Baada ya Lissu kutolewa Sero atahitajika kufanya Reforms ili kujenga Chama chake

Ukitaka kujua CCM wanaakili nenda leo kwenye Mkutano wao pale KAWE

Huko barabarani kumechangamka vilivyo. Mtaani kwetu zimetoka costa nne. Hapa narudi kutoka Sinza kumechangamka vibaya.
Watu wamejipanga
Hizo ndio akili ulizosema Lissu hana na natakiwa awe nazo?
 
Hao wapya watatoka wapi sasa kama wasipoandaliwa na hawa waliopo. Acha tu akina Lissu waendelee na waliopo watajifunza kwa makosa yao
Tundu Lissu hana pumzi na akiendelea hivi kuna uwezekano ukawa ndo mwisho wake kisiasa .

Wako wapi akina Mdude, Soka , Ben saanane n.k
 
Kutumia akili ndio kufanya kitu gani cha upekee? Siasa za TZ ni dhidi ya chama tawala kama uko upinzani, ni mwanasiasa gani aliyetumia akili mbele za CCM akafanikiwa? Huyo anafaa kuwa mfano bora kwa Lissu kumfuata. Kama una mifano tafadhali.

Hata Mbowe ni mwanasiasa aliyetumia mbinu za kimedani kuikabili ccm. Sema muda haukuwa sehemu yake. Hivyo Lisu ilikuwa
Mpango wako ni kuishusha credibility ya Lissu kwa umma. Ushauri wako umejikitika zaidi kumpandikizia elements za "kihuni" kijanja. Andiko lako linawafaa "vipofu". Wenye macho huwapati.

Tunaangalia zaidi matokeo sisi wengine
 
Hata Mbowe ni mwanasiasa aliyetumia mbinu za kimedani kuikabili ccm. Sema muda haukuwa sehemu yake. Hivyo Lisu ilikuwa

Tunaangalia zaidi matokeo sisi wengine
Endelea kuyasubiri. Kila mtu na wito wake hapa duniani. Uzuri Mungu hatoi jukumu bila kutoa vitendea kazi. Lissu ile personality yake hajaumbiwa kwa bahati mbaya!
 
Umesema vizuri, common sense is not common, hapo ndio Lissu anakwama. Momentum mojawapo ambayo ingempa upenyo wa kisiasa ilikuwq kushiriki uchaguzi apate wabunge wengi, wabunge hao wawe ngazi/daraja la kuitikisa CCM baada ya kuichachafya bungeni

..Chadema walishashiriki uchaguzi serikali za mitaa 2024 na ilikuwa vurugu tupu.

..uchaguzi wa 2024 ndio ulipaswa kuwashawishi na kuwahamasisha kushiriki 2025 lakini viashiria vyote vilielekeza kuwa hali itakuwa mbaya.

NB.

..Mama amepitisha sheria ya Tume Huru ya Uchaguzi lakini amegoma kuteua Mwenyekiti, Wakurugenzi, na sekretariat mpya ya Tume hiyo.
 
Tunazungumzia utawala na uongozi katika siasa Mkuu.

Kwenye utawala mbinu zote zinatumika.

Utawala unajua maana yake?
Huyo Mungu unayemtaja na huenda umemjua kwa Biblia au Quran taja mtu kiongozi wa kisiasa aliyetumiwa na Mungu ambaye hakuchanganya mbinu zote

..Zitto Kabwe ana " akili, " je, yuko wapi leo hii?

..James Mbatia ana " akili ," ni mstaarabu, je, yuko wapi leo hii?
 
Usichojua na kuelewa ccm Ina watu wenye akili Sana kumzidi huyo Lissu.

Anachojaribu kuongea hapa Mtibeli kinaleta maana kuwa VITA inahitaji akili .

Kupambana na Ccm bila akili utaishia kuuliwa , kutekwa , kuumizwa n.k

Ccm ndo Dola yenyewe kwahiyo ukitumia approaching za Lissu hauwezi fanikiwa.
Kwa hiyo kwa hoja yako hii unatuambia kuwa approach ya Tundu Lissu ya kupambana CCM na serikali yao dhalimu haijafanikiwa...?

Are you serious with this perception of yours..??

Mimi nakuambia, you are completely wrong....!

