Baada ya kunusurika kifo, Irene Uwoya aokoka!

Baada ya kunusurika kifo, Irene Uwoya aokoka!

Mshindi namba 5 wa Miss Tanzania 2006, muigizaji na mjasiriamali Irene Pangras Uwoya, 35 amempokea Yesu kuwa bwana na mwokozi wa maisha yake!

Muigizaji huyo aliyezaliwa na kulelewa katika Ukatoliki, alifikia uamuzi huo baada ya kukumbwa na maswahibu yaliyotishia uhai wake.

Mjane huyo wa marehemu Ndikumana, ambaye walifunga ndoa takatifu ya Kikristo mwaka 2008 hadi walipotengana 2013, kisha kuolewa na Dogo Janja kwa ndoa ya Kiislam Oktoba 2017 kabla ya kutengana mwaka mmoja baadaye, anaonekana kweli kudhamiria katika imani yake hiyo mpya baada ya kuonekana akiwa amebadili mwenendo hadi wa mavazi yake!

CHANZO NI UZINDUZI WA FILAMU …!
Kama unafuatilia vyema tasnia ya filamu chini, utakuwa umesikia kuhusiana na ujio wa filamu mpya kutoka kwa muigizaji huyo, Olema ambayo ilizinduliwa Septemba 8 mwaka huu jijini Arusha.

Uzinduzi huo ulioambatana na mkusanyiko mkubwa wa nyota wakubwa kutokea tasnia hiyo na wengineo jijini hapo, ulifana kwelikweli!
Pesa ilitumika, pesa ikaonekana katika uzinduzi huo!

Irene aliyeonekana kuwekeza nguvu na pesa nyingi katika filamu hiyo, alikuwa na mipango mingi, ikiwemo uzinduzi katika majiji makubwa nchini.

Hata hivyo, mipango sio matumizi… Mipango hiyo ilivurugika alipotua jijini Mwanza kwa ajili ya maandalizi ya uzinduzi wa filamu hiyo jijini hapo, hali yake ya kiafya ilibadilika ghafla!

Hali ilikuwa mbaya sana, uamuzi wa haraka ukachukuliwa kumuwahisha Dar Es Salaam kwa ajili ya uangalizi zaidi wa kimatibabu.
Irene aliugua sana, hali iliyopekea kupungua kimwili.

USHIRIKINA WATAJWA…
Kama mjuavyo palipo na wengi pana mengi, kila mmoja ana lake juu ya kilichomkuta Uwoya katikati ya uzinduzi wa filamu yake hiyo aliyowekeza hela nyingi.

Irene alipokea sifa kedekede kutoka kwa wadau wa filamu nchini baada ya kuonesha njia ya mabadiliko na mapinduzi baada ya tasnia hiyo kudorora, inasemekana wenzie hawakupendezwa na hilo, wakafanya ya kufanya!

Tazama pichani, hapa ni kabla ya kuuguaView attachment 2855638


Baada ya kuugua… Huu ndio muonekano wake mpya.View attachment 2855639

KUOKOKA SIO KAZI…
Kumrudia Mungu ni jambo jema, na yafaa kupongezwa katika hilo. Lakini haizuii sisi kujiuliza kutokana na aina ya maisha yake iliyozoeleka…
Atadumu katika Ulokole? Vipi zile bata na machawa wake ndio zimekwisha? Aristoste na wenzie watafute cha kufanya mjini boss kaokoka?

Irene ameonesha mabadiliko katika matanuzi kwani hata birthday yake mwaka huu ambayo husheherekea kila mwaka ifikapo Dec. 18 haikuwa kama ilivyozoeleka wakati mwingine akikodi eneo zima la starehe na kufanya kufuru ya hela!
Tumuombee!


Kupitia chanzo changu cha kuaminika,

Nifah
Kifo kikifika kimefika, hata uende kulala kwenye nyumba za ibada,
 
Wanasema huwezi kumtambua kwa kumtazama ama kwa mavazi yake kujua kama ameokoka, ila juzi kinguo alichovaa Mlimani City hakioneshi kuwa ameokoka.

It's like alikuwa anawinda hela za wastaafu [emoji2089][emoji2089]
Irene hawezi kuacha kuvaa nguo fupi maana Ndo maisha yake yule
Afu kuokoka Kwa siku hizi kimchongo tu
 
Nifah,bongo movie na kurogana ni chupa na mfuniko etiii...
Wanaroga mnooo...mengine hatusemi tutafungua mambo ya watu ila sitashangaa km walimpiga chumaa...mwenzao
Masikini Irene ujue aliweka hela nyingi sana?
Na alikuja kwa kasi kweli!

Baada ya kuugua hata sioni akiendelea na chochote kuhusu hiyo filamu!
 
Back
Top Bottom