Baada ya kutunukiwa PhD na kuwa Dkt. mnaonaje jina la "Mama" sasa tukaachana nalo ila Nyumbani wanaweza kuendelea kumuita Mama?

Wanabodi,

Angalizo la Bandiko Hili, sijataja jina la mtu yoyote, naomba na wewe usitaje. Hapa nazungumzia title ya mtu kuitwa Mama.

Japo title ya "Mama" ni jina la heshima kwa mwanamke, kila mwanamke kuitwa mama ni heshima kubwa zaidi kwa mwanamke yoyote kuliko kuitwa tuu jina lake, hivyo Tanzania tulipobahatika kupata rais wa kwanza mwanamke, aliyepatikana kwa kudra tuu za Mwenyeenzi Mungu, tunamuita kwa utangulizi wa jina Mama.

Sasa kwa vile amekuwa daktari, mnaonaje sasa kama officially, tutaachana na kumuita Mama, na badala yake, officially aitwe Dr, halafu ofisini kwake na nyumbani kwake, ndio aendelee kuitwa Mama?.

Lengo la kutoa pendekezo hili, ni kufuatia zile mada zangu za powers, majina yana impact kubwa kwa mhusika, hivyo kuna mambo ya metaphysical, na numerology yanayohusiana na majina na matamshi, kwenye words vibrations, kuna maneno fulani ukitamka, hayo maneno yanatoa powerful vibrations kama kwenye kitu kinachoitwa chanting kwenye dini, Hinduism na Budhism ndio wanatumia sana, ila hata Wakristu kwenye Rozari na Waislamu kwenye Tasbihi, wanatumia chanting.

Jina la Mama likitangulizwa, na kurudiwa rudiwa kunamfanya muhusika kufanya mambo ki mama mama, ki softi softi, kuwa na huruma iliyopitiza hivyo kuna maamuzi magumu atashindwa kabisa kuyatekeleza!. Mfano mtu akiisha itwa mama, ataweza kusaini death warrant?. Wakati wale "jamaa zetu" kuna maamuzi fulani hilazimika kuyachukua, na maamuzi hayo, "ukikosa tuu mara mbili, utatakiwa kuandika maelezo, kwanini umekosa".

Hao jamaa kwenye hizo operesheni maalum za kutokosa mara mbili, kabla hazijatekelezwa lazima mkuu aridhie kwa kuidhinisha kwa maandishi, naniliu zitumike!, sasa mtu akiitwa mama, ataweza kweli kusaini zile nanilii kama za Dodoma, kwenye makazi ya wale naniliu, zitumike?.

Maadam sasa huyu ni dakitari, mnaonaje sasa tukaachana kuitana mama kwenye mambo ya kazkaz halafu akaendelea kuitwa mama na watu wake wa karibu, ofisini na nyumbani kwake, lakini sisi tumuite Dr, ili hata ikibidi kumkoma nyani giladi, unamkoma tuu bila kumuangalia usoni!.

Mnalionaje hili wanabodi, jee tuendelee kumuita mama na yeye kutuita wanangu, hilo mkaliangalie, au sasa tumuite Dr, mambo ya huruma za ki mama mama aziache nyumbani na kwenye familia yake, hapa iwe kazi kazi tuu!.

NB. Hii sio mara yangu ya kwanza kuleta mada humu bila kutaja majina, hata mada hii Ikitokea kuna Kiongozi ana Macho mazuri, na umeyapenda, je, kuna ubaya kumsifia macho yake? Ni ukosefu wa heshima na adabu?

Jumapili Njema.
Paskali
Mkuu, kuna Aya moja nimesoma katika hili bandiko ina kipengere kinachogusia mtu mwenye mamalaka anapotaka kufanya maamuzi magumu kuna kitu anatakiwa kuapply, ila umekificha kwa kukiita nanulii, nifungue hapo kwenye nanulii mkuu.
 
