Baada ya kutoa mabandiko kuhusu hali ya Corona nchini, Kaimu Balozi wa Marekani aitwa Serikali kutoa ufafanuzi

Baada ya kutoa mabandiko kuhusu hali ya Corona nchini, Kaimu Balozi wa Marekani aitwa Serikali kutoa ufafanuzi

Hawajamuweka ndani? Wamuweke ndani mara moja kwa kosa la kuchapisha maudhui potofu. BTW wanafikiri Marekani wanakaa kizembe zembe na hawana details za kila kitu kinachoendelea Tanzania? Ni nini kazi ya CIA? Wanajua mpaka idadi ya vifo halisi vya korona japo walizika usiku kwa kujificha.
CIA waliosema rais wa korea kaskazini amekufa [emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unajua kwamba kwao marekani walificha taarifa pia...
Na baadae ikageuka Trump akalalamika kuwa namba zinaongezwa za uwongo ili kumuharibia kwenye uchaguzi.
Usiamini kwa muzungu ni kwa malaika mkuu.
Kila nchi imekuwa na matatizo ya data.
Hawa wakinyamazia uongo unaoenezwa na kundi hili lenye madaraka watakuwa wanashiriki uhalifu.

Wanachotakiwa kukifanya kwa sasa ni kufichua uongo wote, kwa sababu uwezo wa kufanya hivyo wanao.

Watakuwa wanawasaidia waTanzania waliowekwa mateka kwa kufichua maovu yote wanayofanyiwa.

Tunataka watalii waje, halafu tunaficha taarifa mhimu za ugonjwa. Hizo serikali wanakotoka hao watalii watakuwa hawana akili timamu kutowaeleza raia zao hali halisi ya hatari iliyopo huko wanakotaka kwenda kutalii.

Ni wajibu wa serikali zao kufanya kazi hiyo.
 
Mkuu peleka hizo ulizo nazo, sjui unangoja nini kupeleka hizo Tarifa Maana ndg zako ukiwemo na wewe mna Corona wote!!
 
Naona s
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imemwita Kaimu Balozi wa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania Dkt. Imni Patterson ili kutoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali ambayo Ubalozi huo umekuwa ukiyaandika katika mitandao yake ya kijamii bila ya uthibitisho.

Kaimu Balozi huyo amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, kwenye Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.

Katika mazungumzo hayo, Katibu Mkuu ameeleza masikitiko yake kutokana na namna ambavyo Ubalozi huo umekuwa ukitoa taarifa mbalimbali za ushauri wa kiusafiri (travel advisory) zinazoandikwa na kusambazwa na Ubalozi wa Marekani kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo suala la namna Tanzania inavyoshughulikia ugonjwa wa COVID-19.

Ubalozi wa Marekani wasisitiza maambukizi ya Corona jijini Dar yameshika kasi. Wadai Hospitali zimeelemewa! - JamiiForums

Sasa naona wanataka kumshika simba sharubu zake. Tusubiri matokeo.
 
Mabeberu this time wanahaha
Makaburu hawaamini kuwa tuna uwezo wa kusimamia maamuzi yetu wenyewe! Marekani amekuwa akiburuza hata wazungu wa ulaya. Kwanza walitazamia kuwa tutakufa Sana na korona, haijatokea!! Wao kwa takriban miezi miwili mfululizo walikuwa wanazika watu zaidi ya 2,000 kwa siku!! Wanashangaa siri yetu ni nini? Hawajaamini!! Lakini watalazika kuamini tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawajamuweka ndani? Wamuweke ndani mara moja kwa kosa la kuchapisha maudhui potofu. BTW wanafikiri Marekani wanakaa kizembe zembe na hawana details za kila kitu kinachoendelea Tanzania? Ni nini kazi ya CIA? Wanajua mpaka idadi ya vifo halisi vya korona japo walizika usiku kwa kujificha.
Sidhani kama wewe una asili ya Tanzania au hata kama ni mtanzania

Basi huna uzalendo
 
USA imewaambia raia zake...Si ninyi serikali mnaficha data....Mtakula hizo data sasa. Mtapata watalii chini ya laki moja kwa mwaka. Serikali ya Magufuli ya ovyo, ovyo kweli imejaa washamba, malimbukeni na wauaji. Mtalipa hayo yote mnayoyafanya.
Una utoto Sana
 
Kuna Vienna Convention hapo, kinachoweza kutokea ni kurudishwa USA tu, lakini sasa hivi hakuna hiyo haja kwa sababu USA wana uchaguzi October hivyo anaweza kabisa kubadilishwa mwisho wa mwaka. Hapo anaelezwa ukweli tu, aache longo longo Tanzania ni nchi sio pandikizi la USA.

Toeni data za COVID19 , dunia nzima inafanya hivyo kwa nini sisi???
 
Uzuri mmoja baada ya hayo mahojiano ataandika tena bandiko lingine tena kwa lugha ya kibeberu
Jf noma mtu amecopy comment hapa anaenda kupaste kama comment yake huko twitter 🤣 acheni plagiarism wahusika
20200526_200519.png
 
Hawajamuweka ndani? Wamuweke ndani mara moja kwa kosa la kuchapisha maudhui potofu. BTW wanafikiri Marekani wanakaa kizembe zembe na hawana details za kila kitu kinachoendelea Tanzania? Ni nini kazi ya CIA? Wanajua mpaka idadi ya vifo halisi vya korona japo walizika usiku kwa kujificha.
Lakini kwao wameshindwa kujua kwamba chloroquine ni dawa au sio dawa ya korona
 
Pale walipodai kuwa Hospitali zimeelmewa, mimi nataka kuwauliza tu, Hizi hospitali zipo vichochoroni wanazijua wao tu ubalozi?
 
Back
Top Bottom