halijui kubembeleza mwanamke ukimwona anavaa kiuchi uchi anakutega ila hujui mapenzi nini ,hujui kuwa mke anataka nini wewe ni ugomvi tu.

3. Unamchepuko unayemtunza ndio maana mkeo akifanya hivyoo unaona keroo.

So acha umalaya tulia kwa mkeo . Uenjoy maisha ya ndoa
 
Kuna watu watakwambia ukimchunguza saaana huwezi mla , kumbe tunafanya makosa makubwa sana yanayokuja kutugharimu huko mbeleni ..

Kuijua historia ya mwenza wako kabla ya ndoa ni jambo la muhimu sana kwa mustakabali wa maisha ya mbeleni.

Me/ke ukishatambua madhaifu ya huyo umtarajiaye kuja kuishi naye ni jambo la msingi sana. Tofauti na sasa watu wanaingia kwenye ndoa kwa kujifanya wanakondoo kumbe ni mafisi tu.
 
Na ukiona mke anadokoa visenti vidogo ujue humpi pesa kwaajili ya matumizi yake binafsi.
Next time nunua Tv mbili moja weka chumbani uwe unapumzika huko bila bugudha. Tv ya sebuleni waachie mke na watoto. Ila mke wako ana mdomo nadhani hicho ndo ulimpendea tangu mwanzo.

Wengine tunatamani kupewa likizo hata ya siku mbili twende kwetu hatupewi .
Natamani nipewe likizo🤣🤣🤣 nikitoka asubuhi, Ile jioni nikirudi namkuta mume kakonda, analalamika amenimiss🤣🤣🤣
 
Umuofia kwenu!!

Kama mada ilivyo, nimempeleka kwanza kwao kwa muda usiopungua miezi miwili.....akajifunze kitu (kama ni mwenye kujifunza). Siku moja tu baada ya kutoka kwake;........

1. Leo kwa mara ya kwanza, katika kipindi cha mwaka mmoja na nusu, nimefanikiwa kutulia nyumbani saa mbili usiku na kuangalia taarifa ya habari mwanzo mwisho. Kabla, ilikuwa sikai maana nikibadilisha channel tu na kuweka kituo changu pendwa cha Star TV kuangalia taarifa basi manung'uniko yenye kukera huanza kukimbizana kutoka nje ya kinywa chake.......
"Tutaacha vp kubadilishiwa channel wakati TV sio yetu na hata bei yake hatuijui..."
"Hata kuzima we zima tu, nini kubalisha channel" Dah

2. Nimepumzika kushuhudia mabegi na makwapa ya mke wangu yakionwa na watoto muda wote awapo nyumbani. Jitihada za kumrekebisha ili aendane na desturi yangu, daima huenda sambamba na ugomvi....

3. Nimepumzika kuona sura ya kununanuna pale ninapotoa maelekezo....

4. Udokozi wa vielfu tano tano vyangu katika tigopesa yangu utakoma kwa muda....

5. Nitapumzika kusikia matusi kama 'nyoko we' n.k yanayotolewa kwa watoto kila siku....

6. Nitafurahia vichenji vinavyobaki katika matumizi madogomadogo na kuziweka mezani. Kwa kawaida hivi hutoweka dakika moja tu baaada ya kuviweka.....hata kama akiwa amelala basi huamka ghafla na kuvichukua kisha kulala tena.

Mbona nina furaha sana sasa?!!! Atarudi kweli?!!!!! Arudi ili nije kupata stress tena?!!!!!!!

Ndoa..........mh!
Ezeulu Kweenu!!!
 
Hii kitu sielewagi,hata umpe mwanamke milioni akifua suruali na kukuta buku kumi ataibeba tu.
 
Back
Top Bottom