Baada ya kustaafu katelekezwa na mke na watoto wake. Anaugua ugonjwa wa akili kwa sasa

Hiyo siyo kataa ndoa tu, tusizae knisa, sababu huyo mzee shahawa zake mwenyewe zimemdhuru... Watoto wamemtenda dingi, watoto tunawapata kwenye ndoa ama bila ya ndoa.

iwe ni kampeni ya
KATAA KUKOJOLEA NDANI.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Hiyo siyo kataa ndoa tu, tusizae knisa, sababu huyo mzee shahawa zake mwenyewe zimemdhuru... Watoto wamemtenda dingi, watoto tunawapata kwenye ndoa ama bila ya ndoa.

iwe ni kampeni ya
KATAA KUKOJOLEA NDANI.
Mwendo wa kukojoa nje sio
 
Jamani mimi niwape ushuhuda kidogo,si kwamba naunga mkono watu wasioe,hapana
bali ukioa usijisahau.Kama unafanya kazi,jitahidi weka akiba na kuiheshimu pensheni,
Nimejifunza kwangu mimi mwenyewe,hivyo sishangai kwa yaliyompata huyo mzee.

Mimi kufuatana na shughuli zangu kuwa mbali,nilikuwa nikipata kipato
namkabidhi mke wangu pesa ya matumizi ili kutunza familia,hata karo za watoto naendelea na mishe ya kusaka pesa. Nilifikia hatua ya kuacha na kadi ya benki ili kuondoa usumbufu,
Akilini nikijua mambo yote yako poa.Kumbe haikuwa hivyo
Nadhani kuna shetani alipitia. Karo zikawa halipwi ila muda ukifika anakopa anawapa watoto wanaenda shule.
Tena mikopo ya liba hivyo inaendelea kuzaa deni linaongezeka mimi sina habari.

Baada ya madeni kuwa makubwa,mtu mmoja rafiki yangu ambaye alisikia habari hizo
akanifuata,na kunishauri kuwa pamoja na mishe zangu za kusafiri nijitahidi kumsaidia
mke wangu kulipa ada za watoto anapata sana shida kutafuta pesa.
Niliposikia hivyo nilistuka nadhani naye alijua.lkn nikamwambia sawa nitajitahidi,maana niliona nikionyesha kukerwa
naye atashangaa sana kwa jinsi alivyotujua tunavyoishi na mke wangu.

Nilipoenda kumwuliza akakana,akasema humna kitu kama hicho.hivyo nikaanza utafiti binafsi
Niliyoyakuta ilikuwa story ndefu.Namshukuru Mungu tulifanikiwa kuyamaliza,na nilifanikiwa kulipa hayo madeni,
kuanzia hapo nikaanza kulipa karo kwa mkono wangu mwenyewe
na kufuata ushauri wa mchungaji mgogo kwamba unapotoa matumizi,hakikisha unatoa sebureni siyo chumbani
ili watoto waone jitihada zako za uwajibikaji.

Baada ya kubadilisha mfumo wa maisha tunaendelea vizuri na maisha.
Hivyo vijana msiogope kuoa,kama unamcha Mungu hakuna ubaya utakaofanyika chini ya kapeti usijue.

Tunaolaumu kwamba wanaume hawawajibiki japo sikatai lakini tujitafakari.Hata kama hawawajibiki ni kwa nini tunasubiri wazeeke ndo tuwanyanyase? kwanini msiwakimbie mapema mkaolewe au mkaanzishe maisha nje ya hao wanaowanyanuyasa?

Mi nadhani vijana chukueni ushauri huu,wazazi wako ni wazazi wako.Asiwepo hata mmoja wa kukuambia ubaya wa mwenzake maana walipokutana hukuwepo na wewe
usijifanye bingwa wa kulipa kisasi itakughalimu.Baba asingempa mimba mama yako,usingezaliwa.
Na baba bila mama mimba yako isingetungwa na usingekuja duniani.
Hata kama hukutunzwa. Watunze wazazi wako kwa kadri ya uwezo ulio nao
maana wamekuleta duniani.
Na Mungu atakubariki.
Sign of maturity. Mkuu unaonekana kuwa na busara sana. Yaani wewe una uwezo wa kum console mtu aliyefika terminal kwa mawazo na akarudi upya. Hongera sana mkuu
 
Na watoto wake aliwasomesha English Medium.

Alipoteza hela zake bure masikini
 
Nashindwa sometimes kuelewa nini faida na umuhimu wa ndoa kama mambo yenyewe huwaga hivi.

Kuna mzee mmoja alikua jirani yangu, alikua mhandisi wa shirika moja kubwa hapa nchini

Mzee huyu kutoka kule migombani alioa mke wa migombani pia. Maisha yalikua mazuri wakati mzee bado anafanya kazi.

Alijenga nyumba mikoa mbalimbali na alijitahidi kuwasomesha watoto wake shule nzuri hizi za saint saint.

Watoto wake wote wana shughuli zao nzuri tu.

