Baada ya kutoa mabandiko kuhusu hali ya Corona nchini, Kaimu Balozi wa Marekani aitwa Serikali kutoa ufafanuzi

Baada ya kutoa mabandiko kuhusu hali ya Corona nchini, Kaimu Balozi wa Marekani aitwa Serikali kutoa ufafanuzi

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imemwita Kaimu Balozi wa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania Dkt. Imni Patterson ili kutoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali ambayo Ubalozi huo umekuwa ukiyaandika katika mitandao yake ya kijamii bila ya uthibitisho.

Kaimu Balozi huyo amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, kwenye Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.

Katika mazungumzo hayo, Katibu Mkuu ameeleza masikitiko yake kutokana na namna ambavyo Ubalozi huo umekuwa ukitoa taarifa mbalimbali za ushauri wa kiusafiri (travel advisory) zinazoandikwa na kusambazwa na Ubalozi wa Marekani kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo suala la namna Tanzania inavyoshughulikia ugonjwa wa COVID-19.

Ubalozi wa Marekani wasisitiza maambukizi ya Corona jijini Dar yameshika kasi. Wadai Hospitali zimeelemewa! - JamiiForums

Nimemuona kupitia TV (ITV) akiwa kwa Katibu mkuu wizara ya mambo ya nje...tehtehtehteh
 
Pole pole anasema wameiuliza corona itatoka haitoki? [emoji38][emoji16][emoji23]
Mtu mwenyewe hajaangaika na mitanzania yeye ameamua kuwa alert watu wa nchi yake ambapo kimsingi ni jukumu lake la kwanza. Hapa serikali imefanya utopolo mtupu. Mimi namuunga mkono balozi maana kwa hilo tangazo lake na mimi naponea humo humo kwa kuendelea kuchukua tahadhari. Acha wanaoficha maradhi waendelee hivyo hivyo.

Mnaomba misaada ya kupambana na Corona huku mnasema mumeifuta! [emoji112][emoji112][emoji112][emoji112][emoji112][emoji112]
 
Sisi tutaishia kutoa “masikitiko yetu” tu na ubalozi wataendelea kutoa travel advisory kwa raia wao ambazo kama Nchi hatuna mamlaka ya kuwazuia. Ukitaka kuepusha speculations, weka data hadharani
Sasa sijui wanaficha kitu gani
 
Hii serikali imekaa kishamba sana.
Diplomasia iko sifuri kabisa.
Bado sijajua serikali ilikuwa inatuma ujumbe gani kwa kutueleza kuwa imeita na kumuhoji huyo balozi?
What is next?

Kama lengo ni kumuita na kumhoji ili kujua kwanini balozi huyo amekuwa akitoa hizo taarifa, basi busara ya kidiplomasia huwa ni kulifanya siri hilo jambo, then baada ya ya kuongea naye, matokeo ndio tutayaona.
 
Nyie endeleen na porojo Ila nchi sasaiv inaongoza Kama nchi zingine zilizo endelea lazima ahojiwe ubalozi unapo kua kwenye nchi za watu hutakiw kuropoka unavyo jiskia unatakiwa ujue mipaka yako hongera Tanzania kwa kuendelea kusimama Kama nchi
Hawajamuweka ndani? Wamuweke ndani mara moja kwa kosa la kuchapisha maudhui potofu. BTW wanafikiri Marekani wanakaa kizembe zembe na hawana details za kila kitu kinachoendelea Tanzania? Ni nini kazi ya CIA? Wanajua mpaka idadi ya vifo halisi vya korona japo walizika usiku kwa kujificha.
 
Hawajamuweka ndani? Wamuweke ndani mara moja kwa kosa la kuchapisha maudhui potofu. BTW wanafikiri Marekani wanakaa kizembe zembe na hawana details za kila kitu kinachoendelea Tanzania? Ni nini kazi ya CIA? Wanajua mpaka idadi ya vifo halisi vya korona japo walizika usiku kwa kujificha.
Hizo maiti zinazozikwa usiku hazina ndugu, majirani au rafiki? Au wewe una ndugu, jirani au rafiki aliyezikwa usiku. Subiri na wewe uzikwe usiku.

Unajiaibisha
 
Back
Top Bottom