Jamani mimi niwape ushuhuda kidogo,si kwamba naunga mkono watu wasioe,hapana
bali ukioa usijisahau.Kama unafanya kazi,jitahidi weka akiba na kuiheshimu pensheni,
Nimejifunza kwangu mimi mwenyewe,hivyo sishangai kwa yaliyompata huyo mzee.
Mimi kufuatana na shughuli zangu kuwa mbali,nilikuwa nikipata kipato
namkabidhi mke wangu pesa ya matumizi ili kutunza familia,hata karo za watoto naendelea na mishe ya kusaka pesa. Nilifikia hatua ya kuacha na kadi ya benki ili kuondoa usumbufu,
Akilini nikijua mambo yote yako poa.Kumbe haikuwa hivyo
Nadhani kuna shetani alipitia. Karo zikawa halipwi ila muda ukifika anakopa anawapa watoto wanaenda shule.
Tena mikopo ya liba hivyo inaendelea kuzaa deni linaongezeka mimi sina habari.
Baada ya madeni kuwa makubwa,mtu mmoja rafiki yangu ambaye alisikia habari hizo
akanifuata,na kunishauri kuwa pamoja na mishe zangu za kusafiri nijitahidi kumsaidia
mke wangu kulipa ada za watoto anapata sana shida kutafuta pesa.
Niliposikia hivyo nilistuka nadhani naye alijua.lkn nikamwambia sawa nitajitahidi,maana niliona nikionyesha kukerwa
naye atashangaa sana kwa jinsi alivyotujua tunavyoishi na mke wangu.
Nilipoenda kumwuliza akakana,akasema humna kitu kama hicho.hivyo nikaanza utafiti binafsi
Niliyoyakuta ilikuwa story ndefu.Namshukuru Mungu tulifanikiwa kuyamaliza,na nilifanikiwa kulipa hayo madeni,
kuanzia hapo nikaanza kulipa karo kwa mkono wangu mwenyewe
na kufuata ushauri wa mchungaji mgogo kwamba unapotoa matumizi,hakikisha unatoa sebureni siyo chumbani
ili watoto waone jitihada zako za uwajibikaji.
Baada ya kubadilisha mfumo wa maisha tunaendelea vizuri na maisha.
Hivyo vijana msiogope kuoa,kama unamcha Mungu hakuna ubaya utakaofanyika chini ya kapeti usijue.
Tunaolaumu kwamba wanaume hawawajibiki japo sikatai lakini tujitafakari.Hata kama hawawajibiki ni kwa nini tunasubiri wazeeke ndo tuwanyanyase? kwanini msiwakimbie mapema mkaolewe au mkaanzishe maisha nje ya hao wanaowanyanuyasa?
Mi nadhani vijana chukueni ushauri huu,wazazi wako ni wazazi wako.Asiwepo hata mmoja wa kukuambia ubaya wa mwenzake maana walipokutana hukuwepo na wewe
usijifanye bingwa wa kulipa kisasi itakughalimu.Baba asingempa mimba mama yako,usingezaliwa.
Na baba bila mama mimba yako isingetungwa na usingekuja duniani.
Hata kama hukutunzwa. Watunze wazazi wako kwa kadri ya uwezo ulio nao
maana wamekuleta duniani.
Na Mungu atakubariki.