Mtu mzima HOVYOO andika mambo yenye tija kwa Taifa jina linaathiri nini
 
Mleta Mada, nakumbuka u Mwanasheria. Nina imani Unazijua sheria na miongozo inayoelekeza namna ya kutumia Cheo cha Udaktari wa Heshima. Sheria ya vyuo vikuu (Cap 346 of Law of Tanzania), na Regulation 62 (1) (d) of the University (General) regulations, G.N No. 226 of 2013 and Standard 4.33 of the Standards and Guidelines of University Education in Tanzania, 2019 kwa Pamoja vinaelekeza matumizi ya Udaktari wa Heshima na namna aliyeupata Udaktari huo anavyotakiwa kuitwa.

Kwa ufafanuzi zaidi, na shauri ukajisomee makala ya Prof . J. Kironde yenye kichwa cha habari "A reflection on honorary doctorate (Honoris Causa) award in Tanzania" iliyochapishwa ukurasa wa 10 kwenye TCU Magazine, January -June, 2020.

Tufuate Taratibu zilizopo, vinginevyo tuzibadili taratibu ili zikidhi hitaji la Sasa. Ni hilo tu mleta mada.
 
Jina la Mama likitangulizwa, na kurudiwa rudiwa kunamfanya muhusika kufanya mambo ki mama mama, ki softi softi, kuwa na huruma iliyopitiza hivyo kuna maamuzi magumu atashindwa kabisa kuyatekeleza!. Mfano mtu akiisha itwa mama, ataweza kusaini death warrant?. Wakati wale "jamaa zetu" kuna maamuzi fulani hilazimika kuyachukua, na maamuzi hayo, "ukikosa tuu mara mbili, utatakiwa kuandika maelezo, kwanini umekosa".
Lakini Mleta mada, huyu sina analo jina la Uchifu, yaani Chifu deshi deshi (umesema tusitaje majina). Yaani jina Chifu nalo ni la kimama mama, kweli?

Kwamba Chifu hawezi kusaini, ☠️ warrant? Tafadhali,Mkuu ebu ipange hoja vizuri, kwa namna ilivyo hii hoja "inatetemeka". Ha ha hahahaha AAA!
 
Mkuu, kuna Aya moja nimesoma katika hili bandiko ina kipengere kinachogusia mtu mwenye mamalaka anapotaka kufanya maamuzi magumu kuna kitu anatakiwa kuapply, ila umekificha kwa kukiita nanulii, nifungue hapo kwenye nanulii mkuu.
Mkuu Elpaul, humu ndani kuna mabandiko ya aina tatu,
1. kuna mabandiko yayozungumzia watu, people, ambayo ni ya simple minds ambao kazi yao ni wana discuss watu, nani, kafanya nini na kutaja taja majina, haya mimi nayaita mabandiko ya kitoto. Kwenye haya mabandiko ya kitoto, mtu ni unapikiwa chakula, unapakuliwa, unatafuniwa, unalishwa, kazi yako ni kumeza tuu kama mtoto anavyo lishwa kwa spoon fed.
2. Kuna mabandiko yanayozungumzia matukio, events, haya ni mabandiko ya watu wa kawaida, wanajadili matukio, kimetokea nini, wapi na ikawaje. Hapa unapikiwa, kupakuliwa na kutafuniwa, ila inatakiwa ule mwenyewe na sio kulishwa kama mtoto.
3. Kuna mabandiko ya kujadili ideas, wazo, haya ni ya GT, mabandiko haya, kwanza hatutaji taji majina ya watu, ni unapikiwa na kupakuliwa tuu, lazima ule mwenyewe, utafune mwenyewe ndipo umeze, kwenye mabandiko haya, hakuna mtu wa kukutafunia wewe kazi yako ibaki ni kumeza, bandiko hili ni unatafuna mwenyewe, kama huwezi kutafuna, maana yake hili ni bandiko la kikubwa kuliko kimo chako!, nenda tuu kwenye mabandiko ya saizi yako.
Pole.
P
 
What's in a name...In Africa wonders never cease!

His Excellency, President for Life, Field Marshal, Al Hadji, Doctor Idi Amin Dada, VC, DSO, MC, Lord of All the Beasts of the Earth and Fishes of the Seas and Conqueror of the British Empire in Africa in General and Uganda in Particular.

Her Excellency, Chief, Mama, Rais, Doctor...
 
Back
Top Bottom