Baada ya kusoma vitabu zaidi ya 300, nimegundua kumbe nilitakiwa kusoma Biblia tu

Baada ya kusoma vitabu zaidi ya 300, nimegundua kumbe nilitakiwa kusoma Biblia tu

Bible na Quran ni vitabu vizuri

Ila kuhusu kuwa na kila kitu sio kweli maana maisha yanahitaji uelewa mpana wa mambo ili kufanikiwa vizuri
 
Tafsiri ya Mungu wa kweli kwako ni ipi au nini maana ya Mungu wa kweli?
Ambaye kuna uthibitisho juu ya uwepo wake.

Tukitumia mapokeo binafsi kila mtu atasema Mungu wake ni wa kweli. Waislam watasema Allah, wakristo Yahweh, wahindu watasema kina Brahma nk, nk...
 
Maisha ya Mwanamarundi yanapatikana kwenye Biblia ? Au hapa unamaanisha Biblia gani ? Technically unaweza kusema kila nyanja ina Bible yake; mfano the Bible of Chemistry; Kama-Sutra n.k.

He is not deceived who knows himself to be deceived....

By the way premise yako ni illogical sababu kuna hizi Bible zina editions (sasa kama the thing itself haijotoshelezi mpaka iwe revised na kuongezewa kutokana na muda huoni kwamba the previous lacks what the latter has)?
 
Kwa miaka kadhaa nimesoma vitabu vya uchumi, biashara, mahusiano, saikolojia na namna ya kukabiliana na changamoto za maisha.

Nimesoma vitabu vya wakina Kiyosaki, Brian Trecy, Robert Green, Ralph Waldo Emerson, Tsu Nzu, Napoleon Hill, Donald Trump, Shoga Yuval Noah Harari n.k

Hii ndio hitimisho langu, karibu kila idea ya maana niliyojifunza imeelezewa kwenye Biblia moja kwa moja au kwa kuidecode.

Hivyo mtu ambaye atasoma biblia pekee kitaalam hana sababu ya kuhangaika kusoma vitabu vingine viingi. Ila pia kama unapenda kusomasoma, ukianzia kusoma biblia ukaenda kwenye vitabu vingine utaevielewa kwa haraka sana na utasoma kwa wepesi sana.

Ni hayo tu.
kuna kitu nhaipo sawa na mental model unayotumia kufikiri
 
Bible ni muhimu kuisoma kama Shakespeare na vitabu vingine ambavyo vimesomwa na watu wengi.

Sababu ni cultural intelligence. Hutakiwi kuwa katika mazungumzo halafu mtu anatoa Biblical reference halafu huijui.

Yani usiwe mjinga kiutamaduni kiasi kwamba mtu akikwambia "vita ya leo ni kama ya Daudi na Goliati , nashindana na nguvu kubwa sana, lakini mimi nitashinda kama Daudi", halafu wewe ukawa hujui story ya Daudi na Goliati ilikuwaje na huyu mtu ana maana gani hapa.

Hapo utakuwa na lack of cultural intelligence.

Lakini, kuna mambo mengi sana tumeendelea kielimu baada ya Bible kuandikwa, na kuna makosa mengi sana kwenye Bible tumeyaelewa, kuanzia ethics, logic, science, history etc. Nimeweka makosa na mikanganyiko ndani ya Biblia hapo juu.

Kwa hivyo, Biblia ina makosa kibao pia, si kitabu fulani ambacho ni kitakatifu hivyoo, kina makosa na hakina busara zote .

Ukisoma vitabu vya dini na falsafa za mashariki, kama Vedas, Dhammapada, Tripitaka etc, unaweza kukuta vina busara pengine kupita Bible, ingawa navyo vina mapungufu yake.

Nimesoma vitabu vya Buddhism especially nimeona vina busara sana ya kusisitiza amani na kutotaka vita, ukisoma historia ya Mfalme Asoka na jinsi alivyoacha vita, akafuata Buddhism, it is rather impressive.

Kwenye Biblia unakutana na Mungu anachochea vita, ana taifa lake analolipendelea, unaona kabisa huyu Mungu kaandikwa na watu wa hili taifa huyu.

Tatizo nani kasoma vitabu kama Dhammapada na Tripitaka set hapa?

Yani unakuta watu wengi wanazunguka kwenye Biblia na Quran tu, hata hawajafungua kwingine huko.

Kwa hivyo hata kwenye vitabu vya imani, upeo wao finyu.

The Buddhist books such as Dahammapada/ Tripitaka are far more philosophical and compassionate than the Bible.
Kweli akili ni nywele na kila Mtu ana zake, kwahiyo Buddhism Religion inayokuhadaa kuwa "ukishafariki unageuka kuwa mende, funza, fisi au viumbe hai mbali mbali tofauti na kabla hujafariki na kurudi kuishi upya duniani" ndiyo umeiona ya maana na kuiaminia?

Basi nawe usipangie Binadamu wenzio watachopendezwa kukiamini na jifunze kupokea imani na mitazamo tofauti sawa na wewe ulivyoamini dini tofauti na Watu wengine.
 
Ambaye kuna uthibitisho juu ya uwepo wake.

Tukitumia mapokeo binafsi kila mtu atasema Mungu wake ni wa kweli. Waislam watasema Allah, wakristo Yahweh, wahindu watasema kina Brahma nk, nk...
Sasa mfano mmoja anakwambia huyu mbuzi ndio mungu wangu na akakuonyesha na mwengine akakwamnia ule mlima ndio mungu na akakuonyesha, je hapo watakuwa wote wamethibitisha miungu yao au watakuwa bado hawajathibitisha?
 
Sasa mfano mmoja anakwambia huyu mbuzi ndio mungu wangu na akakuonyesha na mwengine akakwamnia ule mlima ndio mungu na akakuonyesha, je hapo watakuwa wote wamethibitisha miungu yao au watakuwa bado hawajathibitisha?
kunionesha haitoshi kuthibisha, huyo mungu anapaswa ajidhihirishe, ajiweke wazi.

Kwa muktadha huu hakuna mungu wa kweli, utamuabudu yule uliyemkuta kwa wazazi

hakuna mungu aliyejidhihirisha mpaka sasa
 
Brother biblia ina fundisha ujasusi wa uchumi?
Ndiyo inafundisha, kuna mahali Mfalme Daudi aliagiza wana wa Israel waende Taifa flani kuchunguza nyenzo za uchumi wanavyojenga na wanavyomudu kujitegemea kiuchumi bila kuhusisha Mataifa mengine kimaendeleo ya uchumi kwa kutoomba misaada wala namna ya uendeshaji uchumi katika nchi hiyo.
 
kunionesha haitoshi kuthibisha, huyo mungu anapaswa ajidhihirishe, ajiweke wazi.

Kwa muktadha huu hakuna mungu wa kweli, utamuabudu yule uliyemkuta kwa wazazi

hakuna mungu aliyejidhihirisha mpaka sasa
Wewe unataka uthibitisho wa uwepo wa Mungu au unataka Mungu ajidhihirishe? Maana hivyo ni vitu viwili tofauti.
 
Back
Top Bottom