Tundu Lissu, kama sio kutumia nguvu za kumsaka kwa kumuua kwa risasi au kwa sumu, then hakuna mtu ndani ya CCM na serikali mwenye akili ya kupambana naye na kumshinda...!!

Sisi ni wanafunzi wake, tunamwelewa na tuko very much inspired naye...

Namshangaa Robert Heriel Mtibeli anavyosema Tundu Lissu hana wanafunzi...

Kama unataka kujua kuwa Tundu Lissu ana au hana wanafunzi, nenda kwenye jimbo ambalo amewahi kuwa mbunge kwa awamu mbili, utafahamu kuwa jimbo lote walishalishwa mafundisho na itikadi ya Tundu Lissu...

Ukipeleka lolote nje ya kile walicholishwa na Lissu, hawakuelewi...
 
Mwenzako yupo field anapambana wewe umebaki na porojo. Nakufananisha na mtu aliyeko nje ya uwanja anavyowajadili wachezaji ila yeye hata danadana hawezi kupiga. Very stupid.
Heri umemjb uyu sijui nini kinamsumbua lissu ni package ya siasa elimu, ujasiri, uzalendo, akili, ujuzi, kipaji yaan hmna kitu lisu kinahitajika mungu hakumpa. Nakushauri nenda Google andika tundu Lissu ni nani mambo saba muhimu yanayomtambulisha mwanasiasa huyu bbc swahili. Asante sana
 
Hamjambo!

Lisu anasifika kwa Umahiri katika taaluma yake ya sheria. Hivyo kusema Lisu ana akili za kisheria hutokuwa umekosea.
Lisu anapenda ukweli jambo ambalo linamfanya aitwe roporopo na Mahasimu wake au watu ambao anagusa interests zao.
Lisu anapenda kupigania Haki, huo inamfanya awe Mwanaharakati zaidi kuliko mwanasiasa.

Mapungufu ya Lisu
1. Lisu ni jasiri lakini asiyetumia Akili. Ni kweli Lisu ana akili lakini katika upande wa sheria lakini katika utawala na mambo ya siasa kidogo anatumia mihemko kuliko Akili.

REFORMS AMBAZO ANATAKIWA KUFANYA;
1. Awe Master, Mwalimu, Kocha wa kufundisha vijana ndani ya chama chake.
Lisu anawafuasi lakini hana wanafunzi wake. Hili kiutawala au kimedani ni kosa.
Hata Yesu au Yohana, au Musa, wote hao walikuwa na wanafunzi wao.
Lisu ni lazima akitoka aandae mpango wa kutafuta vijana ambao atawafundisha uaminifu, kumuamini, kisha awape skills, maono yake, na itikadi yake.
Awa-train kwa kiwango cha kutosha huku akiendelea kujenga chama

Kuna tofauti kubwa ya kuwa na Mfuasi na kuwa na Mwanafunzi.
Kazi ya wafuasi ni kufuata unachosema lakini vipi usiposema, vipi ukiwa haupo iwe umekufa au umetekwa au upo sero kama hivi leo.

Lakini Mwanafunzi yeye ni zaidi ya mfuasi, yeye ni kama successor wako.
Mtume Mohammad yeye alikuwa na wanafunzi wake. Ambao kwa namna nyingi wanamchango katika uislamu.

2. Asitumie Ujasiri wake Bila Akili na Maarifa.
Lisu kama ni mtu mwenye vision na anataka kuacha Legacy itakayotimizwa Ra ikitokea emergency ameondoka. Lazima asitumie ujasiri wake vibaya.

Kutumia ujasiri bila Akili ni kuhujumu harakati zake na kuhatarisha malengo yake. Ambapo itakuwa kazi sawa na Bure

Kiongozi kujipeleka mbele katika uwanja wa vita tena sehemu yenye mashambulizi makali bila mipango ni kujihujumu na kutaka mchezo uishe haraka kabla ya malengo ya ushindi kufikiwa.

3. Kujadili meza Moja na Mahasimu wako ukiwa down ni moja ya mbinu inayofanya kazi.
Lisu yupo pekeake, anawafuasi lakini hana wanafunzi wa kufanya anayoyafikiri au maoni yake hata akiwa hayupo.
Ukishakuwa down usitake kujitutumua na kutaka vita viendelee wakati umeishiwa silaha na mbinu. Umezidiwa.
Kijeshi, ku- Surrender ni moja ya mbinu ya kununua muda.
Hata kwenye vita kwa kidunia tunaona. Unapoingia vitani unapigana ukiona umeishiwa au ukiona malengo yako ya vita yameenda kinyume unaomba vita visitishwe kidogo kisha mjadili matakwa ya hasimu wako hata kama unajua hutatimiza. Ila ni ile ku buy time tuu.

4. Kuunda Mfumo wenye Itikadi yake.
Huwezi ukapewa chama leo na hapohapo ukaanza kutumia watu uliowakuta bila kuwazoezesha mfumo wako mpya. Bila kuwaweka wanamfumo wako ambao ushawapima na kuwaona wanafaa na kumudu.

Tayari una wanafunzi wako lakini pia tayari umeweka baadhi ya wafuasi waliofiti mfumo na itikadi zako

Unapokuwa kiongozi sehemu yoyote ni rahisi kushindwa kuongoza kama utatumia itikadi yako katika watu waliozoea itikadi na mfumo wa mtangulizi wako.

Chama ni kimoja lakini mawazo ya viongozi yanaweza kutofautiana.
Kila kiongozi ana mfumo wake.

Nitakupa Mfano,
Wakati JPM anaingia alikuwa mkalimkali kama alivyo Tundu Kisu.
Ukali bila hesabu hausaidii.
Unapokuwa kiongozi jambo namba moja ni kujenga mfumo wako ambao utautiisha na utakutii kwa moyo wote. Watu mnaoshare same interest, watu wenye maoni yanayofanana, watu wenye falsafa na mitazamo inayofanana.
Huwezi kuwa kiongozi bila kujenga mtandao. Itakusumbua sana na ni rahisi kwa adui zako kukushambulia hasa kutokea ndani.

Tundu Lisu amefanya haraka sana kufanya mashambulizi kana kwamba mpango wake ulikuwa ni miaka mitano tuu.

Huwezi ukafanya mashambulizi ya haraka kwa kiwango kile wakati unajua huna dola.
Na hata ukiwa na Dola bado itakuhitaji muda ili ku-gain momentum.

Kwa sababu hata ukiwa na Dola alafu ndio umeingia madarakani leo. Lazima ujue aliyetoka bado anamfumo wake katika Dola unaloliongoza. Hivyo kusema watakuwa Loyal kwako kisa ndiye mkuu wao muda huo kuliko mtangulizi wako waliyemzoea itakuwa ni uongo.
Utapasuka usipokuwa Makini.

Huwezi tumia vijana walioandaliwa na watu, kocha mwingine, master mwingine ambaye kifalsafa na kimtazamo na interest mnatofautiana. Labda uwe mjinga.

5. Viongozi Smart sio wapiga Kelele.
Unapopiga piga kelele unatoa mwanya kwa adui yako kukusoma na kujua mambo uliyoyaficha bila hata ya wewe kujua
Viongozi wengi wapiga kelele wengi hulambishwa mchanga mapema kutokana na kuongeongea ambapo wanauza ramani ya vita.
Kwenye vita kanuni inayotumika ni ile ya Predators. Working silently

Ngoja ninywe chai.

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
Nasikitika tu sbb afya yake iko rehani🥲
 
Mwenzako yupo field anapambana wewe umebaki na porojo. Nakufananisha na mtu aliyeko nje ya uwanja anavyowajadili wachezaji ila yeye hata danadana hawezi kupiga. Very stupid.

Sasa wewe upo wapi?
Ambao tuko field tunajua Lisu kimchezo amepoteza na yupo maji ya shingo.

Ninyi msiojua huu mchezo ndio mnapotosha mpaka vijana kama kina mdude wamepotea kwa upumbavu wenu
 
Kwa hiyo kwa hoja yako hii unatuambia kuwa approach ya Tundu Lissu ya kupambana CCM na serikali yao dhalimu haijafanikiwa...?

Are you serious with this perception of yours..??

Mimi nakuambia, you are completely wrong....!

Tundu Lissu, kama sio kutumia nguvu za kumsaka kwa kumuua kwa risasi au kwa sumu, then hakuna mtu ndani ya CCM na serikali mwenye akili ya kupambana naye na kumshinda...!!

Sisi ni wanafunzi wake, tunamwelewa na tuko very much inspired naye...

Namshangaa Robert Heriel Mtibeli anavyosema Tundu Lissu hana wanafunzi...

Kama unataka kujua kuwa Tundu Lissu ana au hana wanafunzi, nenda kwenye jimbo ambalo amewahi kuwa mbunge kwa awamu mbili, utafahamu kuwa jimbo lote walishalishwa mafundisho na itikadi ya Tundu Lissu...

Ukipeleka lolote nje ya kile walicholishwa na Lissu, hawakuelewi...
Mbowe mwenyewe mlimsifu Kama hivi .

Ndo maana kikwete kaanua kuwanyoosha
 
Sasa wewe upo wapi?
Ambao tuko field tunajua Lisu kimchezo amepoteza na yupo maji ya shingo.

Ninyi msiojua huu mchezo ndio mnapotosha mpaka vijana kama kina mdude wamepotea kwa upumbavu wenu
Wangekuwa na I'd wanatumia majina rasmi wasingethubutu kuongea hivyo.

Wamejificha na I'd fake huku wakisema No reform no election .

Hawa vilaza ndo walikuwa wakiwapa vichwa akina mdude , Soka n.k
 
1. Awe Master, Mwalimu, Kocha wa kufundisha vijana ndani ya chama chake.
Lisu anawafuasi lakini hana wanafunzi wake. Hili kiutawala au kimedani ni kosa.
Hata Yesu au Yohana, au Musa, wote hao walikuwa na wanafunzi wao.
Lisu ni lazima akitoka aandae mpango wa kutafuta vijana ambao atawafundisha uaminifu, kumuamini, kisha awape skills, maono yake, na itikadi yake.
Awa-train kwa kiwango cha kutosha huku akiendelea kujenga chama
Mbona anao kina Mahinyila, Brenda rupiah, Gwamaka Mbuge, Gervase Lyenda and many more na ndio hasa walimpigia kura kwa mamia yao kuwa mwenyekiti. Sio wakati wote mpaka umtengeneze mtu mmoja mmoja, sometimes misimamo yako, haiba yako inaweza tengeneza wanafunzi bila kuwatuma.
 
Hamjambo!

Lisu anasifika kwa Umahiri katika taaluma yake ya sheria. Hivyo kusema Lisu ana akili za kisheria hutokuwa umekosea.
Lisu anapenda ukweli jambo ambalo linamfanya aitwe roporopo na Mahasimu wake au watu ambao anagusa interests zao.
Lisu anapenda kupigania Haki, huo inamfanya awe Mwanaharakati zaidi kuliko mwanasiasa.

Mapungufu ya Lisu
1. Lisu ni jasiri lakini asiyetumia Akili. Ni kweli Lisu ana akili lakini katika upande wa sheria lakini katika utawala na mambo ya siasa kidogo anatumia mihemko kuliko Akili.

REFORMS AMBAZO ANATAKIWA KUFANYA;
1. Awe Master, Mwalimu, Kocha wa kufundisha vijana ndani ya chama chake.
Lisu anawafuasi lakini hana wanafunzi wake. Hili kiutawala au kimedani ni kosa.
Hata Yesu au Yohana, au Musa, wote hao walikuwa na wanafunzi wao.
Lisu ni lazima akitoka aandae mpango wa kutafuta vijana ambao atawafundisha uaminifu, kumuamini, kisha awape skills, maono yake, na itikadi yake.
Awa-train kwa kiwango cha kutosha huku akiendelea kujenga chama

Kuna tofauti kubwa ya kuwa na Mfuasi na kuwa na Mwanafunzi.
Kazi ya wafuasi ni kufuata unachosema lakini vipi usiposema, vipi ukiwa haupo iwe umekufa au umetekwa au upo sero kama hivi leo.

Lakini Mwanafunzi yeye ni zaidi ya mfuasi, yeye ni kama successor wako.
Mtume Mohammad yeye alikuwa na wanafunzi wake. Ambao kwa namna nyingi wanamchango katika uislamu.

