Baada ya Magufuli, 2025 Makonda atatufaa sana kwasababu ana uthubutu kuliko hata JPM!

Baada ya Magufuli, 2025 Makonda atatufaa sana kwasababu ana uthubutu kuliko hata JPM!

Wanabodi,
Kabla Magufuli hajawa rais wetu, sisi wengine wenu tulijua tangu mwaka 2014 na tukasema humu!.Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli

Miongoni mwa sifa zilizomuibua Magufuli ni sifa inayoitwa "uthubutu" unreasonably ambayo wengine huita ni udikiteta. Yaani kuachana na mambo ya kufuata sheria, taratibu na kanuni, ndiyo yametufikisha hapa, hawa viongozi wenye "uthubutu" hawahitaji kujua sheria, taratibu na kanuni, zinataka nini, bali hufanya lile linalowezekana,

Ndio maana tukasema humu, japo Magufuli kweli ni dikiteta, Tanzania mahali ilipofika ilimhitaji mtu kama Magufuli na Mwenyeenzi Mungu akaisikia sala yetu, akatupatia Magufuli!.
Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata!. Atakayeleta Fyoko, Ataisoma Namba!

Tukija kwa Makonda, muda mfupi baada ya kuteuliwa DC wa Kinondoni, akaonyesha uwezo, hivyo kama ilivyokuwa kwa Magufuli, mwaka 2014 tulisema ni Magufuli, na mwaka 2015 kweli akawa yeye. Vivyo hivyo kwa Makonda akiwa DC, akina sisi tukasema hivi Nimemkubali Sana DC Makonda, anafaa kuwa Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam
Na kweli haukupita muda akawa!.

Hivyo kwa hii kazi nzuri yote anayoifanya Magufuli, atakapoondoka ile 2025, kama hatamuachia nchi mtu mwenye kufuata nyayo zake, hii kazi nzuri yote ya Magufuli itakuwa ni kazi bure! . Hivyo nimeshauri Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?

Kwa vile katiba sio Msahafu, 2025 tuibadili katiba Magufuli aendelee indefinitely kama Mugabe, mpaka atakapo choka kabisa na kuwa hawezi tena kwa incapacitation, au tumsubirie Mungu, au Tanzania sasa na sisi tuanze mtindo wa spotting na headhunting na kumfantia grooming huyo headhunted.

Kwa maoni yangu Makonda atatufaa sana kumpokea Magufuli, maana kiukweli huyu Jamaa atatufaa sana kwa sababu ana uthubutu mkubwa zaidi kuliko hata Magufuli. Makonda akimpokea kiukweli kabisa Tanzania itanyooka.

Magufuli pamoja na mazuri yake, naye kama binadamu pia ana madhaifu na mapungufu yake, Vivyo hivyo Makonda pia sio malaika naye ana mapungufu yake, moja ya mapungufu makubwa ya Makonda ni inferiority complex inayopelekea ku practice superiority complex na kujikuta ana over do bila kujijua.

Psychoanalysis: Superiority Complex ni Dalili ya Inferiority Complex!. Maneno Mafupi Vitendo Virefu.

Mfano ni jinsi anavyojikomba komba kwa rais Magufuli mpaka kupindukia, karibu kila jambo lazima amtaje rais Magufuli tena kwa majina yake yote manne na sifa zake zote nne "Rais Wetu Mpendwa Mheshimiwa Dr. John Pombe Joseph Magufuli" (si mnajua watu wa Kanda yetu kwa kupenda masifa). Makonda lazima afike mahali aonyeshe anaweza kusimama on his own na sio kila wakati kutegemea apron strings za rais Magufuli.

Hivyo 2025 rais Magufuli asipoongeza muda, Makonda atatufaa sana. Kwa vile Makonda ni Mlolomije, kwa kuanzia 2020 akalichukue lile jimbo la yule chapombe, na atashinda kwa kishindo na kupewa moja ya important portfolio zenye impact, ili 2025 ampokee Magufuli.

Kitendo cha mtu wa Kanda ya Ziwa kushika urais kama alivyo rais Magufuli, ni dalili ya Tanzania kutenda haki ya wengi wape, yaani wenye haki na uhalali wa kutawala nchi ni wale walio wengi!. Hivyo baada ya rais Magufuli aje rais Makonda, na baada ya hapo tuendelee kule kule mpaka na makabila mengine wawe ni walio wengi ndipo nao wastahiki! .

