Baada ya Kutoka mkutanoni Dar es salaam Kagame atoa Tamko na kusema " Hakuna wa Kutupangia"

Baada ya Kutoka mkutanoni Dar es salaam Kagame atoa Tamko na kusema " Hakuna wa Kutupangia"

Baada ya Mkutano wa usuluhishi kukamilika Dar es salaam Rais Kagame wa Rwanda amesema " hakuna wa Kutupangia" linapokuja swala la ulinzi na ustawi wa Rwanda

Watoto wa Kagame Wote ni Wanajeshi

Credit: Citizen TV
Sa 100kajidai Ku host upatanishi ona sasa namna anaonekana Hana maana zaidi ya kupoteza muda bure . Mambo ya nchi yanamshinda, Yale ya Rwanda atayaweza?
 
Tatizo viongozi wa afrika asilimia kubwa wanatawala kigaidigaidi hakuna mwenye usafi wa kuweza kumukemea mwenzake akili zao wamewekeza kwa wazungu,kama Trump hataingilia kati kumshughurikia Kagame atawapelekesha sana,na bila Kagame kudhibitiwa baada ya kumalizana na Kongo utasikia anaichapa Burundi,mwisho afrika mashariki yote itachapwa na Kagame.
 
Baada ya Mkutano wa usuluhishi kukamilika Dar es salaam Rais Kagame wa Rwanda amesema " hakuna wa Kutupangia" linapokuja swala la ulinzi na ustawi wa Rwanda

Watoto wa Kagame Wote ni Wanajeshi

Credit: Citizen TV
Mshamba tu
 
Hivi kwanini Rwanda isiwekewe vikwazo? Ili tuone hizo silaha zitawafikiaje hao m23. Tukiendelea hivi ataendelea kupeleka jeshi Kongo anachimba madini anapata hela ananunua masilaha makubwa, mwisho atakuja kuichukua kweli kongo yote hata east africa kabisa. Mdharau mwiba mguu huota tende
 
Congo ni mteja wetu mkubwa bila ya congo banadari yetu itayumba, huwezi kupeleka mizigo kama kuna vita, na ukirihusu hwa waasi wawe na nguvu kupambana na jeshi la serikali ina maana hata wewe hapa nchini kwako wanaweza kuja kukuvamia na kusema geita ni mali yao wakaanza kukusumbua hawa waasi sio wa kuchekewa
Umenena vema mkuu. Sasa kama ndivyo, hakuna haja ya kuwabembeleza m23. JWTZ wapelekwe kwa wingi kama alivyofanya JK. na baada ya ushindi wasalie huko kwa miaka mingi hadi kutulie kabisa.
 
Umenena vema mkuu. Sasa kama ndivyo, hakuna haja ya kuwabembeleza m23. JWTZ wapelekwe kwa wingi kama alivyofanya JK. na baada ya ushindi wasalie huko kwa miaka mingi hadi kutulie kabisa.
Huo ndio uhalisia jk alikuwa sahihi kuwamaliza hadi kagame akawa anabweka , kuwachekea hawa ni kudumaza uchumi wetu na kufanya waasi waone kumbe inawezekana kupora mali na ardhi, its a very bad precedent inawekwa
 
Back
Top Bottom