2. Asitumie Ujasiri wake Bila Akili na Maarifa.
Lisu kama ni mtu mwenye vision na anataka kuacha Legacy itakayotimizwa Ra ikitokea emergency ameondoka. Lazima asitumie ujasiri wake vibaya.

Kutumia ujasiri bila Akili ni kuhujumu harakati zake na kuhatarisha malengo yake. Ambapo itakuwa kazi sawa na Bure

Kiongozi kujipeleka mbele katika uwanja wa vita tena sehemu yenye mashambulizi makali bila mipango ni kujihujumu na kutaka mchezo uishe haraka kabla ya malengo ya ushindi kufikiwa.

3. Kujadili meza Moja na Mahasimu wako ukiwa down ni moja ya mbinu inayofanya kazi.
Lisu yupo pekeake, anawafuasi lakini hana wanafunzi wa kufanya anayoyafikiri au maoni yake hata akiwa hayupo.
Ukishakuwa down usitake kujitutumua na kutaka vita viendelee wakati umeishiwa silaha na mbinu. Umezidiwa.
Kijeshi, ku- Surrender ni moja ya mbinu ya kununua muda.
Hata kwenye vita kwa kidunia tunaona. Unapoingia vitani unapigana ukiona umeishiwa au ukiona malengo yako ya vita yameenda kinyume unaomba vita visitishwe kidogo kisha mjadili matakwa ya hasimu wako hata kama unajua hutatimiza. Ila ni ile ku buy time tuu.

4. Kuunda Mfumo wenye Itikadi yake.
Huwezi ukapewa chama leo na hapohapo ukaanza kutumia watu uliowakuta bila kuwazoezesha mfumo wako mpya. Bila kuwaweka wanamfumo wako ambao ushawapima na kuwaona wanafaa na kumudu.

Tayari una wanafunzi wako lakini pia tayari umeweka baadhi ya wafuasi waliofiti mfumo na itikadi zako

Unapokuwa kiongozi sehemu yoyote ni rahisi kushindwa kuongoza kama utatumia itikadi yako katika watu waliozoea itikadi na mfumo wa mtangulizi wako.

Chama ni kimoja lakini mawazo ya viongozi yanaweza kutofautiana.
Kila kiongozi ana mfumo wake.

Nitakupa Mfano,
Wakati JPM anaingia alikuwa mkalimkali kama alivyo Tundu Kisu.
Ukali bila hesabu hausaidii.
Unapokuwa kiongozi jambo namba moja ni kujenga mfumo wako ambao utautiisha na utakutii kwa moyo wote. Watu mnaoshare same interest, watu wenye maoni yanayofanana, watu wenye falsafa na mitazamo inayofanana.
Huwezi kuwa kiongozi bila kujenga mtandao. Itakusumbua sana na ni rahisi kwa adui zako kukushambulia hasa kutokea ndani.

Tundu Lisu amefanya haraka sana kufanya mashambulizi kana kwamba mpango wake ulikuwa ni miaka mitano tuu.

Huwezi ukafanya mashambulizi ya haraka kwa kiwango kile wakati unajua huna dola.
Na hata ukiwa na Dola bado itakuhitaji muda ili ku-gain momentum.

Kwa sababu hata ukiwa na Dola alafu ndio umeingia madarakani leo. Lazima ujue aliyetoka bado anamfumo wake katika Dola unaloliongoza. Hivyo kusema watakuwa Loyal kwako kisa ndiye mkuu wao muda huo kuliko mtangulizi wako waliyemzoea itakuwa ni uongo.
Utapasuka usipokuwa Makini.

Huwezi tumia vijana walioandaliwa na watu, kocha mwingine, master mwingine ambaye kifalsafa na kimtazamo na interest mnatofautiana. Labda uwe mjinga.

5. Viongozi Smart sio wapiga Kelele.
Unapopiga piga kelele unatoa mwanya kwa adui yako kukusoma na kujua mambo uliyoyaficha bila hata ya wewe kujua
Viongozi wengi wapiga kelele wengi hulambishwa mchanga mapema kutokana na kuongeongea ambapo wanauza ramani ya vita.
Kwenye vita kanuni inayotumika ni ile ya Predators. Working silently

Ngoja ninywe chai.

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam

No reform no election wewe unaongelea mambo ya mwaka kesho. Matukio ndiyo yanaanza
 
Back
Top Bottom