Baada ya kusoma vitabu zaidi ya 300, nimegundua kumbe nilitakiwa kusoma Biblia tu

Bible na Quran ni vitabu vizuri

Ila kuhusu kuwa na kila kitu sio kweli maana maisha yanahitaji uelewa mpana wa mambo ili kufanikiwa vizuri
 
Tafsiri ya Mungu wa kweli kwako ni ipi au nini maana ya Mungu wa kweli?
Ambaye kuna uthibitisho juu ya uwepo wake.

Tukitumia mapokeo binafsi kila mtu atasema Mungu wake ni wa kweli. Waislam watasema Allah, wakristo Yahweh, wahindu watasema kina Brahma nk, nk...
 
Maisha ya Mwanamarundi yanapatikana kwenye Biblia ? Au hapa unamaanisha Biblia gani ? Technically unaweza kusema kila nyanja ina Bible yake; mfano the Bible of Chemistry; Kama-Sutra n.k.

He is not deceived who knows himself to be deceived....

By the way premise yako ni illogical sababu kuna hizi Bible zina editions (sasa kama the thing itself haijotoshelezi mpaka iwe revised na kuongezewa kutokana na muda huoni kwamba the previous lacks what the latter has)?
 
kuna kitu nhaipo sawa na mental model unayotumia kufikiri
 
Kweli akili ni nywele na kila Mtu ana zake, kwahiyo Buddhism Religion inayokuhadaa kuwa "ukishafariki unageuka kuwa mende, funza, fisi au viumbe hai mbali mbali tofauti na kabla hujafariki na kurudi kuishi upya duniani" ndiyo umeiona ya maana na kuiaminia?

Basi nawe usipangie Binadamu wenzio watachopendezwa kukiamini na jifunze kupokea imani na mitazamo tofauti sawa na wewe ulivyoamini dini tofauti na Watu wengine.
 
Ambaye kuna uthibitisho juu ya uwepo wake.

Tukitumia mapokeo binafsi kila mtu atasema Mungu wake ni wa kweli. Waislam watasema Allah, wakristo Yahweh, wahindu watasema kina Brahma nk, nk...
Sasa mfano mmoja anakwambia huyu mbuzi ndio mungu wangu na akakuonyesha na mwengine akakwamnia ule mlima ndio mungu na akakuonyesha, je hapo watakuwa wote wamethibitisha miungu yao au watakuwa bado hawajathibitisha?
 
kunionesha haitoshi kuthibisha, huyo mungu anapaswa ajidhihirishe, ajiweke wazi.

Kwa muktadha huu hakuna mungu wa kweli, utamuabudu yule uliyemkuta kwa wazazi

hakuna mungu aliyejidhihirisha mpaka sasa
 
Brother biblia ina fundisha ujasusi wa uchumi?
Ndiyo inafundisha, kuna mahali Mfalme Daudi aliagiza wana wa Israel waende Taifa flani kuchunguza nyenzo za uchumi wanavyojenga na wanavyomudu kujitegemea kiuchumi bila kuhusisha Mataifa mengine kimaendeleo ya uchumi kwa kutoomba misaada wala namna ya uendeshaji uchumi katika nchi hiyo.
 
kunionesha haitoshi kuthibisha, huyo mungu anapaswa ajidhihirishe, ajiweke wazi.

Kwa muktadha huu hakuna mungu wa kweli, utamuabudu yule uliyemkuta kwa wazazi

hakuna mungu aliyejidhihirisha mpaka sasa
Wewe unataka uthibitisho wa uwepo wa Mungu au unataka Mungu ajidhihirishe? Maana hivyo ni vitu viwili tofauti.
 
Wewe unataka uthibitisho wa uwepo wa Mungu au unataka Mungu ajidhihirishe? Maana hivyo ni vitu viwili tofauti.
Kwa ninavyoelewa akijidhihirisha atakua amethibitisha uwepo wake, 'kudhihirisha' si kuweka wazi, kuondoa shaka...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…