Baada ya kustaafu hapo ndo akaanza kuona rangi halisi ya mke wake. Kwanza alimtumia wakora wamfanye kitu mbaya ili mke arithi mali mapema bahati nzuri ndugu wa mume wakashtukia mapema mission ikabuma.

Tangu wakati huo mke akaanza kumtenga mume wake na kibaya zaidi hadi watoto wake aliowasomesha wakamtenga baba yao na kumsahau kabisa(sijui mama yao aliwaambia nini)

Dingi akaanza kunyimwa chakula, dingi akakimbiwa chumba na mke wake(alikua anatuambia vijana na kutuhasa juu ya makabila ya kuoa)

Baada ya muda mzee kaanza kurukwa na akili kwa maisha aliyokua anaishi.

Kwa sasa mzee karudi kwao lakini akili yake haiko sawa kaacha mali zote anaishi kijijini kwao. Watoto wake wamemtupa hawana time na baba yao

Je nini hasa wamama wanawaambia watoto wao kiasi cha watoto kuanza kumchukia baba yao na kumtenga ili hali aliwasomesha na kuwalea vizuri na juhudi zake waliziona.?

Hili ni janga kwenye familia nyingi baba akistaafu anaishi maisha magumu ya kunyanyasika juhudi zake zote alizofanya kujenga familia bora zinakua kazi bure anaishia kutengwa na kupata msongo wa mawazo na mwisho kufa.

KATAA NDOA NI UUAJI NA UTAPELI
Inatisha na kusikitisha!
Mwanamke katika ubora wake hapo!
 
Mwanaume hakikisha unajiandalia plan b ya maisha ya uzeeni nje ya familia
 
Yule mzee na familia yake nimeishi nao jirani sana mzee alikua mtu poa na watoto wake walisoma shule nzuri sana ila ndo hivyo wamemtelekeza. Kuna wakati alikua anahudumiwa na binti yake kama kumpikia na kumchotea maji mke wake alisepa sijui alienda kudanga wapi.
Wakati mwingine angalia maisha Yako wakati ukiwa na nguvu ulikuwa unaishi vipi na huyo mwanamke, kama ulikuwa unamtesa na watoto wanajua uzeeni utapata shida sana. Mtunze mkeo na watoto wajifunze kwenu jinsi mnavyopendana hata uzeeni hawatakutenga baba yao
 
Ukioa Mtunze mkeo na usimnyanyase, ukimnyanyasa mkeo watoto watakuwa upande wa mama. Hivyo uzeeni watakuwa hawana muda na wewe. Pia kama huyo Mzee alikuwa anafanya kazi Tena mashirika makubwa SI analipwa pension Kila mwezi hawezi kushindwa kuishi . Pia ana uwezo wakuajili MTU wa kumtunza
 
Yule mzee na familia yake nimeishi nao jirani sana mzee alikua mtu poa na watoto wake walisoma shule nzuri sana ila ndo hivyo wamemtelekeza. Kuna wakati alikua anahudumiwa na binti yake kama kumpikia na kumchotea maji mke wake alisepa sijui alienda kudanga wapi.
Kuna jambo baya alilifanya mzee si bure au hao watoto sio wake kibaiyolojia
 
Nashindwa sometimes kuelewa nini faida na umuhimu wa ndoa kama mambo yenyewe huwaga hivi.

Kuna mzee mmoja alikua jirani yangu, alikua mhandisi wa shirika moja kubwa hapa nchini

Mzee huyu kutoka kule migombani alioa mke wa migombani pia. Maisha yalikua mazuri wakati mzee bado anafanya kazi.

Alijenga nyumba mikoa mbalimbali na alijitahidi kuwasomesha watoto wake shule nzuri hizi za saint saint.

Watoto wake wote wana shughuli zao nzuri tu.

Baada ya kustaafu hapo ndo akaanza kuona rangi halisi ya mke wake. Kwanza alimtumia wakora wamfanye kitu mbaya ili mke arithi mali mapema bahati nzuri ndugu wa mume wakashtukia mapema mission ikabuma.

Tangu wakati huo mke akaanza kumtenga mume wake na kibaya zaidi hadi watoto wake aliowasomesha wakamtenga baba yao na kumsahau kabisa(sijui mama yao aliwaambia nini)

Dingi akaanza kunyimwa chakula, dingi akakimbiwa chumba na mke wake(alikua anatuambia vijana na kutuhasa juu ya makabila ya kuoa)

Baada ya muda mzee kaanza kurukwa na akili kwa maisha aliyokua anaishi.

Kwa sasa mzee karudi kwao lakini akili yake haiko sawa kaacha mali zote anaishi kijijini kwao. Watoto wake wamemtupa hawana time na baba yao

Je nini hasa wamama wanawaambia watoto wao kiasi cha watoto kuanza kumchukia baba yao na kumtenga ili hali aliwasomesha na kuwalea vizuri na juhudi zake waliziona.?

