Baada ya kwenda kufanya manunuzi, nimeazimia kumrudisha nyumbani kwao

Baada ya kwenda kufanya manunuzi, nimeazimia kumrudisha nyumbani kwao

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
Kwema wakuu,

Nianze kwa kusalimia wanaume wenzangu wote mliooa. Shikamooni!

Taikon wikiendi nilitembelewa na hsemeji yenu. Safari hii akaniambia kuwa amekuja moja kwa moja, yaani anataka tufanye maisha. Nilifurahi sana si unajua tena. Basi jana tulienda kuhemea vitu vya ndani. Nilichokutana nacho huko sio mchezo.

Na hivi ndivyo ilivyokuwa;
1. Mchele. 1kg 3000
2. Sukari 1kg 2800
3. Sabuni mche 3500
4. Tambi 1pct. 2000
5. Mafuta ya kula 1ltr 5500
6. Unga wa sembe 1700
7. Unga wa dona 1600
8. Kubadilisha sas mtungi mdogo 25000
9. Kubadilisha gas mtungi mdogo 52000
10. Mahindi ya makande 1700
11. Maharage 1kg. 3000
12. Dagaa 1kg 10,000
13. Nyama 1kg 8500
14. Kuku wa kienyeji 20,000
15. Majani ya chai 500
16. Mafuta ya kupaka low quality 3000
17. Mafuta ya kupaka normal quality 25,000
18. Mafuta ya kupaka high quality 120,000
19. Dawa ya Mswaki low quality 3000, normal 15,000 high quality 70,000

20. Nauli Daladala 500-8500 per 1route
21. Maziwa fresh 1ltr 2300
22. Maziwa mgando 1Ltr 2700
23. Chapati 1pc 400

Kama hujajipanga kuishi na mwanamke unashauriwa upige kwanza hesabu zako vizuri sana, usije ukaumbuka.
Ujue kwa siku na mwezi unakula kiasi gani? Ujue wka mwezi unatumia mafuta na dawa ya mswaki kiasi gani?

Nisije kukaa mwaka mzima sijamlisha mtoto wa watu kuku bure!

Nduki!

Taikon wa Fasihi,
Muuza Genge.
 
Mwanaume hakimbii matatizo, anakabiliana nayo. MUNGU alisema Mwanaume utakula kwa jasho.

No wonder vijana wa kiume wengi siku hizi wanapenda kulelewa.

Mwanaume hakimbii matatizo lakini pia hayafuati matatizo Kwa sababu tuu yeye ni mwanaume.
Zingatia Hilo

Kutokukimbia matatizo hakukufanyi uyafuate Matatizo.

Mwanaume Kama mambo yako hayajakaa vizuri alafu unatafuta kuoa au kuishi na Mwanamke huko ni kutafuta matatizo.
 
duh na yeye ana mahesabu makali, ss mafuta low quality na high quality ya nn. mkeka ulianza vzuri shida ikaja mwishoni
 
Mkuu wewe upo kwa shem na mke "samahani ni mtarajiwa" bado hajaajiriwa

Amekutembelea wapi🤣🤣🤣🤣🤣 haya mambo tuachie sisi wakongwe 😂😂😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom