Baada ya Magufuli, 2025 Makonda atatufaa sana kwasababu ana uthubutu kuliko hata JPM!

Wanabodi,
Kabla Magufuli hajawa rais wetu, sisi wengine wenu tulijua tangu mwaka 2014 na tukasema humu!.Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli

Miongoni mwa sifa zilizomuibua Magufuli ni sifa inayoitwa "uthubutu" unreasonably ambayo wengine huita ni udikiteta. Yaani kuachana na mambo ya kufuata sheria, taratibu na kanuni, ndiyo yametufikisha hapa, hawa viongozi wenye "uthubutu" hawahitaji kujua sheria, taratibu na kanuni, zinataka nini, bali hufanya lile linalowezekana,

Ndio maana tukasema humu, japo Magufuli kweli ni dikiteta, Tanzania mahali ilipofika ilimhitaji mtu kama Magufuli na Mwenyeenzi Mungu akaisikia sala yetu, akatupatia Magufuli!.
Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata!. Atakayeleta Fyoko, Ataisoma Namba!

Tukija kwa Makonda, muda mfupi baada ya kuteuliwa DC wa Kinondoni, akaonyesha uwezo, hivyo kama ilivyokuwa kwa Magufuli, mwaka 2014 tulisema ni Magufuli, na mwaka 2015 kweli akawa yeye. Vivyo hivyo kwa Makonda akiwa DC, akina sisi tukasema hivi Nimemkubali Sana DC Makonda, anafaa kuwa Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam
Na kweli haukupita muda akawa!.

Hivyo kwa hii kazi nzuri yote anayoifanya Magufuli, atakapoondoka ile 2025, kama hatamuachia nchi mtu mwenye kufuata nyayo zake, hii kazi nzuri yote ya Magufuli itakuwa ni kazi bure! . Hivyo nimeshauri Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?

Kwa vile katiba sio Msahafu, 2025 tuibadili katiba Magufuli aendelee indefinitely kama Mugabe, mpaka atakapo choka kabisa na kuwa hawezi tena kwa incapacitation, au tumsubirie Mungu, au Tanzania sasa na sisi tuanze mtindo wa spotting na headhunting na kumfantia grooming huyo headhunted.

Kwa maoni yangu Makonda atatufaa sana kumpokea Magufuli, maana kiukweli huyu Jamaa atatufaa sana kwa sababu ana uthubutu mkubwa zaidi kuliko hata Magufuli. Makonda akimpokea kiukweli kabisa Tanzania itanyooka.

Magufuli pamoja na mazuri yake, naye kama binadamu pia ana madhaifu na mapungufu yake, Vivyo hivyo Makonda pia sio malaika naye ana mapungufu yake, moja ya mapungufu makubwa ya Makonda ni inferiority complex inayopelekea ku practice superiority complex na kujikuta ana over do bila kujijua.

Psychoanalysis: Superiority Complex ni Dalili ya Inferiority Complex!. Maneno Mafupi Vitendo Virefu.

Mfano ni jinsi anavyojikomba komba kwa rais Magufuli mpaka kupindukia, karibu kila jambo lazima amtaje rais Magufuli tena kwa majina yake yote manne na sifa zake zote nne "Rais Wetu Mpendwa Mheshimiwa Dr. John Pombe Joseph Magufuli" (si mnajua watu wa Kanda yetu kwa kupenda masifa). Makonda lazima afike mahali aonyeshe anaweza kusimama on his own na sio kila wakati kutegemea apron strings za rais Magufuli.

Hivyo 2025 rais Magufuli asipoongeza muda, Makonda atatufaa sana. Kwa vile Makonda ni Mlolomije, kwa kuanzia 2020 akalichukue lile jimbo la yule chapombe, na atashinda kwa kishindo na kupewa moja ya important portfolio zenye impact, ili 2025 ampokee Magufuli.

Kitendo cha mtu wa Kanda ya Ziwa kushika urais kama alivyo rais Magufuli, ni dalili ya Tanzania kutenda haki ya wengi wape, yaani wenye haki na uhalali wa kutawala nchi ni wale walio wengi!. Hivyo baada ya rais Magufuli aje rais Makonda, na baada ya hapo tuendelee kule kule mpaka na makabila mengine wawe ni walio wengi ndipo nao wastahiki! .

