PreGE2025 Baada ya kupitisha mchango Makalla aagiza Siglada kwenda kupatiwa matibabu Dodoma

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Wamchukue tu jumla awe mwanaccm
Yote haya kwa sababu alikuwa kambi ya Mbowe? Halafu mnajidai mnataka kuponya majeraha? Kwa matendo haya kwa nini Mwenyekiti wenu asionekane kama dikteta uchwara? Mna tofauti gani na CCM ambao ni mwiko kutofautiana na Mwenyekiti?

Amandla...
 
Wakuu,

Vituko haviishi, yaani ni mwendo wa kuchapwa na matukio tu! Ikitoka episode moja tunaletewa nyingine kali zaidi iliyoongezwa na pilipili:BearLaugh::KEKLaugh:

Uvivu tu wa kuchambua na kuwatia nguvuni waliotajwa kwenye ripoti ya CAG🌚🌚

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

=====

Sakata la kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Siglada Mligo, aliyepigwa na kujeruhiwa na Mlinzi katika kikao cha Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Taifa John Heche mkoani Njombe, limevuta hisia za Chama cha Mapinduzi (CCM) baada ya kada huyo kukosa msaada wa haraka.

Pia soma: Pre GE2025 - CCM yamchangia fedha za matibabu BAWACHA Seglada aliyepigwa na mlinzi

Katibu wa NEC, Itikadi na Mafunzo wa CCM Taifa, Amosi Makala baada ya kuchangisha fedha kwaajili ya matibabu lakini ameenda mbali zaidi kuwaagiza uongozi wa chama hicho mkoa wa Iringa kushughulikia safari ya Mligo kwenda Dodoma kwa ajili ya matibabu zaidi baada ya hali yake kubadilika.
Hiyo ndiyo Ambulance iliyomleta mgonjwa?
Kila kitu kimekuwa usanii nchi hii.
 
Kwa hiyo nyinyi shida ni yeye kuchangiwa? Mgonjwa tangu lini anaomba mchango? Mmemtelekeza ndio maana mkawapa upenyo CCM kutumia hiyo nafasi. Halafu sasa mnataka kumuangushia nyumba mbovu? Huyu bado ni mwanachama wa CDM na hakustahili kufanyiwa mlivyomfanyia. Nyinyi kila mtu anayetofautiana na kambi lenu mnampakazia kuwa ametumwa. Sigrada alikuwa ana malalamiko yake lakini kwa sababu alidiriki kumsifu Mbowe mbele ya Mwenyekiti basi mnafanyia fitna ili aonekane msaliti.Mnakiharibia chama chenu.

Amandla...
Ww sio mwanachama wa cdm wala kwenye kikao hukuwepo, hayo ya kwamba alimsifia Mbowe kwenye huo mkutano umeyajuaje? Je kama sio mmemtuma na akashindwa kucheza script yake vizuri, hicho kilikuwa ni kikao cha kumsifia Mbowe?

Unataka cdm wamtibu, kwani wanachama wote wa cdm wanaopata matatizo huwa wanatibiwa na chama? Je ccm mmewahi kuwatibu wafuasi wengine wa cdm ambao chama hakijawatibu? Kama sio mlimtuma inabidi mbebe hii kadhia ni nini? Bado mko kwenye siasa hizi za propaganda za kizamani?
 
Ni suala tu la muda kabla ya huyo Kamanda wa Bawacha kuvua gwanda, na kuvaa gunia lenye rangi ya kijani na njano.
Hiyo hasa ndio tamati ya mchezo wote huu.

Na gwanda halitovuka hivi hivi, litaambatana na maneno ya fedheha, kejeli na 'kuvujisha' siri.

Sitostaajabu kamanda huyu ndio akaja na 'siri' ya mpox na ebola.

CCM wanaishiwa vibaya mno.
 
Yote haya kwa sababu alikuwa kambi ya Mbowe? Halafu mnajidai mnataka kuponya majeraha? Kwa matendo haya kwa nini Mwenyekiti wenu asionekane kama dikteta uchwara? Mna tofauti gani na CCM ambao ni mwiko kutofautiana na Mwenyekiti?

Amandla...
Mashuhuda waliokuwepo wanasema alijiangusha tu na kupiga makelele kwamba kapigwa.
 
Ww sio mwanachama wa cdm wala kwenye kikao hukuwepo, hayo ya kwamba alimsifia Mbowe kwenye huo mkutano umeyajuaje? Je kama sio mmemtuma na akashindwa kucheza script yake vizuri, hicho kilikuwa ni kikao cha kumsifia Mbowe?

