Baada ya kuona nimepata mirathi kawa mpole sana

Baada ya kuona nimepata mirathi kawa mpole sana

Acheni uchoyo wanawake wenzangu.

Akimnyima, hizo hela zitaisha tu, kama sio kwa matumizi mabaya basi kudhulumiwa au kupata hasara.

Japo sijajua ugomvi wao ukwapi, lakini kutoa 2M ni rahisi sana.

Maisha mafupi haya.
Unauhakika wewe ni mwanamke!? Hebu jichungulie, u r so different kwakweli
 
Miezi kadhaa nyuma niliondokewa na baba mzazi,,, tukaanza process za mirathi, wiki iliyopita tumepata kama mil 18 kila mtu.

Sasa huyu shemeji yenu simuelewi hapo nyuma alibadilika akawa haeleweki tangu mirathi imetoka kawa mpole mapenzi motomoto simuelewi kaamua kujirekebisha au nii hii mirathi anaiwinda.

Hapa nimetulia pesa nimeweka bank sijajua naifanyia nini.
Hamna kitu huyo Kama we Ni mfanyakazi nahujawahi kufanya biashara usijaribu kuifanyianakushauri moja Kati ya haya
1)Tafuta mahali ununue nyumba ndogo ambayo ipo Eneo ambalo Kodi ya pango inaridhisha ununue upangishe
2)Tafuta mahali ununue viwanja kadhaa sehemu ambayo imeanza kujengeka nunua hata vitatu vya mil 5,weka mipaka vizuri hata ya michongoma baada ya miaka mitanno uje uvipige Bei,Bei itakuwa imepanda hata mara tano
3)Badili hizo pesa ziwe katika dola ya marekani zitakuwa Kama dola 7,800/= fungua fixed account katika Moja ya benki kubwa Kila mwaka riba utapata asilimia Kati ya 5 Hadi 10 huku pesa yako bado ipo.
Kwa mwaka riba ikiwa asilimia 10 utapata dola (780 kwa mwaka wa Kwanza)ndani ya miaka mitanno utakuwa na dola 3900+7800+riba ya dola zingune utakuwa na dola 12,000++ na zaidi sio haba itakuwa Ni sawa na umejega nyumba umepangisha


. ......Huyo mtu wako Hana wemaa Ni mnafki kaona pesaa ndo anajisogeza atakupigaa......
 
Ufanye mpango muachane na huyo mwanaume. Vihela vyako visimfanye umnyanyase.

Kama mmefunga ndoa peaneni talaka ule pesa zako kwa amani.
Ungeweza kupitia nyuzi zangu za nyuma ungeelewa nachokimaamisha
 
Naomba Utuliee.

Shemeji yetu ni SABAYA ALIYECHANGAMKA.

ninao ushuhuda wa Watoto wa Ndugu mmoja ivi.

Baada ya Mirathi, Bidada akawa amepata 30+M

Jamaa yake akamdandiaa, penzi mototmoto , demu akawa kipofu.

Alipigwa KO moja hiyoooo , akabaki mweupe, mbaya zaidi, TUMBUA TUMBUA YA JPM ,IKAPITA NAYEEE TENA.

SIKU hizi wana wanajipigia tuuu ili demu aishi.
Kumfanyia mtoto wa watu ukatili wa namna hii ni dhambi kubwa, yaani unamtia umasikini na unamkimbia hakika nakwambia malipo yake utayasikia!
Mungu sio wa kumchukulia poa kiasi hicho!
 
Ok fanya hivi nipe million 3 niizungushe mwisho wa Mwezi faida tunapata million 5 hizo 3 nakurudishia alaf ile mbili tunaendelea kuizungusha unakua unachukua 1.5M kila mwezi
Screenshot_20211109-144611.jpg
 
Miezi kadhaa nyuma niliondokewa na baba mzazi,,, tukaanza process za mirathi, wiki iliyopita tumepata kama mil 18 kila mtu.

Sasa huyu shemeji yenu simuelewi hapo nyuma alibadilika akawa haeleweki tangu mirathi imetoka kawa mpole mapenzi motomoto simuelewi kaamua kujirekebisha au nii hii mirathi anaiwinda.

Hapa nimetulia pesa nimeweka bank sijajua naifanyia nini.
Mambo ya ndoa bana,mnapendana lakini inafikia mahali mnaanza kuviziana kama Chui na Swala,mko ndani huyu anawaza pesa za mwenzake huyu anawaza jinsi ya kumsaliti mwenzake,hapa ndio nagundua kuwa,chanzo kikubwa cha misuguano ndani ya ndoa ni kupishana kwa roho,mwanzoni roho zinakuwa zimeungana,lakini baadaye inapofikia zinaachana ndio tabu inapoanza.Nini kifanyike basi, Maombi na sala ni muhimu hapa,tena kwa kudhamiria...
 
Unauhakika wewe ni mwanamke!? Hebu jichungulie, u r so different kwakweli

Kwahiyo unafikiri wanawake wote tuna tabia zinazofanana?

Ha ha ha

Mi sioni shida akimpa tena sio mkopo....mumewe? Hata kama wamegombana afanye tu just for her peace na kwaajili ya Bwana.
 
Sister nakushauri nunua bond za serikali hautojuta ,fixed account unapewa riba ndogo sana yaani Sana. Mfano nishawahi taka kuweka 35M nikaambiwa for 3 months nitapata 135k nikaona ni ujinga. Mana riba zake kwa mwaka ni 3-5% kwa mwaka. So piga hesabu. Ila bond za serikali unapata riba from 12-17 kutegemeana kuwa unaikopesha serikali muda gani. Kumbuka huwa ni kuanzia miaka mitano ndipo unapopata riba nzuri ingawa Kuna bills and notes za miezi ama under one year.
Ila Kama hautolkuwa na shida hela iyo. Utalipwa riba yako semi annually or quarterly.

Kama ukiona vipi Kuna jamaa akatoa ushauri mzuri Sana kuwa nunua ardhi Ila usiwe na haraka.
Mana ardhi huwa hakuna inflation Kama hizo bonds or fixed account.ardhi inaweza ikakupa maisha. Mana ikitokea Boss mmoja amependa eneo lako unatangaziwa day la maana unashawishika unaiuza.yaani ulinunua 3-5M ukauza even above 100M. Mana inategemeana na potentiality ya eneo husika.
Ardhi ni Mambo yote Mana kila siku Kuna watu wanaongezeka kuhitaji ardhi ya kujenga kumbuka saivi vijana walio chini ya 20yrs hao after 10yrs wote wenye from 15+ watahitaji kuwa na malazi so laizma land value iongezeke
Mkuu Serikali hihiii inayoamka na sera tofauti kila siku aisee hapana... Kama Kuna biashara siwezi Kufanya basi ni inayohusisha taasisi za serikali
 
Mkuu Serikali hihiii inayoamka na sera tofauti kila siku aisee hapana... Kama Kuna biashara siwezi Kufanya basi ni inayohusisha taasisi za serikali
Kununua bond za serikali ni kuwa umeikopesha serikali wanakulipa riba.
Kama vipi nunua USA government bonds zipo mpaka za miaka 25
 
Back
Top Bottom