Makonda konyesha uwezo wa uthubutu, jee mnalionaje hili la kwanini asiwe Makonda kumpokea Magufuli?.

Kwa kwa wale mashabiki wa upinzani mtanisamehe bure, kwenye urais upinzani ni bado sana.

Paskali.
Mkuu Pascal Mayalla kumbe hii ndio imekufanya leo ukengeuka na kutaka sheria uliyoisoma kwa jasho inajisiwe?
 
Mkuu, kuna popote imeelezwa kuwa mkurupukaji hawezi kuwa rais wa Tanzania?!. Kwenye hii hoja ya ukurupukaji, wewe umemuona Makonda Tuu?!.
P.
Sikupingi ndugu yangu kwa hoja zako huwa una maono lakini kwa Makonda akisimama kugombea urais upinzani utakuwa na nguvu sana na kama sio upinzani kuchukua nchi basi watapishana kura chache sana
 
Sikupingi ndugu yangu kwa hoja zako huwa una maono lakini kwa Makonda akisimama kugombea urais upinzani utakuwa na nguvu sana na kama sio upinzani kuchukua nchi basi watapishana kura chache sana
Mkuu Alpha, Jee Tanzania tunaupinzani wa kuishinda CCM?. Jee hujawahi kusikia kuwa CCM itatawala milele?.

Kupata maendeleo ya kweli, Watanzania ni lazima tujifunze kuukubali ukweli!. Hili la CCM kutawala milele ni kweli!. - JamiiForums

In 2015 Election, Tanzania had A Choice To Choose From. Jee Kwa 2020, Do We Still Have A Choice?. - JamiiForums

Je, CHADEMA inaweza kushinda 2020? Is it serious, credible & mature enough opposition?!. - JamiiForums

P
 
Anaweza kuja kurithishwa au baada ya kumuona ana uwezo, ni halali yake kuja kumpokea, na ndio maana sisi wengine tayari tumeisha anza kumpigia chapuo!.

P.
Paskal, hivi uwezo ni kuvitafuta vyombo vya habari vifuatane nawe kila uendako na kutangaza
Nini jambo alofanya likafaulu Makonda tumpe sifa? Mie nakuambia hii issue ya makontena ya vifaa asemavyo vya shule habari za ndani kabisa zinasema hapo ndio amebugi, mambo yako hadharani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
U
Paskal, hivi uwezo ni kuvitafuta vyombo vya habari vifuatane nawe kila uendako na kutangaza
Nini jambo alofanya likafaulu Makonda tumpe sifa? Mie nakuambia hii issue ya makontena ya vifaa asemavyo vya shule habari za ndani kabisa zinasema hapo ndio amebugi, mambo yako hadharani

Sent using Jamii Forums mobile app
Ukiwa ni mpakwa mafuta, ni YEYE mwenyewe atasimamia kila kitu na yote yatapita, mpakwa mafuta atasimama!.

Kwani kwenye issue ya uvamizi wa Clouds, Nape anakosa gani?.

Tafuta kisa cha Shadrack, Meshaki na Abednego kwenye Bible utaelewa.

Angalia mapito ya kijana
Mafanikio ya Makonda ni Uthibitisho Wa Jiwe Walilolikataa Waashi Litafanywa Kuwa Jiwe Kuu la Pembeni - JamiiForums
P
 
Ukisikia uendawazimu ndio huu, naona lengo lako ni kujaribu kubakisha 'utukufu' ktk 'kanda pendwa'. sikutarajia kama ungeweza kuleta kichekesho kama hiki Mayala.
 
Hapa sasa naona kama unahukumu na kulaani. Unajuaje kama viongozi Wasukuma hawatakuja kufanya vizuri?, kwani wewe ni Mungu?!.

Hili la kuhukumu nakushauri

Tuacheni Ramli Chonganishi: Tusihukumu, Tusije Tukahukumiwa!. "Karma Ndio Pekee Hutoa Hukumu ya Haki Hapa Duniani!.

Hili la Wasukuma hawajawahi kufanya vizuri it's just a matter of time, kama hii ni miaka 3 tuu,
  1. Barabara za lami nchi nzima!.
  2. Barabara za juu kwa juu!.
  3. Midege 7 mipya hadi dreamliner
  4. Reli ya SGR
  5. Mabasi ya mwendo kasi
  6. Mijengo ya ajabu!.
  7. Kuhamia Dodoma!.
  8. Watumishi Hewa!.
  9. Waliofoji vyeti out!.
  10. Utumbuaji Majipu!.
  11. Safari za Nje!.
  12. Mafisadi...
  13. Wavivu...
  14. Wazembe...
  15. Wala Rushwa...
  16. Vita vya rushwa
  17. Vita vya ufisadi
  18. Mfariji wa wanyonge
  19. Makinikia
  20. Gawio la mabilioni
  21. Maduhuli yanakusanywa
  22. Kodi inakusanywa
  23. Hapa kazi tuu
  24. Live kibao za Ikulu
  25. Sheria ya haki ya kupata habari
  26. Sheria mpya ya habari
  27. Sheria mpya ya madini
  28. Elimu bure
  29. Mikopo ya Elumu ya juu
and the list goes on..
Tumeshauri
Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?
P.
Kuanzia no.5 jitafakari

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mkuu mbona umeandika bila kutoa hoja zenye mashiko..

Uthubutu waweza fanyika hata kwa mambo yasiyo na tija kama ilivyo kwa makonda. Ni heri ungefafanua amekuwa na uthubutu kwenye mambo gsni yenye tija kwa wana dsm?

Pili huwezi sifia mtu mwenye uthubutu wa kuua watu na kukalia sheria za nchi mabaya yanakuwa mengi zaidi ya mazuri hapa msifiaji ni lazima hayuko neutral.

Unasifia bila kuangalia ule upande wa wanaoumizwa bila sababu za msingi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kitendo cha mtu wa Kanda ya Ziwa kushika urais kama alivyo rais Magufuli, ni dalili ya Tanzania kutenda haki ya wengi wape, yaani wenye haki na uhalali wa kutawala nchi ni wale walio wengi!. Hivyo baada ya rais Magufuli aje rais Makonda, na baada ya hapo tuendelee kule kule mpaka na makabila mengine wawe ni walio wengi ndipo nao wastahiki! .
Mkuu saluti kwanza!!! Kuna wakati Mwalimu alisema kuna makabila fulani musiype urais. Sisi hatukumsikia. Leo tunaona. Nadhani akitoka Makonda, 2035, iwe zamu yako. Munafanana kiasi ingawa siyo sana. Lakini wewe una sifa za ziada. Kwamba umechanganya. Kuishi kwingi ni kuona mengi. Ishi mwanangu uone dunia.
 
Huu uzi kwa kukurupuka huwezi kuuelewa
Mimi nimekuelewa sana mkuu Pascal Mayalla
Mkuu Kwetu Kaya, jf was meant to be the home of great thinkers, wenye great minds, hivyo kuna threads only the great minds ndio wanaelewa, lakini kwa vile pia tuko na simple minds, na ordinary minds, wote ni wenzetu, twende nao hivyo hivyo, kila mmoja wao kwa kiwango cha uelewa wake.
P.
 
Ukisikia uendawazimu ndio huu, naona lengo lako ni kujaribu kubakisha 'utukufu' ktk 'kanda pendwa'. sikutarajia kama ungeweza kuleta kichekesho kama hiki Mayala.
Mkuu Kichaa, kauli huumba, hata mtu kama ulikuwa mzima kabisa, ukajiita kichaa, kutokana na kuitwa kichaa, ukichaa unakuingia bila wewe kujijua, kwa sababu

Kuwa Kichaa Sio Mpaka Kuokota Makopo!. Jee Tanzania Tuna Vichaa Wengi Kuliko Tunavyojidhania?!. - JamiiForums

Kitendo cha kuliita bandiko hili ni uendawazimu ndio uthibitisho wa ukichaa wako.

Kama unadhani lengo ni kubakisha, subirie yatimie, ndipo tutaelewana, nani mwendawazimu.
Pole na samahani.
P.
 
Back
Top Bottom