Baada ya Magufuli, 2025 Makonda atatufaa sana kwasababu ana uthubutu kuliko hata JPM!

Mkuu Pascal Mayalla kumbe hii ndio imekufanya leo ukengeuka na kutaka sheria uliyoisoma kwa jasho inajisiwe?
 
Mkuu, kuna popote imeelezwa kuwa mkurupukaji hawezi kuwa rais wa Tanzania?!. Kwenye hii hoja ya ukurupukaji, wewe umemuona Makonda Tuu?!.
P.
Sikupingi ndugu yangu kwa hoja zako huwa una maono lakini kwa Makonda akisimama kugombea urais upinzani utakuwa na nguvu sana na kama sio upinzani kuchukua nchi basi watapishana kura chache sana
 
Sikupingi ndugu yangu kwa hoja zako huwa una maono lakini kwa Makonda akisimama kugombea urais upinzani utakuwa na nguvu sana na kama sio upinzani kuchukua nchi basi watapishana kura chache sana
Mkuu Alpha, Jee Tanzania tunaupinzani wa kuishinda CCM?. Jee hujawahi kusikia kuwa CCM itatawala milele?.

Kupata maendeleo ya kweli, Watanzania ni lazima tujifunze kuukubali ukweli!. Hili la CCM kutawala milele ni kweli!. - JamiiForums

In 2015 Election, Tanzania had A Choice To Choose From. Jee Kwa 2020, Do We Still Have A Choice?. - JamiiForums

Je, CHADEMA inaweza kushinda 2020? Is it serious, credible & mature enough opposition?!. - JamiiForums

P
 
Anaweza kuja kurithishwa au baada ya kumuona ana uwezo, ni halali yake kuja kumpokea, na ndio maana sisi wengine tayari tumeisha anza kumpigia chapuo!.

P.
Paskal, hivi uwezo ni kuvitafuta vyombo vya habari vifuatane nawe kila uendako na kutangaza
Nini jambo alofanya likafaulu Makonda tumpe sifa? Mie nakuambia hii issue ya makontena ya vifaa asemavyo vya shule habari za ndani kabisa zinasema hapo ndio amebugi, mambo yako hadharani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
U
Ukiwa ni mpakwa mafuta, ni YEYE mwenyewe atasimamia kila kitu na yote yatapita, mpakwa mafuta atasimama!.

Kwani kwenye issue ya uvamizi wa Clouds, Nape anakosa gani?.

Tafuta kisa cha Shadrack, Meshaki na Abednego kwenye Bible utaelewa.

Angalia mapito ya kijana
Mafanikio ya Makonda ni Uthibitisho Wa Jiwe Walilolikataa Waashi Litafanywa Kuwa Jiwe Kuu la Pembeni - JamiiForums
P
 
Ukisikia uendawazimu ndio huu, naona lengo lako ni kujaribu kubakisha 'utukufu' ktk 'kanda pendwa'. sikutarajia kama ungeweza kuleta kichekesho kama hiki Mayala.
 
Kuanzia no.5 jitafakari

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mkuu mbona umeandika bila kutoa hoja zenye mashiko..

Uthubutu waweza fanyika hata kwa mambo yasiyo na tija kama ilivyo kwa makonda. Ni heri ungefafanua amekuwa na uthubutu kwenye mambo gsni yenye tija kwa wana dsm?

Pili huwezi sifia mtu mwenye uthubutu wa kuua watu na kukalia sheria za nchi mabaya yanakuwa mengi zaidi ya mazuri hapa msifiaji ni lazima hayuko neutral.

Unasifia bila kuangalia ule upande wa wanaoumizwa bila sababu za msingi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu saluti kwanza!!! Kuna wakati Mwalimu alisema kuna makabila fulani musiype urais. Sisi hatukumsikia. Leo tunaona. Nadhani akitoka Makonda, 2035, iwe zamu yako. Munafanana kiasi ingawa siyo sana. Lakini wewe una sifa za ziada. Kwamba umechanganya. Kuishi kwingi ni kuona mengi. Ishi mwanangu uone dunia.
 
Huu uzi kwa kukurupuka huwezi kuuelewa
Mimi nimekuelewa sana mkuu Pascal Mayalla
Mkuu Kwetu Kaya, jf was meant to be the home of great thinkers, wenye great minds, hivyo kuna threads only the great minds ndio wanaelewa, lakini kwa vile pia tuko na simple minds, na ordinary minds, wote ni wenzetu, twende nao hivyo hivyo, kila mmoja wao kwa kiwango cha uelewa wake.
P.
 
Ukisikia uendawazimu ndio huu, naona lengo lako ni kujaribu kubakisha 'utukufu' ktk 'kanda pendwa'. sikutarajia kama ungeweza kuleta kichekesho kama hiki Mayala.
Mkuu Kichaa, kauli huumba, hata mtu kama ulikuwa mzima kabisa, ukajiita kichaa, kutokana na kuitwa kichaa, ukichaa unakuingia bila wewe kujijua, kwa sababu

Kuwa Kichaa Sio Mpaka Kuokota Makopo!. Jee Tanzania Tuna Vichaa Wengi Kuliko Tunavyojidhania?!. - JamiiForums

Kitendo cha kuliita bandiko hili ni uendawazimu ndio uthibitisho wa ukichaa wako.

Kama unadhani lengo ni kubakisha, subirie yatimie, ndipo tutaelewana, nani mwendawazimu.
Pole na samahani.
P.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…