Baada ya kwenda Dodoma kikazi ameanza dharau “kama zote”

Baada ya kwenda Dodoma kikazi ameanza dharau “kama zote”

Kwa huo wema wako na mapenzi yako ya dhati, tangu uende Dodoma umeshamtumia sh ngapi? Nawashangaa wanaume wanaosema wana mapenzi ya dhati wakati hawawahudumii wapenzi wao kwa chochote mpaka wanakuja kutusumbua sie huku wa pembeni.
Sasa mwenzako keshapata bwana, ukute hapo keshamuhonga simu, ana mtoa outing za maana nk. Unaweza ukasema una mapenzi ya dhati, kwa SI unit yako ila kwa standards za kimataifa ukawa unaburuta mkia. Jitafakari. Kama umepwaya acha nafasi.
Mapenzi ya dhati sio kupiga piga simu ovyo na kumuuliza mwenzako amekula na wakati hujui hata hiyo ela ya kula ameitoa wapi. Wenye mapenzi ya dhati wako wanacheza na M pesa tu.
Nilimpa kutokana na uwezo wangu ulipoishia.. nisingeweza kuiba ili nimridhishe
 
Habari za majukumu wana jf..

Nimatumaini yangu mu wa zima wa afya njemaa..

Back to the point..

Ndugu zangu nimekuwa kwenye mahusiano na binti fulani kwa takribani miaka miwili na nusu sasa.

Kilicho nifanya nije jukwaani hapa muda huu ni kuhusu tabia za huyu mwenzangu ambazo ameanza kuzionesha takribani kwa miezi miwili sasa.

Mi kwasasa nipo Dodoma kikazi na mwenzangu nimemuacha Dar ila tabia yake ndo inaniacha hoi.

Naweza piga simu hata missed calls 8 na hapo nimepiga asubuhi ila cha ajabu akajibu saa 4 usiku tena kwa ufupi tu.

Natuma text ambazo ni za muhimu lakini hajibu wala nikimtafuta nikimuuliza kwanini hakujibu zile txt hunijibu kwa dharau na kwa ufupi tu.

Nimejaribu kujitafakari labda kuna kitu nimemkwaza lakini naona sina kosa. Nimemuuliza mara kwa mara kama kuna shida yoyote kati yetu aniambie asinifiche tuwekane wazi tu ila anadai kila ktu kipo poa tu wakati naona dharau zinazidi kuongezeka siku hadi siku.

Sijathibitisha kama kapata mwanaume wa kumfanya awe hivo au la. Japo ukweli nakapenda mnoo ila kwa dharau zake aisee nimekoma.

Kitu kingine ambacho nimegundua wanawake wembamba ni wana dharau sana na wanajiona wao ndio viumbe bora kabisa hapa duniani. Huyu ni demu wangu wa tatu tunashindwana wa sampuli hii.

Don't trust a woman aisee. Leo nimeamini kuwa mwanamke anapenda awe ananyanyasika tu hapo ndo atatulia.

Siamini wa sithamini tena mwanamke.. Nlijifanya mi ndo mwema na nina mapenzi ya dhati saivi najuta tu.

Nawasilisha
Grow up son.
 
Daaah aisee bado najiuliza hivi hao wanaoaga huwa inakuwaje aisee
Siku ukimpata yule uliyeumbiwa, hakutakuwa na zengwe. Utaona mambo yote ni kama mteremko wa Kitonga. Endelea kubonyeza bonyeza nyanya kisha nunua bilinganya. Hawa madem warembo ni shida. Ndio maana wanaume wengi huwa wanaoa wanawake wa kawaida na wakati walishadate na madem wakali kinoma.
 
Siku ukimpata yule uliyeumbiwa, hakutakuwa na zengwe. Utaona mambo yote ni kama mteremko wa Kitonga. Endelea kubonyeza bonyeza nyanya kisha nunua bilinganya. Hawa madem warembo ni shida. Ndio maana wanaume wengi huwa wanaoa wanawake wa kawaida na wakati walishadate na madem wakali kinoma.
Thanks so much broo.. maneno yako yamenijenga sana aisee
 
Nilimpa kutokana na uwezo wangu ulipoishia.. nisingeweza kuiba ili nimridhishe
Wengine sio wa kujibu kaa kimya fanya hivi usimpigie simu siku nzima wa kumtext nae akikaa kimya bila kukutext na siku ya pili hivyo hivyo jiongeze hapo huna chako wenda atakuwa kampata huyo wa kumtoa outing za maana kama ulivyoambiwa ila huwa wanarudi wenyewe utasikia wanasema ni shetani tu ndo kasababisha kuwa makini na kingine usipende kumpa mwanamke pesa nyingi wakti bado yuko kwao akikuacha ndo chanzo cha kujiua bila kukusudia be care acha aende kwa hao wenye hela utampata tu mwingine maumivu na mawazo ni ya muda tu focus kufanya na kutenda shughuli zako utaongeza kipato na kumpata sitahiki yako
 
Not getting a message is also a message mkuu jiongeze.. au unataka mpaka uitiwe band na matarumbeta ndo uamini kama upendwi tena.. na kwa situation kama hii yako njia au solution sahihi ni ku move on never beg any one to stay in your life.
 
Mkuu utakuwa ume invest sana kwa huyu demu, sidhani kama kilio chako ni cha mapenzi tu.

Kuwa muangalifu kwenye mapenzi, usitupe karata zako zote.
 
ukiwa bado huna mpango wa kuoa usijenge kibanda, ununua tembea..ushauri wa kiume...
 
Tatizo hayo mapenzi ya dhati ume invest kwa wanawake tofauti tofauti na hilo ndio mushkeli mkubwa.
Kwa ushauri wangu achana na fg bali oa kujipunguzia pressure za kila wakati.
Unapenda mtu ambae sio mke wako wala mama yako ni shida sana
 
Back
Top Bottom