Unataka cdm wamtibu, kwani wanachama wote wa cdm wanaopata matatizo huwa wanatibiwa na chama? Je ccm mmewahi kuwatibu wafuasi wengine wa cdm ambao chama hakijawatibu? Kama sio mlimtuma inabidi mbebe hii kadhia ni nini? Bado mko kwenye siasa hizi za propaganda za kizamani?
Mimi sio mwanachama wa CDM lakini ni mmojawapo wa watu watakaoombwa kura na vyama vyote kama uchaguzi utafanyika. Na ni mmoja wa watu ambao CDM inawashawishi kuunga mkono campaign yao ya " No Reforms No Elections ". Au mnategemea wanachama wa CDM peke yao ndio watakaoifanikisha?

Sagrida alimsifia Mbowe katika shughuli za Bawacha za siku ya Mwanamke. Alisema hivyo mbele ya Mgeni wa Heshima wa shughuli yenyewe. Na alirekodiwa na akarushwa You Tube.

Hakuna mahali niliposema kuwa CDM wamtibu. Nilichokisema ni kumjulia hali. Inaelekea bado mko kwenye giant za uchaguzi mlioshinda. Ile ya character assassination.Kila mtu akitofautiana na nyie ni ama ni CCM au ametumwa na CCM. Propaganda za kizamani ndio hizo za " zidumu fikra sahihi za Mwenyekiti "! Shida ni kuwa katika upofu wenu hamlioni hilo. Sagrida sio adui wa CDM. Nyinyi ambao hamtaki kufikiri ndio maadui wa CDM. Mnadhani mnajenga kumbe mnakiharibia.

Kampeni pole Sagrida. Haitawagharimu kitu. Hata kama hamumpendi.

Amandla...
 
Mashuhuda waliokuwepo wanasema alijiangusha tu na kupiga makelele kwamba kapigwa.
Sawa. Alijiangusha wakati anaingia kwenye kikao? Na anapata faida gani kusema Noel alimpiga? Kuweni na aibu kidogo.

Mnafanya yale yale ambayo mlifanyiwa. Tunakumbuka tulivyoambiwa kuwa mnajiteka wenyewe. Na Mwenyekiti wenu aliposhambuliwa tukaambiwa alianguka kwa sababu alikuwa amelewa.

You should be better than this.

Amandla...
 
Mimi sio mwanachama wa CDM lakini ni mmojawapo wa watu watakaoombwa kura na vyama vyote kama uchaguzi utafanyika. Na ni mmoja wa watu ambao CDM inawashawishi kuunga mkono campaign yao ya " No Reforms No Elections ". Au mnategemea wanachama wa CDM peke yao ndio watakaoifanikisha?

Sagrida alimsifia Mbowe katika shughuli za Bawacha za siku ya Mwanamke. Alisema hivyo mbele ya Mgeni wa Heshima wa shughuli yenyewe. Na alirekodiwa na akarushwa You Tube.

Hakuna mahali niliposema kuwa CDM wamtibu. Nilichokisema ni kumjulia hali. Inaelekea bado mko kwenye giant za uchaguzi mlioshinda. Ile ya character assassination.Kila mtu akitofautiana na nyie ni ama ni CCM au ametumwa na CCM. Propaganda za kizamani ndio hizo za " zidumu fikra sahihi za Mwenyekiti "! Shida ni kuwa katika upofu wenu hamlioni hilo. Sagrida sio adui wa CDM. Nyinyi ambao hamtaki kufikiri ndio maadui wa CDM. Mnadhani mnajenga kumbe mnakiharibia.

Kampeni pole Sagrida. Haitawagharimu kitu. Hata kama hamumpendi.

Amandla...
Cdm hawataki kura yako boss wana kura za kutosha. Nimekuuliza hukuwepo kwenye kikao cha cdm huyo dada aliyepigwa. Umejuaje sababu za ndani, unakuja na story za kwamba alimsifia Mbowe.

Cdm hawahitaji kwenda kumjulia hali huyo dada na macamera, nyie ndio mnahitaji kwenda na macamera maana mnamtumia kwa ajenda zenu. Toka amepigwa kama mnavyosema, umeona ndugu zake wakiwa kwenye macamera wakimjulia hali, ama ccm ndio ndugu zake sana? Hizo siasa za kizee endeleeni nazo nyinyi, lakini cdm hawana muda huo. Na hakikisheni anapona, na ikibidi mpeni card ya chama chenu aje awasaidie kumsifia Samia kama alivyokuwa anamsifia Mbowe. Una lingine?
 
Wakuu,

Vituko haviishi, yaani ni mwendo wa kuchapwa na matukio tu! Ikitoka episode moja tunaletewa nyingine kali zaidi iliyoongezwa na pilipili:BearLaugh::KEKLaugh:

Uvivu tu wa kuchambua na kuwatia nguvuni waliotajwa kwenye ripoti ya CAG🌚🌚

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

=====

Sakata la kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Siglada Mligo, aliyepigwa na kujeruhiwa na Mlinzi katika kikao cha Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Taifa John Heche mkoani Njombe, limevuta hisia za Chama cha Mapinduzi (CCM) baada ya kada huyo kukosa msaada wa haraka.