Makonda konyesha uwezo wa uthubutu, jee mnalionaje hili la kwanini asiwe Makonda kumpokea Magufuli?.

Kwa kwa wale mashabiki wa upinzani mtanisamehe bure, kwenye urais upinzani ni bado sana.

Paskali.
Kabla hamjafanya hayo vunjeni muungano kwanza murudi kwenye tanganyika yenu ,kwasababu Sisi wa zanzibari tushachoka na huo muungano bila ya dikteta je ujekua na dikteta ?
 
Kama Makonda atakuwa Raisi wa Tanzania basi Tanzania na watanzania watapata tabu sana kimaisha "national na International",kweli Makonda ni mthubutu lakini uthubutu wake ni usiofata sheria,mtu kama huyo hafai kuwaongoza wenzake!,sheria zinatungwa na watanzania wenyewe ili ziwaongoze katika maisha yao ya kila siku..

Kiongozi anaepinga sheria za nchi sio tu anakuwa Dikteta bali anakuwa kawadharau wale anao waongoza,Watanzania wengi hivi sasa ukiwauliza kuhusu Raisi wao Magufuli watakwambia hawampendi kwasababu anakiuka sheria na katiba ya nchi...

Makonda maamuzi yake mengi anayoyafanya ni ya kikejeli,kiubabe na ya kuwadharau watanzania,Nchi ikitaka iendelee lazima ifate sheria zake,lazima ifate katiba yake la si hivyo hapo kunakuwa hakuna nchi kunakuwa hakuna viongozi isipokuwa kunakuwa na genge la watu wanaowatawala na kuwaongoza watu wengine,Na hivyo ndivyo ilivyo Tanzania katika utawala huu wa Magufuli
 
Pascal hebu jaribu kumuogopa Mungu.
Yaani unamzungumzia Makonda huyu huyu alotupigia mzee wetu Warioba!
kampiga mzee tena jaji na waziri mkuu mstaafu sa unazani atashindwa nini kutukandamiza wanyonge.
Pascal ana kila dalili za kulipwa na makonda kumtetea,a true purpet!
 
Seriously mtu
Unapost mada kusema Makonda awe rais! Atauza nchi haswa na atajimilikisha kupita maelezo, kama kaanza kuhadaa kaja na saman za shukr
Kumbe kun zake binafsi what do you expect? Tuache utan bana Makonda hana sifa za uongozi! Hastahili
Kua kiongozi labda akajifunde chuo cha uongozi ndio tumfikirie
 
Wanabodi,
Kabla Magufuli hajawa rais wetu, sisi wengine wenu tulijua tangu mwaka 2014 na tukasema humu!.Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli

Miongoni mwa sifa zilizomuibua Magufuli ni sifa inayoitwa "uthubutu" unreasonably ambayo wengine huita ni udikiteta. Yaani kuachana na mambo ya kufuata sheria, taratibu na kanuni, ndiyo yametufikisha hapa, hawa viongozi wenye "uthubutu" hawahitaji kujua sheria, taratibu na kanuni, zinataka nini, bali hufanya lile linalowezekana,

Ndio maana tukasema humu, japo Magufuli kweli ni dikiteta, Tanzania mahali ilipofika ilimhitaji mtu kama Magufuli na Mwenyeenzi Mungu akaisikia sala yetu, akatupatia Magufuli!.
Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata!. Atakayeleta Fyoko, Ataisoma Namba!

Tukija kwa Makonda, muda mfupi baada ya kuteuliwa DC wa Kinondoni, akaonyesha uwezo, hivyo kama ilivyokuwa kwa Magufuli, mwaka 2014 tulisema ni Magufuli, na mwaka 2015 kweli akawa yeye. Vivyo hivyo kwa Makonda akiwa DC, akina sisi tukasema hivi Nimemkubali Sana DC Makonda, anafaa kuwa Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam
Na kweli haukupita muda akawa!.

Hivyo kwa hii kazi nzuri yote anayoifanya Magufuli, atakapoondoka ile 2025, kama hatamuachia nchi mtu mwenye kufuata nyayo zake, hii kazi nzuri yote ya Magufuli itakuwa ni kazi bure! . Hivyo nimeshauri Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?

Kwa vile katiba sio Msahafu, 2025 tuibadili katiba Magufuli aendelee indefinitely kama Mugabe, mpaka atakapo choka kabisa na kuwa hawezi tena kwa incapacitation, au tumsubirie Mungu, au Tanzania sasa na sisi tuanze mtindo wa spotting na headhunting na kumfantia grooming huyo headhunted.

