Aisee wewe una akiri sana. Niliwahi kuwa na demu aliyenichunia wiki nzima. Kila nikipiga simu hapokei au nikiandika message hajibu. Sasa nikaamua kumtega kwa message kuwa "baby nimekutumia fedha kidogo kama laki moja hivi. Ikiingia nijulishe." Weeee alikuja fasta eti Oooh samahani baby mara nyingi simu yangu haioneshi kama inaita, kifupi ina matatizo. Kisha akasema baby ila hela haijaingia, nikamwambia subirisubiri labda itaingia. Basi alinisumbua wiki nzima na mimi nikawa namdanganya kwamba nawasiliana na watu wa mpesa nijue nini kimejiri. Baada ya wiki nilimpasulia tu kwamba hakuna cha hela wala nini, nilikuwa nakupima upendo wako tu, sasa nimegundua wewe ni money monger, hamna kitu na tusijuane tena. Yaani alitoa tusi hilo siwezi kulielezea hapa. Na huo ukawa mwisho wa uhusiano wetu.