Kuna uwezekano Watanzania tuna tatizo la uelewa? Nikimsikiliza Polepole, namuona Mwl. Nyerere. Nyie msiomuelewa Polepole, je Nyerere mngemuelewa?

Kuna uwezekano Watanzania tuna tatizo la uelewa? Nikimsikiliza Polepole, namuona Mwl. Nyerere. Nyie msiomuelewa Polepole, je Nyerere mngemuelewa?

Wanabodi,

Kuna uwezekano uelewa wa Watanzania walio wengi kuelewa mambo makubwa, ni uelewa finyu, uelewa mdogo, uelewa duni au uelewa wenye mushkeli?. Maana kuna siku niliwahi kuandika makala fulani, kwenye gazeti fulani, kuulizia jambo fulani, tena na alama ya kuuliza ikawekwa!, niliitwa mahali kuhojiwa! Ati nimetoa statement fulani!, Nilipouliza ni statement gani?, mbona nimeuliza swali, nikajibiwa "alama ya kuuliza haikuonekana!

Hii ni kufuatia wengi kutomwelewa Humphrey Polepole. Nikimwangalia Polepole na kumsikiliza kwa makini, namuona kabisa, hii ni reincarnation ya Mwalimu Nyerere! Sasa hawa madogo wengi za sasa ambao hawakumjua Mwalimu, kama Mwalimu angekuwepo, wangemuelewa kweli?

Mbona mimi najiona kama namwelewa sana Polepole!

Hebu msikilize hapa, angalia jinsi anavyoongea.

Ni kama Mwalimu kabisa!

Kwenye ule mkutano wa Mwalimu Nyerere na Waandishi wa Habari, wa Simba Grill, Hoteli ya Kilimajaro, mwaka 1995, mimi nilikuwepo.

Mwalimu alisema kila anapokwenda, anatembea na vijitabu viwili, Biblia na Azimio la Arusha. Sasa kila akilisoma Azimio la Arusha, haoni kosa lolote. Serikali ya awamu ya pili ililifuta Azimio la Arusha, ikapitisha Azimio la Zanzibar. Mwalimu askasema, "serikali yetu imefanya mazuri na mengine ya kijinga!, akashangaa, awamu iliyofuata, imeyaacha mazuri kama miiko ya Uongozi kwenye Azimio la Arusha, na kukumbatia ya kijinga"

Watu wasichoelewa kumhusu Polepole ni nini haswa?

Paskali
Update

Naunga mkono hoja, japo nimeishi Msasani jirani na kwa Nyerere, pale kwa Nyerere kwetu was a playing ground, japo nimesali St. Peters ambalo ni kanisa la Nyerere na alikuwa anasali misa ya asubuhi daily, lakini ni kweli naweza nisimfahamu Nyerere hivyo kuhitaji kumfahamu zaidi, na ili umfahamu mtu ni lazima ama uzungumze naye ama umuulizie taarifa zake. Thanks God kwa upande wangu I did both, nimezungumza na Nyerere, nimefanya nae mahojiano, hivyo kwa kiasi changu namfahamu Nyerere, na nimemzunguza sana tuu humu.

Mtu kufanana na mtu mwingine, sio lazima wafanane kila kitu, wanaweza kufanana mawazo, matendo, maneno, misimamo, tabia, etc. Polepole, anafanana na Nyerere kwa kuongea, anaongea kama Nyerere, ana kichwa kama cha Nyerere, hata umbo kama la Nyerere, he jokes kama Nyerere, nadhani he is intelligent kama Nyerere! Japo tuna viongozi wengi , sii wote ni viongozi intelligent kama Nyerere, Polepole is, lakini ukiwa huna intelligence ya kumwelewa Polepole, then Nyerere ndio kabisa!

Mengine yoote wafananishe lakini, fahamu kuanzia leo kuwa misimamo ya Mwalimu Nyerere haikuwa SEASONALLY.
Maana yake, wakati anacho au ana uwezo wowote na wakati hana au hana uwezo wowote.

Kwa fikra na matendo yake:
1: Polepole wa bunge la katiba alikuwa tofauti na 👇
2: Polepole wa utawala wa Mh. Magufuli, nae Polepole huyo yuko tofauti katika misingi hiyo na 👇
3: Polepole wakati wa utawala wa Mh. Samia 👇
4: Tutarajia Polepole mwingine ajaye??

Tafakari kwa kina.
 
Wanabodi,

Kuna uwezekano uelewa wa Watanzania walio wengi kuelewa mambo makubwa, ni uelewa finyu, uelewa mdogo, uelewa duni au uelewa wenye mushkeli?. Maana kuna siku niliwahi kuandika makala fulani, kwenye gazeti fulani, kuulizia jambo fulani, tena na alama ya kuuliza ikawekwa!, niliitwa mahali kuhojiwa! Ati nimetoa statement fulani!, Nilipouliza ni statement gani?, mbona nimeuliza swali, nikajibiwa "alama ya kuuliza haikuonekana!