Hili ni janga kwenye familia nyingi baba akistaafu anaishi maisha magumu ya kunyanyasika juhudi zake zote alizofanya kujenga familia bora zinakua kazi bure anaishia kutengwa na kupata msongo wa mawazo na mwisho kufa.

KATAA NDOA NI UUAJI NA UTAPELI
Ndoa haikataliwi Bali jua Kuna kuachwa na mke/Mme, au watoto, ndugu na marafiki Cha muhimu baba ataendelea kuwa baba hata akiwa na miaka mia hivyo, usipoteze kipato yaani umeweka vitega uchumi hakikisha hiviachii mpaka kifo na kama Kuna anayekuunga mkono huyo Kaa naye karibu haijalishi ni mtoto ndugu au mtu Baki, usipoteze uwezo wa kifedha
 
Ukioa Mtunze mkeo na usimnyanyase, ukimnyanyasa mkeo watoto watakuwa upande wa mama. Hivyo uzeeni watakuwa hawana muda na wewe. Pia kama huyo Mzee alikuwa anafanya kazi Tena mashirika makubwa SI analipwa pension Kila mwezi hawezi kushindwa kuishi . Pia ana uwezo wakuajili MTU wa kumtunza
Wengine fanya ufanyavyo wanakusubiria uchoke ndo uone majanga, na kutomnyanyasa mke watoto na ndugu ni wajibu, linguine oa mke mwenye kufanya ibada na maadili mema pia fundisha watoto ibada na maadili mema
 
Nashindwa sometimes kuelewa nini faida na umuhimu wa ndoa kama mambo yenyewe huwaga hivi.

Kuna mzee mmoja alikua jirani yangu, alikua mhandisi wa shirika moja kubwa hapa nchini

Mzee huyu kutoka kule migombani alioa mke wa migombani pia. Maisha yalikua mazuri wakati mzee bado anafanya kazi.

Alijenga nyumba mikoa mbalimbali na alijitahidi kuwasomesha watoto wake shule nzuri hizi za saint saint.

Watoto wake wote wana shughuli zao nzuri tu.

Baada ya kustaafu hapo ndo akaanza kuona rangi halisi ya mke wake. Kwanza alimtumia wakora wamfanye kitu mbaya ili mke arithi mali mapema bahati nzuri ndugu wa mume wakashtukia mapema mission ikabuma.

Tangu wakati huo mke akaanza kumtenga mume wake na kibaya zaidi hadi watoto wake aliowasomesha wakamtenga baba yao na kumsahau kabisa(sijui mama yao aliwaambia nini)

Dingi akaanza kunyimwa chakula, dingi akakimbiwa chumba na mke wake(alikua anatuambia vijana na kutuhasa juu ya makabila ya kuoa)

Baada ya muda mzee kaanza kurukwa na akili kwa maisha aliyokua anaishi.

Kwa sasa mzee karudi kwao lakini akili yake haiko sawa kaacha mali zote anaishi kijijini kwao. Watoto wake wamemtupa hawana time na baba yao

Je nini hasa wamama wanawaambia watoto wao kiasi cha watoto kuanza kumchukia baba yao na kumtenga ili hali aliwasomesha na kuwalea vizuri na juhudi zake waliziona.?

Hili ni janga kwenye familia nyingi baba akistaafu anaishi maisha magumu ya kunyanyasika juhudi zake zote alizofanya kujenga familia bora zinakua kazi bure anaishia kutengwa na kupata msongo wa mawazo na mwisho kufa.

KATAA NDOA NI UUAJI NA UTAPELI
Nawaasa vijana. Ukioa unakuwa mtawala mpaka miaka 55. Baada ya kufikisha umri huo mama anachukua mamlaka. Kumbuka alikuwa msaidizi wako, akishachukua mamlaka utawala wake utategemea ulivyokuwa mamlakan uliishije nae. Kama alikuwa very close na rafiki utaishi kama mfalme kama ulikuwa unawapitisha rafu road ujue ndio zamu yake. Kumbuka daima maisha yanakupa kile ulichoipa. Mama akishachukua mamlaka nae utawala wake mwisho ni miaka 75. Baada ya hapo watoto wanachukua mamlaka nao itategemea ulivyowalea. Ndio pale Biblia inakuambia ulipokuwa kijana ulikuwa unaenda utakapo ila ukiwa mzee watakupeleka usipopataka na huwez kuzuia. Kingine usidhulumu usiwe mchawi au kuiba maana utalipia gharama no matter what. Wewe au wanao.
 
Kuna mzee jirani yangu alikuwa anafanya lazi katika sekta ya ulinzi huko. Alipo staafu akawehuka na mafao. Akamtelekeza mke na watoto .Akawa anajishughulisha na Viruka njia . Pesa hazikudumu zikamwishia. Akarudi kwa mkewe tena akiwa mkali balaaa.Mke alichoamua akamwachia mjengo .akaenda kupanga uswahilini. Hivi sasa Mzee anateseka vibaya hana msaada hata jirani.
WANAUME TUKUMBUKE FAINAL UZEENI
 
Back
Top Bottom