Baada ya Mahakama kusema Polisi hawajawashikilia akina Soka Malisa aandika haya

Nawaza kusema vijana waachane na siasa.

Ona sasa, watu wanapotea hii inaleta simanzi kwa wazazi, misiba isiyojulikana.

Akina Mbowe wao wapo tu .

Una lawama za kijinga kweli. Serikali wamteke soka ila lawama unawapa akina Mbowe. Kwa akili hizi ndio maana hata bunge halina huruma na wananchi hata watekwe wote. Maana wanajua wote vilaza.
 
Labda hao wavunja sheria kama wewe mbona watz tuko salama tu. Nenda SA au hapo Kenya tu uone hali ya usalama ilivyo mbaya. Acheni siasa zenu uchwara.

Siasa uchwara unazo wewe. Watu wanaongelea Tanzania wewe unaleta mifano ya Kenya. Halafu mtu useme hao watu mia moja waliopotea walifanya makosa gani?. Maana unaongea kana kwamba hao sio raia wa Tanzania.
 
Kuna siku wataingia mtaa ambao raia wake hawatakubali na ndipo watakapojitambulisha.
 
Kwani wanaingia kila mtaa?
Hawaji kama majini. Huwa wanashuhudiwa na majirani, ndugu na marafiki na wanaachwa tu waondoke na mhusika.
 
Yule tajiri wa mwanza Zakaria aliwavunja miguu kwa risasi ndio baadae inakuja kujulikana ni askari kanzu, watu tembeeni na mapanga, kuna video inasambaa mtandaoni jamaa kenya huko alikamatwa kienyeji akapiga kelele watu wakajaa watekaji(ambao ni askari) wakawa hawana la kufanya, USIKUBALI KWENDA POPOTE BILA KUONA KITAMBULISHO WALA NGUO ZA POLICE
Story ya uongo hii
Zakaria hsjawahi kuvunja watu miguu kwa risasi
 
Labda hao wavunja sheria kama wewe mbona watz tuko salama tu. Nenda SA au hapo Kenya tu uone hali ya usalama ilivyo mbaya. Acheni siasa zenu uchwara.
Wamevunja sheria gani kima wewe
 
Ukweli ni huu ! kufanya siasa kwa africa kama haupati maslahi ni hatari sana kwa maisha yako , hasa nyie chipukizi .

Ukweli tutaendelea kusema kama hauna maslahi na watu wakubwa kukulinda tafuta dili nyingine .

Mnafanya siasa zenu kama sehemu za maslahi , mkitekwa mnajifanya anatafuta pulic sympathy hayo ndio maisha mliyochagua .
 
Jana Mahakama Kuu ya Tanzania, imesema kwamba Polisi haijawashikilia Deus Soka na wenzie wawili (Frank Mbise na Jacob Mlay) wanaodaiwa kutekwa maeneo ya Yombo Buza, na watu wenye silaha kwa kutumia gari aina ya Toyota Noah. Hukumu hiyo ilitolewa na Jaji Wilson Dyansobera ambaye alisema Mahakama imejiridhisha kuwa vijana hao watatu hawapo Polisi na hivyo kutaka Polisi iwatafute.

Hukumu hii imeleta simanzi kubwa kwa ndugu wa vijana hawa, na wapenda haki wote nchini. Lakini pia imeset "precedence" kwa matukio ya utekwaji na watu kupotea;

1. Hukumu hii inamaanisha ukifuatwa mtaani na watu wasio na sare za Polisi, vitambulisho na arrest warranty usikubali kwenda. Pambania uhai wako, bora wakuulie hapo ulipo kuliko wakupeleke huko wanakotaka. Kwa lugha rahisi bora ufie nyumbani ndugu zako watakuzika, kuliko ukafie pasipojulikana na ndugu zako wasione hata maiti yako.

2. Hukumu hii inamaanisha baadhi ya Polisi wenye "nia ovu" wanaweza kukukamata na baadae wakakanusha sio wao na usiwe na la kufanya. Na mahakama itakosa ushahidi wa kuwatia hatiani.

Pia soma: Mahakama yaamuru Polisi kuwatafuta viongozi wa BAVICHA (kina Deusdedith Soka) waliopotea

3. Hukumu hii inamaanisha kwamba Tanzania kuna genge la kuteka watu ambalo sio sehemu ya jeshi la Polisi. Kama Mahakama inakubali kuwa akina Soka "walitekwa" lakini sio na polisi, it means mahakama inakubali genge la utekaji lipo. Je genge hilo limeundwa na nani? Linamtumikia nani? Kwa maslai gani?

4. Hukumu hii inamaanisha kuwa vyombo rasmi vya ulinzi vipo dhaifu kiasi kwamba raia wanaweza kutekwa kwenye nchi yao na "genge la watu wasiojulikana" na Polisi wasiweze kuzuia.

5. Hukumu hii inamaanisha usalama wa wakosoaji wa serikali upo mashakani. Hivyo basi usitembee peke yako. Kama wewe ni mkosoaji wa serikali hakikisha hukai kifala.

NB: Ni bahati mbaya haya yote yanafanyika katika nchi inayojinasibu kuheshimu uhuru wa maoni na utawala wa sheria. Ni bahati mbaya zaidi kuwa Waziri wa mambo ya ndani anajisifia kuwa nchi ipo salama wakati kuna watu wanadaiwa kutekwa na kupotezwa na hakuna hatua za maana zinazochukuliwa kukomesha vitendo hivi!
Walebmnaobsemabsiasa haziwahusu sasa ndio mjuwa kama haziwahusu mtatawaliwa na wajinga ambao ambao wataruhusu utekaji na kupoteza watu kuwa sehemu ya siasa. Nchi

Nchi yetu ipo mikononi mwa majambazi na washezi. Vitu serious kama uhai wa watu vinachukuliwa kimzaha mzaha. Halafu vitu vya kijinga vinaonekana vya maana . Raisi anaonekana kwenye tamasha za burudani . Ila kwenye issues za kitaifa anaziita ni drama.
 
Story ya uongo hii
Zakaria hsjawahi kuvunja watu miguu kwa risasi
Aisee

aisee muda mwingine uwe unajaribu kuficha upuuz wako mkuu, hii hapa nini

Naona harufu mbaya ya watu Fulani kujiteka Ili kupata mileage lawama kwa serikali!

Serikali haiwezi fanya kazi kiboyoboya hivyo.
 
This is tricky.

Wanaweza kukufungulia kesi ya uhaini kwa kushambulia serikali, adhabu yake nadhan ni kifo au maisha jela
Kama mahakama na bunge wanawakana huku polisi wakiruka moja kwa moja ni wahalifu.
Halafu wakishafanyiziwa Kila mtu atafute hifadhi yake vinginevyo tutabaki watu wa kulalamika.
 
Back
Top Bottom