Hii ni kufuatia wengi kutomwelewa Humphrey Polepole. Nikimwangalia Polepole na kumsikiliza kwa makini, namuona kabisa, hii ni reincarnation ya Mwalimu Nyerere! Sasa hawa madogo wengi za sasa ambao hawakumjua Mwalimu, kama Mwalimu angekuwepo, wangemuelewa kweli?

Mbona mimi najiona kama namwelewa sana Polepole!

Hebu msikilize hapa, angalia jinsi anavyoongea.

Ni kama Mwalimu kabisa!

Kwenye ule mkutano wa Mwalimu Nyerere na Waandishi wa Habari, wa Simba Grill, Hoteli ya Kilimajaro, mwaka 1995, mimi nilikuwepo.

Mwalimu alisema kila anapokwenda, anatembea na vijitabu viwili, Biblia na Azimio la Arusha. Sasa kila akilisoma Azimio la Arusha, haoni kosa lolote. Serikali ya awamu ya pili ililifuta Azimio la Arusha, ikapitisha Azimio la Zanzibar. Mwalimu askasema, "serikali yetu imefanya mazuri na mengine ya kijinga!, akashangaa, awamu iliyofuata, imeyaacha mazuri kama miiko ya Uongozi kwenye Azimio la Arusha, na kukumbatia ya kijinga"

Watu wasichoelewa kumhusu Polepole ni nini haswa?

Paskali
Update

Naunga mkono hoja, japo nimeishi Msasani jirani na kwa Nyerere, pale kwa Nyerere kwetu was a playing ground, japo nimesali St. Peters ambalo ni kanisa la Nyerere na alikuwa anasali misa ya asubuhi daily, lakini ni kweli naweza nisimfahamu Nyerere hivyo kuhitaji kumfahamu zaidi, na ili umfahamu mtu ni lazima ama uzungumze naye ama umuulizie taarifa zake. Thanks God kwa upande wangu I did both, nimezungumza na Nyerere, nimefanya nae mahojiano, hivyo kwa kiasi changu namfahamu Nyerere, na nimemzunguza sana tuu humu.

Mtu kufanana na mtu mwingine, sio lazima wafanane kila kitu, wanaweza kufanana mawazo, matendo, maneno, misimamo, tabia, etc. Polepole, anafanana na Nyerere kwa kuongea, anaongea kama Nyerere, ana kichwa kama cha Nyerere, hata umbo kama la Nyerere, he jokes kama Nyerere, nadhani he is intelligent kama Nyerere! Japo tuna viongozi wengi , sii wote ni viongozi intelligent kama Nyerere, Polepole is, lakini ukiwa huna intelligence ya kumwelewa Polepole, then Nyerere ndio kabisa!

Kama ulivyokwisha kusema kua watanzania tuna matatizo yakutoelewa.. naam ni imani yangu kubwa kua na wewe ni Mtanzania ndio maana unathubutu kumtukana Mwl. Nyerere kwa kumfananisha na mwanasiasa wa hovyo kama Polepole.

Mwl alieichukua nchi ikiwa kwenye mfumo wa chama kimoja ila alivumilia kuona ikiwa ya vyama vingi leo hii hawa wahuni wachache wanaotamani kuangamiza mifumo ya ki demokrasia na hata kuua upinzani na kunyamazisha wanaohoji ndio unadhubutu kuwafananisha na waasisi wa hili taifa?

Tuongeeni kwenye uhalisia mnadhani hiki kizazi cha nne na cha tano cha siasa za tanzania kama nchi ingrkua iko bado kwenye mfumo wa chama kimoja hawa wenaosema wanashuhulikia wahuni unadhani wangeachia nchi? Na ikulu ingejengwa kanda ya ziwa walah
 
Paskali kabla ya Polepole kuendelea kutupigia kelele aseme kwanza kwanini alitaka watu wanyamaze walipokuwa wakinyoosha nchi na sasa kwa nini yeye hataki kunyamaza wenzake wanapofungua nchi?

Haki ya kuongea anaitoa wapi ilihali wao hawakutaka wengine wapate haki hiyo alipokuwa akizunguka na Vee Eiteh?
@paskali mayala
 
Yan mtu ambaye juzi tu hapa alikuwa injinia wa biadhara chafu ya kununua vijana wa kitanzania, akitumia kodi zetu tunazozitoa kwa jasho jingi, lengo ili aue demokrasia na uhuru wa nchi hii, leo analilia demekrasia na uhuru!! Huu si ukasuku? Unamlinganisha Mwalimu wa nchi hii na kiroboto?!! Hiv mwalimu angeweza kutumia pesa za walipa kodi kuwanunua wanasiasa?!!!! Wewe pasikali wewe?!!!!
ndo maana nikasema watanzania wana ugonjwa wa kusahau. wameshasahau yote, kumbe ni mwaka jana tu hapa kulikuwa na uchaguzi.
 
Polepole sio mjamaa wala hajui ujamaa, ni msaka tonge kwa kutumia kalamu yake.