Pia soma: Pre GE2025 - CCM yamchangia fedha za matibabu BAWACHA Seglada aliyepigwa na mlinzi

Katibu wa NEC, Itikadi na Mafunzo wa CCM Taifa, Amosi Makala baada ya kuchangisha fedha kwaajili ya matibabu lakini ameenda mbali zaidi kuwaagiza uongozi wa chama hicho mkoa wa Iringa kushughulikia safari ya Mligo kwenda Dodoma kwa ajili ya matibabu zaidi baada ya hali yake kubadilika.
Wataenda kumuua ili watengenese doa kubwa sana kwa uongozi wa cdm hawa watu hawajawahi kua rafiki
 
Kwa vile ubunifu na ujuzi wa Mtanzania hapo ndiyo mwisho wake wanaweza kufanya hivyo ili wailetee nchi madawa na vifaa tiba hospital zote, bima ya afya kwa wote, ajira kwa vijana wote na kushusha bei za vifaa vya ujenzi nchi nzima, maji safi na salama kila Kijiji na kitongoji.
 
Cdm hawataki kura yako boss wana kura za kutosha.
Sawa. Nawatakia kila la kheri.
Nimekuuliza hukuwepo kwenye kikao cha cdm huyo dada aliyepigwa. Umejuaje sababu za ndani, unakuja na story za kwamba alimsifia Mbowe.
Shida ni uelewa. Nimesema moja ya sababu Sagrida anafanyiwa visa ni ile ya kumsifia Mbowe mbele ya Lissu, wewe unakazania kuniuliza kama nilikuwepo kwenye kikao cha Njombe!

Cdm hawahitaji kwenda kumjulia hali huyo dada na macamera, nyie ndio mnahitaji kwenda na macamera maana mnamtumia kwa ajenda zenu.
Kwa hiyo CDM walienda kumjulia hali? Kumbe ni kweli amelazwa hospitali!
Toka amepigwa kama mnavyosema, umeona ndugu zake wakiwa kwenye macamera wakimjulia hali, ama ccm ndio ndugu zake sana?
Ndugu zake wanahusika vipi hapa? Na kuna ubaya gani wa mtu kuwa na ndugu ambao ni CCM? Mbona Mwenyekiti wenu kaka yake ni CCM?
Hizo siasa za kizee endeleeni nazo nyinyi, lakini cdm hawana muda huo. Na hakikisheni anapona, na ikibidi mpeni card ya chama chenu aje awasaidie kumsifia Samia kama alivyokuwa anamsifia Mbowe. Una lingine?
Ndio umemaliza hapo? Kupona ata
pona kwa mapenzi ya Mungu. Au unataka asipone?

Uchaguzi umeisha. Mmeshinda. Lakini bado mnawaandama ambao hawakuwaunga mkono. Halafu mkiitwa madikteta uchwara mna kasirika. Mna tofauti gani na hao mnaozunguka kuwananga kuwa hataki demokrasia?

Kwa heri. Una nipotezea muda.

Amandla...
 
😄😄😄😄ila Drama za kijani
Kweli njaa mbaya Sana unaweza kukutoa utu. Soon huyo demu anaunga juhudi
 
Wakuu,

Vituko haviishi, yaani ni mwendo wa kuchapwa na matukio tu! Ikitoka episode moja tunaletewa nyingine kali zaidi iliyoongezwa na pilipili:BearLaugh::KEKLaugh:

Uvivu tu wa kuchambua na kuwatia nguvuni waliotajwa kwenye ripoti ya CAG🌚🌚

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

=====

Sakata la kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Siglada Mligo, aliyepigwa na kujeruhiwa na Mlinzi katika kikao cha Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Taifa John Heche mkoani Njombe, limevuta hisia za Chama cha Mapinduzi (CCM) baada ya kada huyo kukosa msaada wa haraka.

Pia soma: Pre GE2025 - CCM yamchangia fedha za matibabu BAWACHA Seglada aliyepigwa na mlinzi

Katibu wa NEC, Itikadi na Mafunzo wa CCM Taifa, Amosi Makala baada ya kuchangisha fedha kwaajili ya matibabu lakini ameenda mbali zaidi kuwaagiza uongozi wa chama hicho mkoa wa Iringa kushughulikia safari ya Mligo kwenda Dodoma kwa ajili ya matibabu zaidi baada ya hali yake kubadilika.
Kwani aliyesema apelekwe huko,yeye ni daktari wa nini?
 
Back
Top Bottom