Baada ya Magufuli, 2025 Makonda atatufaa sana kwasababu ana uthubutu kuliko hata JPM!

Wanabodi,
Kabla Magufuli hajawa rais wetu, sisi wengine wenu tulijua tangu mwaka 2014 na tukasema humu!.Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli

Miongoni mwa sifa zilizomuibua Magufuli ni sifa inayoitwa "uthubutu" unreasonably ambayo wengine huita ni udikiteta. Yaani kuachana na mambo ya kufuata sheria, taratibu na kanuni, ndiyo yametufikisha hapa, hawa viongozi wenye "uthubutu" hawahitaji kujua sheria, taratibu na kanuni, zinataka nini, bali hufanya lile linalowezekana,

Ndio maana tukasema humu, japo Magufuli kweli ni dikiteta, Tanzania mahali ilipofika ilimhitaji mtu kama Magufuli na Mwenyeenzi Mungu akaisikia sala yetu, akatupatia Magufuli!.
Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata!. Atakayeleta Fyoko, Ataisoma Namba!

Tukija kwa Makonda, muda mfupi baada ya kuteuliwa DC wa Kinondoni, akaonyesha uwezo, hivyo kama ilivyokuwa kwa Magufuli, mwaka 2014 tulisema ni Magufuli, na mwaka 2015 kweli akawa yeye. Vivyo hivyo kwa Makonda akiwa DC, akina sisi tukasema hivi Nimemkubali Sana DC Makonda, anafaa kuwa Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam
Na kweli haukupita muda akawa!.

Hivyo kwa hii kazi nzuri yote anayoifanya Magufuli, atakapoondoka ile 2025, kama hatamuachia nchi mtu mwenye kufuata nyayo zake, hii kazi nzuri yote ya Magufuli itakuwa ni kazi bure! . Hivyo nimeshauri Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?

Kwa vile katiba sio Msahafu, 2025 tuibadili katiba Magufuli aendelee indefinitely kama Mugabe, mpaka atakapo choka kabisa na kuwa hawezi tena kwa incapacitation, au tumsubirie Mungu, au Tanzania sasa na sisi tuanze mtindo wa spotting na headhunting na kumfanyia grooming huyo headhunted?.

Kwa maoni yangu Makonda atatufaa sana kumpokea Magufuli, maana kiukweli kwa sababu ana uthubutu mkubwa zaidi kuliko hata Magufuli. Makonda akimpokea Magufuli ile 2025, kiukweli kabisa Tanzania itanyooka!.

Magufuli pamoja na mazuri yake, naye kama binadamu pia ana madhaifu na mapungufu yake, vivyo hivyo Makonda pia sio malaika naye ana mapungufu yake, moja ya mapungufu makubwa ya Makonda ni inferiority complex inayopelekea ku practice superiority complex na kujikuta ana over do things bila kujijua!.

Psychoanalysis: Superiority Complex ni Dalili ya Inferiority Complex!. Maneno Mafupi Vitendo Virefu.

Mfano ni jinsi anavyojikomba komba kwa rais Magufuli mpaka kupindukia, karibu kila jambo lazima amtaje rais Magufuli tena kwa majina yake yote manne na sifa zake zote nne "Rais Wetu Mpendwa Mheshimiwa Dr. John Pombe Joseph Magufuli" (si mnajua watu wa Kanda yetu kwa kupenda masifa). Makonda lazima afike mahali aonyeshe anaweza kusimama on his own na sio kila wakati kutegemea apron strings za rais Magufuli.

Hivyo 2025 rais Magufuli asipoongeza muda, Makonda atatufaa sana. Kwa vile Makonda ni Mkolomije, kwa kuanzia 2020 akalichukue lile jimbo la yule chapombe, pale Kolomije na atashinda kwa kishindo na kupewa moja ya important portfolio zenye impact, ili 2025 ampokee Magufuli.

Kitendo cha mtu wa Kanda ya Ziwa kushika urais kama alivyo rais Magufuli, ni dalili ya Tanzania kutenda haki ya wengi wape, yaani wenye haki na uhalali wa kutawala nchi ni wale walio wengi!. Hivyo baada ya rais Magufuli aje rais Makonda, na baada ya hapo tuendelee kule kule mpaka na makabila mengine nao wawe ni walio wengi ndipo nao watastahiki! .

Makonda konyesha uwezo wa uthubutu, jee mnalionaje hili la kwanini asiwe Makonda kumpokea Magufuli?.

Kwa kwa wale mashabiki wa upinzani mtanisamehe bure, kwenye urais wa Tanzania, upinzani ni bado sana.

Paskali.
Update,
Kumbe wanaoesema baada ya Magufuli, Makonda atatufaa, siko peke yangu,
Msikilize kiongozi huyu wa dini, msikilize mpaka mwisho

Viongozi wakuu wa dini, wanaletwa na MWENYEWE YEYE, hivyo baada ya kuisikia kauli kama hiyo ya kiongozi wako wa dini, wewe kama ni muumini safi na wa kweli, ni kuikubali, hiyo ni sauti ya Mungu ikinena kupitia vinywa vya Manabii, wewe ni nani upinge?.
P
Kama mwanahabari wa tabia hizi. Basi niseme tu hakuna Kama Tundu lissu
 
Mkuu othuman dan fodio, baadhi ya mabandiko yangu, ni mabandiko mahsus kwa watu mahsus na yana ujumbe mahsus kwa hao walengwa tuu, kwa lengo la kufikisha ujumbe huko kunako, hivyo kuyasoma kichwa kichwa, utaishia kuingia chaka!. Hebu soma huku umetulia, soma mstari kwa mstari, nimekufupishia, usipoelewa nilikuwa namaanisha nini, then bandiko langu kama hili
Elections 2015 - Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli mtu kama wewe ndio utatoka kapa kabisa!, empty with nothing !.
P
Wenye akili wanakuelewa sana.

Bahati mbaya wapo wanaodhani unajipendekeza wakati sijawahi kuona popote ukifanya hivyo
 
Tumekuelewa lakini haya ndio mambo yamekunyima tunzo ya heshima hapa JF na badala yake ametunukiwa Mzee Mohammed Said.

Ulistahili tunzo kwa mchango wako wa muda mrefu hapa JF lakini kosa la kupanda treni ya wasukuma ndio iliondoa sehemu ya credibility yako na kupuuzwa, jiulize hivi ni kwa nini Mzee Mwanakijiji naye haeshimiki tena? Hata tuzo za JF wala hajafikiriwa?

Wewe na Mzee Mwanakujiji mjiangalie mliojikwaa, jirekebisheni tusonge mbele, na hapa sina maana kuunga mkono upinzani hapana bali kumpendekeza Msukuma baada ya msukuma halafu wote makatili, ilikuwa ni zaidi ya ukabila na kujipendekeza.
Mkuu Matola, kwanza asante kwa post hii, nimeipenda objetivity yako na ushauri wako nitauzingatia.

Tukija kwenye uandishi humu jf kwa maana haswa ya uandishi, JF tunaye mwandishi mmoja tuu, the one and only Maalim Mohamed Said , kunilinganisha nae ni kutaka kunivimbisha kichwa kwa kilemba cha ukoka!.

Hapo nyuma pia Mkuu Mzee Mwanakijiji ndie mwandishi wa kwanza humu, he deserves recognitation. Mimi humu JF sio mwandishi kivile bali ni mchokoza mada tuu, ila hakuna yoyote kati yetu anaandika jf ili kupata tuzo, tunaandika just for the love of it, hivyo with tuzo or without tuzo tutaendelea kuandika and expresing our opinions the way we feel na sio kuandika vitu watu wanataka au kumfurahisha mode ili next time tusikose tuzo.

Mimi kwa upande wangu, sijajikwaa popote, the respect I command in jf, is just enough and its more than tuzo yoyote, kitendo cha JF modes kuni recognize as the one and only "Kada wa Chama Cha Mapinduzi"
ni recognitation tosha.

P
 
Japo jf was meant to be a home to Great Minds, as days go by, ma GT wa ukweli wa Jeiefu, wanazidi kupungua huku average people wakiongezeka kwa wingi na miongoni mwao, vilaza ni wengi na sasa ndio wanatamalaki zaidi humu jeiefu, hivvo mtu ukipandisha bandiko kama hili linalohitaji uwezo wa to read in between the lines wengi wanatoka kapa na wengine kuishia chaka, hivyo nikipata muda nitakuwa naendesha darasa la to read in between the lines, hivyo kuwaa transform from hawa average jf members from ordinary into great mind.

Hapo nimetoa somo la kufuata katiba sheria, taratibu na kanuni.

Hapo kuna kitu nilimtaja Mungu na kweli Mungu akatenda.

Hapa nimezungumzia Tanzania kunyooka

Kujikomba komba kulipungua

Hii pia ilipungua

Hili alishindwa

Kuna kitu nilikisema hapo...

Natumaini nimeeleweka.
P

Aisee. I sympathize with you brother. Usihangaike sana. Bila shaka sasa unauona uharibifu mkubwa uliofanywa na unaoendelea kufanywa na chama dola ambacho ulijiunga kupambania ubunge wa Kawe. Sijui napo tusome btl ili kuelewa nini hasa lilikuwa kusudio lako? Anyway, mfumo wetu haujengi uwezo na subira inayohitajika katika critical analysis hasa masuala ya hali halisi ya maisha yetu yanapoguswa.

Dola awamu ya tano ilitibua watu wengi sana hata wasiotarajia kiasi cha kuua kabisa “anasa” ya mijadala ya hoja. Watu walikuwa polarised kiasi cha kutoa cheche wakiguswa tu! Watu kama mmkj walibadilika sura kiasi cha kutotambulika tena! JF kama home of great thinkers ilivamiwa na vikosi lukuki vya LB7 na MATAGA kiasi cha kuigeuza kuwa Facebook na Instagram za matineja! Baadhi ya wahenga wanaotegemewa kwa hoja nzito nao waliishia kujiunga na hayo makundi ya praise & worship.

Kiongozi mkuu wa nchi ndiye alikuwa akiongoza kwa kumwagia watu “shombo” tena baada ya kuwafanyia ubandido wa waziwazi. Sabaya & Makonda walikuwa ndio kielelezo cha modus operandi ya awamu ile. Na ndio walikuwa masterling wakihanikizwa na mpiga zumari wao msiba!

Sasa wewe unaleta falsafa zako kanganyizi halafu unatarajia watu wawe na muda na subira ya kusoma kati kati ya mistari ili waipate maana halisi? Kwa “anasa” ipi waliyokuwa nayo chini ya utawala ule wa jiwe? Hata sasa chini ya SSH bado hawajarecover. Endelea tu kubomoa codes mwenyewe ueleweke hakuna namna. Bahati nzuri jiwe hayupo na yake hayapo tena. Ama sivyo Dodoma 2.0 ingekuhusu. This is Tanzania. You have my sympathies, sincerely.
 
Tumekuelewa lakini haya ndio mambo yamekunyima tunzo ya heshima hapa JF na badala yake ametunukiwa Mzee Mohammed Said.

Ulistahili tunzo kwa mchango wako wa muda mrefu hapa JF lakini kosa la kupanda treni ya wasukuma ndio iliondoa sehemu ya credibility yako na kupuuzwa, jiulize hivi ni kwa nini Mzee Mwanakijiji naye haeshimiki tena? Hata tuzo za JF wala hajafikiriwa?

Wewe na Mzee Mwanakujiji mjiangalie mliojikwaa, jirekebisheni tusonge mbele, na hapa sina maana kuunga mkono upinzani hapana bali kumpendekeza Msukuma baada ya msukuma halafu wote makatili, ilikuwa ni zaidi ya ukabila na kujipendekeza.

Not fair. In all honesty, Mayala alikuwa na ni tofauti kabisa na mmkj. Tatizo lake lugha aliyochagua kuandikia ilikuwa “mbaya” sana. Haikuwa na “wasomaji”. Too codified.
 
Japo jf was meant to be a home to Great Minds, as days go by, ma GT wa ukweli wa Jeiefu, wanazidi kupungua huku average people wakiongezeka kwa wingi na miongoni mwao, vilaza ni wengi na sasa ndio wanatamalaki zaidi humu jeiefu, hivvo mtu ukipandisha bandiko kama hili linalohitaji uwezo wa to read in between the lines wengi wanatoka kapa na wengine kuishia chaka, hivyo nikipata muda nitakuwa naendesha darasa la to read in between the lines, hivyo kuwaa transform from hawa average jf members from ordinary into great mind.

Hapo nimetoa somo la kufuata katiba sheria, taratibu na kanuni.

Hapo kuna kitu nilimtaja Mungu na kweli Mungu akatenda.

Hapa nimezungumzia Tanzania kunyooka

Kujikomba komba kulipungua

Hii pia ilipungua

Hili alishindwa

Kuna kitu nilikisema hapo...

Natumaini nimeeleweka.
P
Eee bwana Mayalla naona unajisafisha kwa Dodoki lililokatwa Kwa chandarua Cha msaada wa hisani ya Watu wa Marekani!

Mayalla mara ngapi umekikana kivuli chako humu ndani?

Haya endelea na tabia zako hizo hata hua hujifunzi kwamba Unafiki haufichiki hata ukiuficha ndani ya vazi la chupi!

The terrible!
 
Wanabodi,
Kabla Magufuli hajawa rais wetu, sisi wengine wenu tulijua tangu mwaka 2014 na tukasema humu!.Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli

Miongoni mwa sifa zilizomuibua Magufuli ni sifa inayoitwa "uthubutu" unreasonably ambayo wengine huita ni udikiteta. Yaani kuachana na mambo ya kufuata sheria, taratibu na kanuni, ndiyo yametufikisha hapa, hawa viongozi wenye "uthubutu" hawahitaji kujua sheria, taratibu na kanuni, zinataka nini, bali hufanya lile linalowezekana,

Ndio maana tukasema humu, japo Magufuli kweli ni dikiteta, Tanzania mahali ilipofika ilimhitaji mtu kama Magufuli na Mwenyeenzi Mungu akaisikia sala yetu, akatupatia Magufuli!.
Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata!. Atakayeleta Fyoko, Ataisoma Namba!

Tukija kwa Makonda, muda mfupi baada ya kuteuliwa DC wa Kinondoni, akaonyesha uwezo, hivyo kama ilivyokuwa kwa Magufuli, mwaka 2014 tulisema ni Magufuli, na mwaka 2015 kweli akawa yeye. Vivyo hivyo kwa Makonda akiwa DC, akina sisi tukasema hivi Nimemkubali Sana DC Makonda, anafaa kuwa Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam
Na kweli haukupita muda akawa!.

Hivyo kwa hii kazi nzuri yote anayoifanya Magufuli, atakapoondoka ile 2025, kama hatamuachia nchi mtu mwenye kufuata nyayo zake, hii kazi nzuri yote ya Magufuli itakuwa ni kazi bure! . Hivyo nimeshauri Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?

Kwa vile katiba sio Msahafu, 2025 tuibadili katiba Magufuli aendelee indefinitely kama Mugabe, mpaka atakapo choka kabisa na kuwa hawezi tena kwa incapacitation, au tumsubirie Mungu, au Tanzania sasa na sisi tuanze mtindo wa spotting na headhunting na kumfanyia grooming huyo headhunted?.

Kwa maoni yangu Makonda atatufaa sana kumpokea Magufuli, maana kiukweli kwa sababu ana uthubutu mkubwa zaidi kuliko hata Magufuli. Makonda akimpokea Magufuli ile 2025, kiukweli kabisa Tanzania itanyooka!.

Magufuli pamoja na mazuri yake, naye kama binadamu pia ana madhaifu na mapungufu yake, vivyo hivyo Makonda pia sio malaika naye ana mapungufu yake, moja ya mapungufu makubwa ya Makonda ni inferiority complex inayopelekea ku practice superiority complex na kujikuta ana over do things bila kujijua!.

Psychoanalysis: Superiority Complex ni Dalili ya Inferiority Complex!. Maneno Mafupi Vitendo Virefu.

Mfano ni jinsi anavyojikomba komba kwa rais Magufuli mpaka kupindukia, karibu kila jambo lazima amtaje rais Magufuli tena kwa majina yake yote manne na sifa zake zote nne "Rais Wetu Mpendwa Mheshimiwa Dr. John Pombe Joseph Magufuli" (si mnajua watu wa Kanda yetu kwa kupenda masifa). Makonda lazima afike mahali aonyeshe anaweza kusimama on his own na sio kila wakati kutegemea apron strings za rais Magufuli.

Hivyo 2025 rais Magufuli asipoongeza muda, Makonda atatufaa sana. Kwa vile Makonda ni Mkolomije, kwa kuanzia 2020 akalichukue lile jimbo la yule chapombe, pale Kolomije na atashinda kwa kishindo na kupewa moja ya important portfolio zenye impact, ili 2025 ampokee Magufuli.

Kitendo cha mtu wa Kanda ya Ziwa kushika urais kama alivyo rais Magufuli, ni dalili ya Tanzania kutenda haki ya wengi wape, yaani wenye haki na uhalali wa kutawala nchi ni wale walio wengi!. Hivyo baada ya rais Magufuli aje rais Makonda, na baada ya hapo tuendelee kule kule mpaka na makabila mengine nao wawe ni walio wengi ndipo nao watastahiki! .

Makonda konyesha uwezo wa uthubutu, jee mnalionaje hili la kwanini asiwe Makonda kumpokea Magufuli?.

Kwa kwa wale mashabiki wa upinzani mtanisamehe bure, kwenye urais wa Tanzania, upinzani ni bado sana.

Paskali.
Update,
Kumbe wanaoesema baada ya Magufuli, Makonda atatufaa, siko peke yangu,
Msikilize kiongozi huyu wa dini, msikilize mpaka mwisho

Viongozi wakuu wa dini, wanaletwa na MWENYEWE YEYE, hivyo baada ya kuisikia kauli kama hiyo ya kiongozi wako wa dini, wewe kama ni muumini safi na wa kweli, ni kuikubali, hiyo ni sauti ya Mungu ikinena kupitia vinywa vya Manabii, wewe ni nani upinge?.
P

Ila Paschal 🤣🤣🤣 maisha haya
 
Huyu mtoa mada ndiye aliyesema Makonda anafaa kua rais wa nchi hii,. Kweli huyu mayala mayala yanamsumbua mpaka kwenye ubongo
Mkuu Robidinyo , hili bandiko linakuhusu, mkiitwa vilaza mnalalamika!.
Nenda kalisome tena bandiko hili huku ukishirikisha ubongo wako, only if kwenye kichwa chako kuna ubongo
Lakini kama unajijua kichwani ni an empty shell, please just save your time.
P
 
Hivi hapa Mkuu ukifikiria nini?? Au nikipindi anavuma ukaona anafaa kuongoza taifa la watu 60ml? Au mlikuwa washikaji nawewe kunakitubulikuwa unapalilia tuwe wakweli.
 
Duh...!. Hata wewe KakaKiiza , mutu ta Tahajudi umeshindwa kweli kabisa kunisoma?. Unisome huku umetulia kwa kushirikisha medulla oblingata yako!.
P
 
Back
Top Bottom