Nyerere aliwafananisha na mercenaries yaani mamluki. Yeye anafuata dau tu ndio unakuwa msimamo wake"He who pays the piper calls the tune".

Anachofanya sasa hivi ni sampuli ya kinyonga, ila anasahau kubadirisha misamamo hakubarishi genetical make up yake.
 
Tukichukulia watu zaidi ya milion 60 watanzania na wewe mtu mmoja ambaye ata elimu yako siielewi tuachilie mbali elimu ata maadili yako si ya watanzania walio wengi ya kutukana watu hovyo. Jitafakali taifa lina watu wengi ambao kila mmoja anataka fursa sawa sio la watu wachache wanaojiona wao ndo wanastahili kula keki ya taifa na wajukuu zao.watanzania tunahitaji maji,umeme,shule nzuri,reli za kisasa kama sgr na vyote hivyo polepole na magufuli ndo yalikuwa malengo yao makuu na leo ndo una mmwita mpumbavu time will tel u

Sent from my SM-T355Y using JamiiForums mobile app
Hakuna shetani mwema kwa binadamu, hao wote uliowataja ni mashetani tu.
 
Huyu mtoa mada ndiye aliyesema Makonda anafaa kua rais wa nchi hii,. Kweli huyu mayala mayala yanamsumbua mpaka kwenye ubongo
Mkuu Robidinyo , hili bandiko linakuhusu, mkiitwa vilaza mnalalamika!.
Nenda kalisome tena bandiko hili huku ukishirikisha ubongo wako, only if kwenye kichwa chako kuna ubongo
Lakini kama unajijua kichwani ni an empty shell, please just save your time, don't!.
P
 
Dikteta alituambia mayala maana yake ni njaa
 
...alituambia mayala maana yake ni njaa
Ni kweli, ila sio njaa za tumbo inayohitaji shibe ya chakula ni baa la njaa, drought, famine, iliyosababishwa na ukame, inayohitaji mvua!. Alhamdidulahi, sasa mvua zimeanza kuonyesha!, maana...
P
 
Ukiwa mwanasiasa muda mwingine unalazimika tu kujifanya huna akili kumbe unazo, hii hoja ya Pasco ni mojawapo ya hoja za hovyo, zenye upofu na upogo, na utovu mwingi wa nidhamu!
Tangu siku ile aliyochukuwa fomu za ccm kugombea ubunge wa Kawe ndipo nilipopata jibu sahihi kuna tatizo kwenye halmashauri ya ubongo wa Paskal.

Atuombe radhi Watanzania, hii ni kejeri za makusudi na dharau kwa Baba wa Taifa.

Magufuli na ukichaa wake wote hakuwahi kujifananisha na Baba wa Taifa.
 
imagine, haujawahi kua mbunge tangu uzaliwe, Rais Samia anakuteua ubunge wa bure ambao hata sio wa kupigiwa kura, unakula mshahara na marupurupu, usafiri everything, afu siku moja from nowhere unasikika ukiutangazia umma kwamba, wakitaka kukupora ubunge wachukue tu hauwaogopi. hivi kuna wangapi wangepewa nafasi yako hiyo ambao wangekuwa hata na adabu? wakati huo yule aliyekuteua hajakujibu wala nini na ni mtu mwenye mamlaka makubwa. vijana ndio maana wanashindwa kuaminiwa. vigeugeu sana.
 
Pascal mayala anaona mbali...one dei the team will rise and the dead will arise again
 
Vip mkuu kampeni za kumfanya homeboy kolomije boy awe prezidaa wa sita wa wadanganyika zimefikia wap??!!
Ahaa... kumbe na wewe uko kundi la vila...?!. Kanisome tena huku ukishirikisha ubongo wako!.
P
 
Ahaa... kumbe na wewe uko kundi la vila...?!. Kanisome tena huku ukishirikisha ubongo wako!.
P
Nimesoma mkuu; kwamba homeboy kolomije ni mdhubutu kuliko hata dikteta hivyo ndo mwenye sifa ya kuwa lais wa 6; kama hiyo haitoshi kiloboto ana akili kama nyelele (au pengine kumzidi?!!); vip unapendekeza kiloboto awe lais wetu wa 7 baada ya homeboy kolomije?!! Kwa sababu wachunga ngombe ndo wengi basi ndo wenye haki ya kutawara mpaka hapo maeneo mengine nako watakapokuwa wengi... Duh! Ila ma homu boizi mna loho ngumuuuu!!!!
 
Sijui kwa nini Pasco, kila mara, watu waovu, yeye anaona ndio wanaofaa kuwa viongozi.

Habari za ndani kabisa ni kwamba Polepole ndiye aliyekuwa akiandaa majina ya watu wanaotakiwa kushughulikiwa na watu wasiojulikana. Walitekwa na kurundikwa chumba kimoja cha mateso, ghorofa ya 5, ofisi ndogo Lumumba. Baada ya mateso makali ama walikabidhiwa polisi au wasiojulikana waliwachukua, na baada ya hapo, kuonekana kwao ilikuwa ni maajaliwa.
 
Back
Top Bottom