Kwa maoni yangu Makonda atatufaa sana kumpokea Magufuli, maana kiukweli huyu Jamaa atatufaa sana kwa sababu ana uthubutu mkubwa zaidi kuliko hata Magufuli. Makonda akimpokea kiukweli kabisa Tanzania itanyooka.

Magufuli pamoja na mazuri yake, naye kama binadamu pia ana madhaifu na mapungufu yake, Vivyo hivyo Makonda pia sio malaika naye ana mapungufu yake, moja ya mapungufu makubwa ya Makonda ni inferiority complex inayopelekea ku practice superiority complex na kujikuta ana over do bila kujijua.

Psychoanalysis: Superiority Complex ni Dalili ya Inferiority Complex!. Maneno Mafupi Vitendo Virefu.

Mfano ni jinsi anavyojikomba komba kwa rais Magufuli mpaka kupindukia, karibu kila jambo lazima amtaje rais Magufuli tena kwa majina yake yote manne na sifa zake zote nne "Rais Wetu Mpendwa Mheshimiwa Dr. John Pombe Joseph Magufuli" (si mnajua watu wa Kanda yetu kwa kupenda masifa). Makonda lazima afike mahali aonyeshe anaweza kusimama on his own na sio kila wakati kutegemea apron strings za rais Magufuli.

Hivyo 2025 rais Magufuli asipoongeza muda, Makonda atatufaa sana. Kwa vile Makonda ni Mlolomije, kwa kuanzia 2020 akalichukue lile jimbo la yule chapombe, na atashinda kwa kishindo na kupewa moja ya important portfolio zenye impact, ili 2025 ampokee Magufuli.

Kitendo cha mtu wa Kanda ya Ziwa kushika urais kama alivyo rais Magufuli, ni dalili ya Tanzania kutenda haki ya wengi wape, yaani wenye haki na uhalali wa kutawala nchi ni wale walio wengi!. Hivyo baada ya rais Magufuli aje rais Makonda, na baada ya hapo tuendelee kule kule mpaka na makabila mengine wawe ni walio wengi ndipo nao wastahiki! .

Makonda konyesha uwezo wa uthubutu, jee mnalionaje hili la kwanini asiwe Makonda kumpokea Magufuli?.

Kwa kwa wale mashabiki wa upinzani mtanisamehe bure, kwenye urais upinzani ni bado sana.

Paskali.
Kwahiyo msomi unataka tutawaliwe na zero brain?

Sent using Mikoyan MiG-29
 
Hapa sasa naona kama unahukumu na kulaani. Unajuaje kama viongozi Wasukuma hawatakuja kufanya vizuri?, kwani wewe ni Mungu?!.

Hili la kuhukumu nakushauri

Tuacheni Ramli Chonganishi: Tusihukumu, Tusije Tukahukumiwa!. "Karma Ndio Pekee Hutoa Hukumu ya Haki Hapa Duniani!.

Hili la Wasukuma hawajawahi kufanya vizuri it's just a matter of time, kama hii ni miaka 3 tuu,
  1. Barabara za lami nchi nzima!.
  2. Barabara za juu kwa juu!.
  3. Midege 7 mipya hadi dreamliner
  4. Reli ya SGR
  5. Mabasi ya mwendo kasi
  6. Mijengo ya ajabu!.
  7. Kuhamia Dodoma!.
  8. Watumishi Hewa!.
  9. Waliofoji vyeti out!.
  10. Utumbuaji Majipu!.
  11. Safari za Nje!.
  12. Mafisadi...
  13. Wavivu...
  14. Wazembe...
  15. Wala Rushwa...
  16. Vita vya rushwa
  17. Vita vya ufisadi
  18. Mfariji wa wanyonge
  19. Makinikia
  20. Gawio la mabilioni
  21. Maduhuli yanakusanywa
  22. Kodi inakusanywa
  23. Hapa kazi tuu
  24. Live kibao za Ikulu
  25. Sheria ya haki ya kupata habari
  26. Sheria mpya ya habari
  27. Sheria mpya ya madini
  28. Elimu bure
  29. Mikopo ya Elumu ya juu
and the list goes on..
Tumeshauri
Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?
P.
Sio sure inaanza kwa na wasiwasi...!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom